Nifanyeje ili nipate ujasiri wa kupima HIV?

Mkuu Pdidy ukweli ni kwamba mademu wote niliokula kavu kavu hawana ngoma kwa sababu wao wana ujasiri wa kupima kila mara,kuna demu nimeachana na ye mwaka juzi ambaye ilikuwa nioe kabisa,kila mara alikuwa anapima na alikuwa hana mpaka tunaachana na tulikuwa wote kwa miaka miwili,mwingine tumeachana mwezi wa saba mwaka huu na alienda kupima hana,lakini kila nikiga hesabu kwenda kupima nakosa ujasiri kaka

Mmh! Na we jamaa ni kiwembe kweli, lazima ubadilike, Kila mtu tu unatembea nae, utafupisha maisha yako ndugu
 
Hatua ya kwanza ilikuwa hiyo ya kuwaza kupima, hongera kwa kuruka kihunzi namba moja.

Hatua ya pili ni kuchukua hatua ya kwenda kupima. Ukifika pale utapewa ushauri nasaha na kuambiwa faida lukuki za kupima. Ili uchukue hatua, unapashwa kufahamu kuwa hiv sio death sentence anymore. Kuna watu lukuki wamekaa na ugonjwa up to 20+ years kabla hawajaanza kuumwa na kutumia dawa. Ukijua hali yako kwamza kihoro kitakuisha. Hakuna kitu kibaya kama haya maisha unayoishi ya kukohoa tu unawaza kama ndio ngoma.

Nenda kwa ushauri, kupima sio lazima. Utakapojisikia utaendelea na hatua ya kupima. Kuna uhuru wa ajabu baada ya kupima.
 
Ushauri
Jipe moyo kuwa ukikutwa + kuna dawa za kupunguza makali ambazo unaweza ishi up to 30 years na huo ugonjwa
kuna mtu namjua alijigungua miaka ya 80 na bado anadunda na anatoa ushuhuda.

Pia unaweza tafuta ndugu au rafiki unayemuamini akusindikize hii itakupa moyo kiasi fulani.

mimi nilipima kwa sababu ilibidi nimtolee damu mama yangu ambaye alikuwa ktk hatari ya kupoteza maisha, ukweli ni kwamba sikuogopa majibu because nilikuwa namfikiria mama yangu.

jipe moyo ndigu yangu, mbona watu wanapima cancer kila siku na hawaogopi kupima, why not ukimwi.

"You can fool some people sometimes.
But you can't fool all the people all the
time."--Bob Marley
 
Mkuu Pdidy ukweli ni kwamba mademu wote niliokula kavu kavu hawana ngoma kwa sababu wao wana ujasiri wa kupima kila mara,kuna demu nimeachana na ye mwaka juzi ambaye ilikuwa nioe kabisa,kila mara alikuwa anapima na alikuwa hana mpaka tunaachana na tulikuwa wote kwa miaka miwili,mwingine tumeachana mwezi wa saba mwaka huu na alienda kupima hana,lakini kila nikiga hesabu kwenda kupima nakosa ujasiri kaka

Sidhani kama kuna ukweli wowote hapa..........yaani wote unaotembea nao wamepima hawana sasa iweje wewe uogope kwenda kupima???!!!! Mchukue mmoja kati ya hao uende nae atakupa nguvu na matumaini wakati unasubiria kujua status yako. Kama vipi niambie nikusindikize,mie siogopi hata!!
 
hakuna kitu kinanipa shida kama kwenda kupima afya yangu na kuijua afya yangu,nimejitahidi sana kujipa moyo lakini nashindwa kabisa kupata ujasiri wa kupima,nakumbuka mara ya mwisho pale mbeya nilikwenda kupima lakini wakati wa majibu nilipotea na sikupenda kurudi kwenye kituo tena,jamani kuna njia yoyote ya kuniwezesha nipime afya yangu?japo ni bure kupima lakini nimekosa ujasiri,hii ni mara ya pili naleta hii mada humu ndani kuhusu HIV,naomba washauri au wale ambao mliweza kupima mnisaidie ushauri kwani naweza kushawishiwa na ushauri wenu hapa jf kwa kuwa mimi ni msomaji mzuri wa mada za jf
naomba mliopima na kukutwa na virus mniambie yaliyowakuta siku ile baada ya kupewa result
na wale mliopima mkakutwa hamja athirika naomba mseme mlijisikiaje??

Pole sana. Ungewaachia namba ya simu wakutumie kwenye meseji
 
Ole wao wafanyiao umbea miili yao,maana majibu watakayopata yatawaharakisha kuiaga dunia hii na kukosa raha walizojaaliwa.Nzagamba 12:6

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Nunua home test kit ( I think inaitwa bio line test), fundishwa namna ya kujipima na kusoma majibu kwa usahihi. Then on sunday after church kula viroba vya kutosha upate confidence but do not over drink. Ole wako ukosea kujipima na majibu yaonyeshe una ngoma wakati huna, utajuta.!
 
Acha woga mtoto wa kiume! Nakushangaa unaogopa kupima HIV, je unaogopa nini kuchukua majibu? Inafaa nini kuwa na mwili bila kuwa na uhakika wake?
Nenda kesho kapime HIV, pima pia na homa ya ini (Hepatitis B). Usisikilize kauli za kizamani kama kupima hakuna faida, ni kujipunguzia muda wa kuishi n.k.
 
Mkuu Episodes!

Kama roho inasita usijaribu kupima!
kuna watu humu jamvin wanataka wakudanganye
 
Mkuu siku unaenda nistue tuende wote, manake hata mimi kila kukicha napoteza ujasiri wangu wa awali.
Siku nikipata huu ujasiri na nikakuta sina ngoma, lazima nitoe mshahara wa mwezi mzima kama sadaka...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom