Nifanyeje niache ARV?

sinajinasasa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
2,989
4,129
Wana JF!!

Samahani sana, naomba msaada wenu, najua mpo wengi wenye uelewa wa mambo.
Sasa naomba kuelimishwa, pia kwa faida ya wengine wenye matatizo kama yangu.
Nipo hapa kwa niaba ya kaka yangu ambaye alipima na kuonekana ana '' HIV" mwaka 2011 mara moja wakamuanzishia matibabu ya ARV. Hakuwa na shida nyingine, zaidi ya kuwa na constipation..hakuwa anakula vizuri baada ya kufilisika duka lake, akawa anafanya kazi ngumu bila kula vizuri zaidi ya chapati tena zilizokobolewa unga. Kutokana na kudhoofika afya nilimpeleka hospitali na alipopima HIV alionekana HIV+ , lakini cha ajabu mke wake ni HIV- ni muda mrefu sasa.

Sasa huyu kaka yangu pamoja na kuwa anakunywa hizo dawa, naona sasa zinamdhuru hasa ngozi yake inakuwa na spots, ambapo juzi tu wakampa madawa ya TB wakati hana hiyo TB, dawa zikamdhuru hadi mdomo unababuka ngozi. Bado anaendelea na kazi yake ya kilimo cha bustani na pia boda boda, physically hayupo vibaya sana.

Kutokana na elimu niliyoipata humu hasa ile thread ya V.V.U na Upimaji wake, nimegundua huyu bro hana ngoma, ila labda ni lishe bora tu na life style mbovu.
Kwa vile ameshakuwa mhanga wa ARV nifanyeje ili nimuachishe dawa hizo bila kumletea madhara, aweze kurudia hali yake ya kawaida. Naogopa nisije kumshawishi aache akaanza kuumwa nikalaumiwa mimi.

Naomba ushauri kama akiacha ARV atumie nini, ambacho kitamfanya awe Normal?

CC: Kaveli, Deception
 
Ushauri wangu aendelee na hizo dawa kama dr alivyoshauri maana hapa kupishana na vipimo vya maabara sio poa ila kikubwa jitaid apate mlo kamili na pia apunguze kazi za kilimo ni bora apige bodaboda na pia apate muda mwing wa kupumzika na apunguze mawazo nadhani baada ya muda utaona mabadiliko makubwa matunda mboga za majani maji mengi anywe vyakula vyenye wanga
 
Kwanza kabisa naomba tukubaliane kama vipimo vilisoma postv inamaanisha anamaambukiz ya VVU!

Mtu akishaanza kutumia ARV haruhusiw kuacha kwa namna yoyte ile namaanisha ataendelea kutumia kwa maisha yake yote. Na hiz dawa zmegawanyika kimistari kuna mstari wa kwanza na mstari wa pili ambapo kila mstari unadawa kadhaa ambapo mgonjwa akipata madhari ya dawa moja wapo bas anahamishiwa kwny dawa mbadala ktk mstari huo huo anaotumia..

Kwa kawaida wanaanzishiwa msta
ri wa kwanza kama ikishindkana ndio anahamishiwa kwny dawa za mstari wa pili na ukishndkana mstari wa pili ndio bas tena..
Sasa hawa wadudu wanapata usugu kwa haraka sana tofaut na wadudu wa magonjwa mengne na ndio maana mtu akishaanza kutumia dawa hatakiw kuacha na kama akiacha atakapoanza tena upya atabadilishiwa kwnda kwny mstari wa pili kitu ambacho kinamuweka kwny hatar ya kumaliza dawa zote na kama akishndwa kurespond vzr kwny mstari wa pili tutakosa dawa ya kumpa.. Naomba umshaur asiache dawa kama amereact vbaya kwny hyo anayotumia aongee na daktari wake atabadilishiwa kulingana na mwongozo uliopo.

Kuhusu dawa za TB.. Hizo waathirika wote hupewa kama kinga kutokana na wao kuwa kwny hatar kubwa ya kupata maaambkiz ya tb hvyo ataztumia hzo kwa miez6 baada ya hapo atakuja kurudia tena baada ya miaka3 kama itahitajika. Kama na hiz zinamletea madhara mrudshe kwny clinic yake atapewa pyridoxine vit B6 kuzuia hayo madhara ya dawa za TB haswa isoniazide
 
Wana JF!!

Samahani sana, naomba msaada wenu, najua mpo wengi wenye uelewa wa mambo.
Sasa naomba kuelimishwa, pia kwa faida ya wengine wenye matatizo kama yangu.
Nipo hapa kwa niaba ya kaka yangu ambaye alipima na kuonekana ana '' HIV" mwaka 2011 mara moja wakamuanzishia matibabu ya ARV. Hakuwa na shida nyingine, zaidi ya kuwa na constipation..hakuwa anakula vizuri baada ya kufilisika duka lake, akawa anafanya kazi ngumu bila kula vizuri zaidi ya chapati tena zilizokobolewa unga. Kutokana na kudhoofika afya nilimpeleka hospitali na alipopima HIV alionekana HIV+ , lakini cha ajabu mke wake ni HIV- ni muda mrefu sasa.
Sasa huyu kaka yangu pamoja na kuwa anakunywa hizo dawa, naona sasa zinamdhuru hasa ngozi yake inakuwa na spots, ambapo juzi tu wakampa madawa ya TB wakati hana hiyo TB, dawa zikamdhuru hadi mdomo unababuka ngozi. Bado anaendelea na kazi yake ya kilimo cha bustani na pia boda boda, physically hayupo vibaya sana.
Kutokana na elimu niliyoipata humu hasa ile thread ya V.V.U na Upimaji wake, nimegundua huyu bro hana ngoma, ila labda ni lishe bora tu na life style mbovu.
Kwa vile ameshakuwa mhanga wa ARV nifanyeje ili nimuachishe dawa hizo bila kumletea madhara, aweze kurudia hali yake ya kawaida. Naogopa nisije kumshawishi aache akaanza kuumwa nikalaumiwa mimi.
Naomba ushauri kama akiacha ARV atumie nini, ambacho kitamfanya awe Normal?

