Nifanye nini iliniweze kurudisha mkopo na riba

7m mkopo...ni hela kiduchu huwezi kufanya la maana hasa kama ndio unaanza moja...na kwa sababu hauna plan yeyote...warudishie tu hela yao kabla ya interest haijafanya mambo yake...

Ulitaka apewe mkopo wa sh. ngapi kama security ni chattel mortgage na gari yenyewe ni Toyota Vitz?

Hata hivyo Mil 7 si ndogo kama unavyozani, binafsi nilianza na mtaji wa Tzs. laki 9 mil miaka ya tisini, sasa hivi my net worth ......

So tusimkatishe tamaa jamaa, 7 mil ni nyingi sana if he has relevant financial knowledge and experience katika field anayotaka ku invest.

Though kama mpaka sasa hivi hana idea yoyote ya nini afanya, ni bora arudishe pesa au aombe grace period ya miezi kadhaa ili ajipange in terms of the waht to do, developing a business plan, and start up days for the business ambapo sales inakuwa ndogo sana huku iki pick up slowly!!

Otherwise, I wish you all the best!!
 
7m mkopo...ni hela kiduchu huwezi kufanya la maana hasa kama ndio unaanza moja...na kwa sababu hauna plan yeyote...warudishie tu hela yao kabla ya interest haijafanya mambo yake...
KUSEMA KWAMBA 7M NI NDOGO AU NYINGI IT DEPENDS ON THE TYPE OF BUSINESS HE WANTS TO START........ kuanzisha biashara ya kuuza magari hiyo fedha ni kiduchu sana lakini kwa biasha ya steshenare, tena ya kuiendeleza hiyo inatosha........... REMEMBER, A REFERENCE POINT IS VERY IMPORTANT WHEN DOING COMPARISON..........
 
Friends, Ni kweli Masikini jeuri amesha kosea, ingawa naamini alikuwa na plan fulani kabla ajakopa. Sasa tayari ameharibu, So mwenzetu anaanzia wapi?

Nikifikiri Biashara anayoweza kufanya with return ya more than 500.000/= a month!!!!!
Bado sijaijua.

Wandugu tuchemsha Mbogo.
 
Kwanza pole, ni kweli watu tunahitaji elimu ya ujasiriamali, mie ushauri wangu ni biashara za vitu vya kula, mtu anaweza acha kuvaa, kusoma au mengine lakini lazima wale. Kama umemsoma Pearl biashara za kuku wawe wa kienyeji kwa kuwabeba na kuwaleta mjini kuuza au kufuga kama uko kwako unaweza zalisha hiyo hela kwa mwezi au zaidi. Ila hizi ni simple ambazo wala haitaji mtaji mkubwa hivyo. Kama unataka tu kuongezea biashara wakati unasubiri hiyo stationary itakufaa kupunguza hilo deni.
 
Kama ulichua hizo hela na bado unazo wakati huu unapoomba ushauri na kama ni za kuanzia biashara au shughuli mpya na sio kuiendeleza nakushauri zirudishe haraka kwa mwenyewe. Hesabu za haraka haraka nilizo fanya zinaonyesha mpaka mwisho wa mwaka utakuwa umelipa jumla ya TZS 15,190,000.00 zikiwa mkopo wa TZS 7,000,000.00 pamoja na riba jumla ya TZS 8,190,000.00
 
mi naona kama ni tshs 8,260,000.00 ( mkopo 7m na interest ni 1,260,000) wajuzi wa hesabu msaada kwa tuta
 
Usishangae haya ni matatizo ya kawaida sana katika biashara za bongo,mikopo yetu ina liba kubwa sana na wengi wanashindwa kulipa, ushauri wangu ili uweze kulipa mkopo wako ni vyema ukafanya mambo kadhaa, la kwanza fanya heasabu zako za mauzo ujue kwa kila siku ukiuza unapata faida kiasi gani na unaweza ku ludisha mtaji kiasi gani, then tengeneza heasabu ujue ukigawa mapato hayo kwa siku nzako za kazi unahitaji siku ngapi kuwa umepata kiwango cha rejesho kwa mwezi, baada ya hapo weka utaratibu wa kutunza hakiba hiyo kwa idadi ya siku ulizopata.
 
kama ulichua hizo hela na bado unazo wakati huu unapoomba ushauri na kama ni za kuanzia biashara au shughuli mpya na sio kuiendeleza nakushauri zirudishe haraka kwa mwenyewe. Hesabu za haraka haraka nilizo fanya zinaonyesha mpaka mwisho wa mwaka utakuwa umelipa jumla ya tzs 15,190,000.00 zikiwa mkopo wa tzs 7,000,000.00 pamoja na riba jumla ya tzs 8,190,000.00


let me check:d
 
mkuu jeuri:
Mi nakosa kuona shida lako. Ikiwa haujauchukua huo mkopo, si usimamishe aliyekukopesha mpaka mipango ya biashara iwe settled?
 
Nilikuwa nimepata nafasi ya stationery eneo la chuo ambalo mpaka sasa naendelea kufuatilia na hapo kabla nilikuwa na endesha stationery kwenye jengo amabalo mwenye amelibomoa. Na maombi ya mkopo niliyafanya wakati niko bado kwenye biashara na umekuja kukubaliwa hivi punde

Mkuu kama kwa sasa huoni namna ya kuutumia mkopo huo na kupata faida, ni bora uzirudishe kabla hujazigusa ili kuepuka riba kubwa sana.
 
Kwa ujumla kukopa hela kabla hujajua cha kuzifanyi ni kosa la kwanza. Ili kupunguza mzigo wa riba rudisha hela kwa aliyekukopesha upesi. Then rudi ukae chini jitathimini una uwezo/ujuzi gani? Uwezo huo unafaa katika biashara zipi? Utaweza kuwa na ubunifu upi kuwazidi wale wanaoifanya biashara hiyo sasa? Nk. Maana biashara ni ushindani? Usipokuwa na uwezo wa kushindana kuwazidi wanaoifanya biashara hiyo sasa huwezi kutarajia mafanikio makubwa. Ukishajitathimini na kutambua uwezo/ujuzi wako katika kushindana kwenye biashara husika, andaa mpango wako wa biashara kwa kuzingatia matokeo ya tathimini yako. Halafu kakope. Mafanikio yatakufuata kwa kasi. Biashara iliyoniletea mafanikio mimi si lazima wewe pia uiweze, kwani watu tunatofautiana uwezo na umakini wa kuendesha na kusimamia. Mungu akubariki
 
Naunga mkono suala la kusitisha mkopo huo; kwa sababu haitatosha kufanyia utafiti wazo jipya katika wiki moja iliyobaki.

Asanteni sana kwa ushauri na tuendelee kujadili changamoto zaidi.
 
erry84 hunitakii mema ndugu yangu!

Kwanza maadili hayaniruhusu kucheza kamari na sijawahi kucheza kamari maishani mwangu! Asante nishausitisha mkopo nashukuru wote walikokuwa mstari wa mbele kunisaidia!
 
Wazo la kurudisha mkopo nfio mjalabu na hata bank wayaelewa kuwavulikopa kwasababu ya biashara iliyopo lakini sasa haipo kwa sababu ulizozitaja za kubomolewa kwa jengo ulilokuwa unafanyia biashara.
 
Back
Top Bottom