Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,627
- 154,995
ILIPOSIKIKA sauti yake kila mpenzi wa muziki anayefuatilia bendi za hapa nyumbani alihisi kuna kitu kipya kimeingia katika tasnia ya
muziki wa dansi. Hiyo ilikuwa mwaka 1982 alipoingia kwa mara ya kwanza nchini mwimbaji hatari kutoka mkoa wa Pwani nchini Kenya Nico Zengekala akiwa ni mwimbaji tumaini wa bendi ya Les Quban.
Bendi hiyo ilianzishwa nchini Kenya lakini ilikuwa na wanamuziki kutoka Tanzania ambapo awali ilikuwa pamoja na mwimbaji maarufu Juma Kilaza aliyetamba sana mkoani Morogoro kabla ya kufanyika mapinduzi ya uongozi yaliyomnyang'anya Kilaza uongozi na pia kumtimua kwenye bendi na jahazi hilo kushikwa na mpuliza saxophone marehemu Comson Mkomwa.
Walipoingia katika kumbi za burudani za jijini Dar bendi hiyo ikiwa pia na mpiga gitaa la solo Mohamed Tungwa, wapuliza ala za
upepo kama Said Makelele, Jumanne Mwamzungu, akina Majuto Mbungani na Shaibu Monduli bendi hiyo iliweza kuingiza
ushindani kwa bendi kongwe kama Juwata wakati huo, Mlimani Park na hata bendi zilizokuwa na asili ya wanamuziki kutoka nchini Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) kama vile Orchestra Safari Sound, Marquiz du Zaire na Matimila.
Nyimbo zilizozipeleka puta bendi nyingine pamoja na mashabiki kwa ujumla ni pamoja na Shemango, Kambarage Nyerere, Jack na
nyingine kadhaa. Uimbaji wa Zengekala ulianza kupata sifa ndani na nje ya bendi hiyo na watabiri wa masuala ya muziki wakati huo walithubutu hata kueleza wazi kwamba mwanamuziki huyo kamwe asingedumu katika bendi hiyo.
Hatimaye, mawazo hayo yakawa kweli kwani Zengekala mwenyewe alimueleza mwimbaji mwenzake wa karibu wakati huo, Shaibu Monduli kwamba yeye alitamani sana kuiimbia bendi ya Juwata Jazz inayotumia mtindo wa Msondo Ngoma. Akamsisitizia kwamba dhamira hiyo alikuwa nayo tangu alipokuwa nchini kwao Kenya ambako alizisikia nyimbo za bendi hiyo na pia akatamani siku moja kuimba na akina Hassan Bitchuka, Shaaban Dede, Joseph Lusungu na waimbaji wengine wakongwe.
Hivyo alitaka hatua yake ya kufika nchini Tanzania iende na dhamira yake ya kujiunga na bendi hiyo endapo atakubaliwa. Vurumai kubwa ilijitokeza miongoni mwa viongozi wa bendi ya Les Quban waliokuwa wakitumia mtindo wa Vinavina na wale wa Juwata baada ya kujua nyota ile ya jaha inaangazia kwenye bendi yao.
Hatimaye Zengekala akatua Msondo na kuweka mapenzi makubwa ya urafiki na mwimbaji mwingine chipukizi aliyemkuta
Msondo marehemu Tino Masinge. Alipojiunga tayari bendi hiyo ilishawakamata waimbaji mbalimbali akiwemo TX Moshi William kutoka bendi ya Polisi Jazz.
Wimbo wake wa kwanza na bendi ya Juwata ulikuwa ni Solemba ambao alipenda apigiwe solo na gwiji la chombo hicho Dk
Saidi Mabela na yeye akashirikiana kuimba akiwa na Suleyman Mbwembwe na Tx Moshi William. Enzi hizo tayari Hassan Bitchuka alishaihama Msondo na kujiunga na Mlimani Park lakini ikatokea siku moja bendi hiyo kufanya shoo katika ukumbi mmoja pale DDC Magomeni Kondoa.
Kwa kuwa siku hiyo Bitchuka naye alikuwemo ukumbini na Msondo ndiyo iliyopata nafasi ya kufungua pazia la burudani ile basi umati wa watu uliojaa ulidhani Bicthuka ameamua kwenda kuipiga tafu Sikinde kumbe ilikuwa ni sauti ya Nico Zengekala aliyekuwa akiimba wimbo uitwao Sogea karibu.