CC: Kaveli, Deception
Ningekushauri huyo kakayo aende clinic, naamini atapa maelezo na huduma bora kabisa kabla ya kufanya maamuzi ya kuacha dawa zake. Kuhusu kwa nini yeye anao na mke wake hana, hiyo watalamu wanaju nafikiri huita descodant couple.Kuwa mke anao na mume hana au mume anao na mke hana. Utafiti umeonyesha, ingawa hii tuliijua tangu miaka ya 2007, kuwa mtu mwenyekiwango cha chini kabisa virus ni vigumu kuambukiza, na ni zahiri kabisa kwa vile kakayo viral load yake iko chini, ni vigumu kumuambukiza mkewe, lakini haina maana kuwa yeye hana HIV, na kuwacha dawa. Kumbuka sio kuwa unapomuingilia mtu mwenye HIV, na wewe utapata HIV inategemea mambo mengi pamoja na viral load ya mwenye virus. Hii haina mana ujimwage tu, kuwa muangalifu na kufanya hilo tendo bila kinga, Kuhusu kutoka spot na inawezekana na kuwasha, baazi ya dawa za TB inasababisha hilo na hata baazi ya ARV, na mpaka baazi ya magonjwa huwanyemelea watu wenye HIV, husababisha
 
Mkuu,umegunduaje hana ngoma? Kisa mkewe ni -ve?

Share with us huo ugunduzi.
 
kisebengo nilishaambiwa kuna mdada alikuwa anatumia arv na baada ya muda cd4 zake zikafika 800 continuous for six month akashauriwa kuacha dawa. je kuna ukweli hapomaana nasikia bado anamonitor cd4 lakini amestabilizi. wataalam watujuze
 
Kwa ushauri wangu asiache kutumia dawa kbs atumie dawa na kwanini unakataa kaka ako hana HIV wakat kipimo kilionesha ameathilika
 
HIV infection is for life na ARVs is commitment for life.Sasa mambo mengine ni maamuzi ya MTU mwenyewe.

Ukiamua kuacha au kuendelea na dawa.Wataalam watakuelezea kila uamuzi unataka Ku chukua faida na hasira zake.

Ktk wanandoa kuwa na mmoja HIV Positive na mwingine Negative huwa inatokea ila Mara machache sana.(Discordant)

Kwa maendeleo ya tafiti zinazoendelea labda kutakuwa na mabadiliko mbele ya safari.
 
Wana JF!!

Samahani sana, naomba msaada wenu, najua mpo wengi wenye uelewa wa mambo.
Sasa naomba kuelimishwa, pia kwa faida ya wengine wenye matatizo kama yangu.
Nipo hapa kwa niaba ya kaka yangu ambaye alipima na kuonekana ana '' HIV" mwaka 2011 mara moja wakamuanzishia matibabu ya ARV. Hakuwa na shida nyingine, zaidi ya kuwa na constipation..hakuwa anakula vizuri baada ya kufilisika duka lake, akawa anafanya kazi ngumu bila kula vizuri zaidi ya chapati tena zilizokobolewa unga. Kutokana na kudhoofika afya nilimpeleka hospitali na alipopima HIV alionekana HIV+ , lakini cha ajabu mke wake ni HIV- ni muda mrefu sasa.
Sasa huyu kaka yangu pamoja na kuwa anakunywa hizo dawa, naona sasa zinamdhuru hasa ngozi yake inakuwa na spots, ambapo juzi tu wakampa madawa ya TB wakati hana hiyo TB, dawa zikamdhuru hadi mdomo unababuka ngozi. Bado anaendelea na kazi yake ya kilimo cha bustani na pia boda boda, physically hayupo vibaya sana.
Kutokana na elimu niliyoipata humu hasa ile thread ya V.V.U na Upimaji wake, nimegundua huyu bro hana ngoma, ila labda ni lishe bora tu na life style mbovu.
Kwa vile ameshakuwa mhanga wa ARV nifanyeje ili nimuachishe dawa hizo bila kumletea madhara, aweze kurudia hali yake ya kawaida. Naogopa nisije kumshawishi aache akaanza kuumwa nikalaumiwa mimi.
Naomba ushauri kama akiacha ARV atumie nini, ambacho kitamfanya awe Normal?

CC: Kaveli, Deception
Ningekushauri, ni kurudi clinic au hospitali ambako huwa anapata huduma, kabla ya kufanya maamuzi ya kuachana na dawa. Kuhusu kuwa mmoja anao na mwengine hana, hiyo inatokea sio kigeni nafikiri watalaamu wanaita discordant couple.
Kumbuka kuwa sio lazima unapoingiliana kimwili na mtu wenye HIV, na wewe kuwa . lazima upate HIV, inategemea mambo mengi, pamoja na viral load. Utafiti unaonyesha kuwa mtu mwenye viral load ya chini ni vigumu kuambukiza, hii ilikuwa inajulikana tangu miaka 2007. lakini haina maana kuwa watu wajimwage tu bila kuwa wangalifu na kutokutumia kinga. Kuhusu hizo spot, wakati mwengine kuwashwa badhi ya dawa za TB, HIV husababisha hivyo na hata baazi ya magonjwa yanayoambatana na HIV husababisha. Kumbuka la muhimu ni kurudi hospitali au clinic
 
Back
Top Bottom