Nidhamu ya woga

Zing

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
1,767
470
Kuna hili tatizo ambalo tukiliangalia na kulitatua ndani ya jamii yetu mabadiliko ya ya maendeleo ya kweli yanawezekana. Tatizo hili ni NIDHAMU YA WOGA


  • wengi tumeezaliwa na kulelewa kwenye mazigira ambayo mtoto kwa mzazi hatakiwi kubisha, ni hatukupewa nafasi ya kuchangia

  • Shuleni kuanzia, chekechea primary secondary na hata vyuoni uhusiano kati ya mwalimu/mkufunzi na mwanfunzi ni kama paka na panya.kama mwanafuzi tulijengewa uoga na kuwaogopa walimu

  • matatizo haya yanakuja mapka mtu anapopata kazi ofisini. Nidhamu ya woga imeota mizizi mtu unaogopa kumkosoa bosi ingawa unajua kabisa wazo au ushauri wako ni mzuri. Hivyo hivyo mabosi wengine anajiona kukosolewa au wazo lake kupingw ana mtu wa chini yake ni kujidharirisha.

  • Hata kwenye ndoa kuna mke na mume wanaogopana ogopana kiasi kila mtu anaweza kutoka kuvinjari nje sababu anahisi kuna mambo akimwambia mkewe au mumewe basi atamuona muhuni. matokea yake ndo nyumba ndogo kwa wanaume na vidumu kwa wanawake
Kuuukata huu mnyororo inabidi inabidi watoto wanaozaliwa kipindi hiki wafundishwe kujiamini na kuelezea hisia zao wazi mapema zaidi.mabadiliko yatakuja kwa wazazi kubadilika, walimu kubadilika na viongozi kubadilika juu ya mtazamo walionao kwa watu wa chini.


Tujifunze Kukubali kutokubaliana na tujue kila mmoja wetu ana mchango muhimu

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom