Nifanyeje ili nipate ujasiri wa kupima HIV?

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Hakuna kitu kinanipa shida kama kwenda kupima afya yangu na kuijua afya yangu, nimejitahidi sana kujipa moyo lakini nashindwa kabisa kupata ujasiri wa kupima, nakumbuka mara ya mwisho pale Mbeya nilikwenda kupima lakini wakati wa majibu nilipotea na sikupenda kurudi kwenye kituo tena, jamani kuna njia yoyote ya kuniwezesha nipime afya yangu?

Japo ni bure kupima lakini nimekosa ujasiri, hii ni mara ya pili naleta hii mada humu ndani kuhusu HIV, naomba washauri au wale ambao mliweza kupima mnisaidie ushauri kwani naweza kushawishiwa na ushauri wenu hapa JF kwa kuwa mimi ni msomaji mzuri wa mada za JF.

Naomba mliopima na kukutwa na virus mniambie yaliyowakuta siku ile baada ya kupewa result na wale mliopima mkakutwa hamjaathirika naomba mseme mlijisikiaje??
 
Kunywa viroba vya kutosha kama kumi hivi then kapime akili itakwambia liwalo na liwe hutokuwa na hofu tena
 
Nenda kapate ushauri nasaha, kama bado hujiamini usipime hadi utakapo pata ujasiri huo.
 
Kwani ulipitia chaka bovu? Au kitu gani kilichokupa wasiwasi mpaka ukataka kupima? Demu wako hajatulia aka mwingi wa habari aka mama huruma? Au wewe ni bandika bandua chapa ilale? Unaudhuria sana ambiance,jolly,leaders club road,kinondoni graveyard etc?
 
episodes kama huna ujasiri wa kupima usipime kabisa, maana ukijilazimisha kwenda na matokeo yakawa tofauti unaweza ukafa kwa kihoro.
 
Last edited by a moderator:
hakuna muda mbaya, kama muda wa kusubiria majibu ya HIV! Lord Have Mercy! Kama huna ujasiri ndugu, usiendeeeeeeee!
 
Kama huna sababu kama hizi nakushauri usijisumbue kwenda kupima Ukimwi utaitesa nafsi yako bure:-
1. Kutaka kuoa
2. Kutaka kuzaa mtoto
3. Kuugua homa za mara kwa mara au magonjwa yenye dalili za mtu aliyeathirika.
4. Kuugua kifua kikuu
5. Mpenzi au yeyote uliyefanya naye mapenzi au Mke wako kugundulika kafa kwa Ukimwi
 
Hamna kitu kizuri kama kupima, ukigundua kama upo +- nadhani utapata muda mzuri wa kujipanga kimaisha, wasikutishe kama una hofu kwenda kupimwa nipime mwenyewe nunua kile kifaa cha kupima mwenyewe nyumbani, nadhani si zaidi ya elfu hamsini. lakini kumbuka kuwa kuwa na virusi si mwisho wa maisha usiogope - kata shauri uende, mbona wana jf wote wamepima? teh teh
 
Kupima ni jambo moja ila kuchukua majibu ni suala gumu sana kwa wengi wetu hasa ambao walicheza michezo ambayo si salama.
Kama mtu haujawa tayari kupima ni bora ukaacha mpaka utayari uwepo maana bila hivyo utasababisha kifo cha muda mfupi tena bila kutegemewa.
 
Ushauri
Jipe moyo kuwa ukikutwa + kuna dawa za kupunguza makali ambazo unaweza ishi up to 30 years na huo ugonjwa
kuna mtu namjua alijigungua miaka ya 80 na bado anadunda na anatoa ushuhuda.

Pia unaweza tafuta ndugu au rafiki unayemuamini akusindikize hii itakupa moyo kiasi fulani.

mimi nilipima kwa sababu ilibidi nimtolee damu mama yangu ambaye alikuwa ktk hatari ya kupoteza maisha, ukweli ni kwamba sikuogopa majibu because nilikuwa namfikiria mama yangu.

jipe moyo ndigu yangu, mbona watu wanapima cancer kila siku na hawaogopi kupima, why not ukimwi.
 
Mimi pia nakushauri kama huna sababu ya msingi inayokufanya ukapime,usiende kupima kawasababu inaweza kufupisha hata umri wako wa kuishi hapa duniani kutokana na kihoro,ila kama sababu ipo nenda kapime itakusaidia uishi zaidi kwani hizo dawa za kurefusha maisha kwa watu wengine zinawarudishia CD4 zao mpaka wanapunguziwa dawa za kunywa kutokana na kuwa na kinga kubwa sana katika miili yao ambayo inasababisha virusi wapotee kabisa kwenye damu yao.
 
hakuna kitu kinanipa shida
kama kwenda kupima afya yangu na kuijua afya yangu,nimejitahidi sana
kujipa moyo lakini nashindwa kabisa kupata ujasiri wa kupima,nakumbuka
mara ya mwisho pale mbeya nilikwenda kupima lakini wakati wa majibu
nilipotea na sikupenda kurudi kwenye kituo tena,jamani kuna njia yoyote
ya kuniwezesha nipime afya yangu?japo ni bure kupima lakini nimekosa
ujasiri,hii ni mara ya pili naleta hii mada humu ndani kuhusu HIV,naomba
washauri au wale ambao mliweza kupima mnisaidie ushauri kwani naweza
kushawishiwa na ushauri wenu hapa jf kwa kuwa mimi ni msomaji mzuri wa
mada za jf
naomba mliopima na kukutwa na virus mniambie yaliyowakuta siku ile baada
ya kupewa result
na wale mliopima mkakutwa hamja athirika naomba mseme
mlijisikiaje??

Piga msuba wa kufa mtu!
 
Oops @epsodes mpaka leo hujapima tu ,,
Cha msingi kama unaogopa sana nenda kwa watu wa ushauri nasaha
Nenda siku ya kwanza ya pili ya tatu hata mwezi
mwisho wa siku utajikuta umekata shauri la kupima...
 
Kama huna sababu kama hizi nakushauri usijisumbue kwenda kupima Ukimwi utaitesa nafsi yako bure:-
1. Kutaka kuoa
2. Kutaka kuzaa mtoto
3. Kuugua homa za mara kwa mara au magonjwa yenye dalili za mtu aliyeathirika.
4. Kuugua kifua kikuu
5. Mpenzi au yeyote uliyefanya naye mapenzi au Mke wako kugundulika kafa kwa Ukimwi

Mwache akapime tu.Kuna faida zake za msingi. Mfano kama atakuwa hajaathirika ita -motivate kujilinda zaidi na kuwa mwanagalifu.Na kama atakuwa ameathirika itamsaidia achukue hatua mapema na kuanza tiba kabla hajaanza kukohoakohoa na vijihoma..
Namshauri ajikaze kiume na aende
 
hakuna kitu kinanipa shida kama kwenda kupima afya yangu na kuijua afya yangu,nimejitahidi sana kujipa moyo lakini nashindwa kabisa kupata ujasiri wa kupima,nakumbuka mara ya mwisho pale mbeya nilikwenda kupima lakini wakati wa majibu nilipotea na sikupenda kurudi kwenye kituo tena,jamani kuna njia yoyote ya kuniwezesha nipime afya yangu?japo ni bure kupima lakini nimekosa ujasiri,hii ni mara ya pili naleta hii mada humu ndani kuhusu HIV,naomba washauri au wale ambao mliweza kupima mnisaidie ushauri kwani naweza kushawishiwa na ushauri wenu hapa jf kwa kuwa mimi ni msomaji mzuri wa mada za jf
naomba mliopima na kukutwa na virus mniambie yaliyowakuta siku ile baada ya kupewa result
na wale mliopima mkakutwa hamja athirika naomba mseme mlijisikiaje??

kumbe waoga tuko wengi...mie aisee sijui hata kama naweza kuthubutu , nahisi nitapata presha. maana nikisikia tu ule ushauri nasaha hata kwenye TV nahamisha station
 
Kama huna sababu kama hizi nakushauri usijisumbue kwenda kupima Ukimwi utaitesa nafsi yako bure:-
1. Kutaka kuoa
2. Kutaka kuzaa mtoto
3. Kuugua homa za mara kwa mara au magonjwa yenye dalili za mtu aliyeathirika.
4. Kuugua kifua kikuu
5. Mpenzi au yeyote uliyefanya naye mapenzi au Mke wako kugundulika kafa kwa Ukimwi

mkuu sijaugua wala sijawahi kuugua magonjwa hayo,ila kila siku najiuliza nikija kuugua itakuwaje??nimepitia mambo mabovu sana ndio maana naogopa
 
Tembea na mwenye hiv utapata nguvu ya kupima waala usiumizekichwa mpwa
 
mkuu sijaugua wala sijawahi kuugua magonjwa hayo,ila kila siku najiuliza nikija kuugua itakuwaje??nimepitia mambo mabovu sana ndio maana naogopa
mkuu usiumize kichwa kama umepitia mambo mabovu wapo waliopita milima mibovu na mungu akawaokoa na wewe waweza kuwa mmoja wao usiogope ...kama una binti mpe mimba wala aijifichi utaona uko fit ama lah mtoto akitoka kila la kheri
 
mkuu usiumize kichwa kama umepitia mambo mabovu wapo waliopita milima mibovu na mungu akawaokoa na wewe waweza kuwa mmoja wao usiogope ...kama una binti mpe mimba wala aijifichi utaona uko fit ama lah mtoto akitoka kila la kheri

Mkuu Pdidy ukweli ni kwamba mademu wote niliokula kavu kavu hawana ngoma kwa sababu wao wana ujasiri wa kupima kila mara,kuna demu nimeachana na ye mwaka juzi ambaye ilikuwa nioe kabisa,kila mara alikuwa anapima na alikuwa hana mpaka tunaachana na tulikuwa wote kwa miaka miwili,mwingine tumeachana mwezi wa saba mwaka huu na alienda kupima hana,lakini kila nikiga hesabu kwenda kupima nakosa ujasiri kaka
 
Back
Top Bottom