Nicholas E. Mgaya amjibu JK

Umeridhishwa na majibu ya Mgaya dhidi ya JK?


  • Total voters
    65
Watu wengi wameongea kuwa wa bongo ni ma kondoo....Naamini kuwa hakuna nchi rahisi kutawala kama BONGO. Mkulu kapiga kelele na kupinga haki ya wanyonge ambao ndio wengi hapa nchini na hapo majuzi tu watu wachache walioiba vijisenti vya jasho la hawa wanyonge,hakusimama na kukemea.........Ajabu zaidi ni vile wazee wetu walikaa wanamshangilia.......what a shame
 
Ndugu Wafanyakazi, kauli ya Mheshimiwa Rais katika Hotuba yake kuwa ‘ Serikali haiwezi kuwalipa wafanyakazi wake kima cha chini cha shs.315,000/= hata wakigoma miaka nane (8) ni ya kushtua na ya kukatisha tamaa kwa vile inaonyesha jinsi gani Serikali hii isivyo na mipango na mikakati madhubuti ya jinsi ya kuongeza pato la Taifa na hatimaye kuongeza Mishahara ya Watumishi wake ambao ni muhimu katika ukuzaji uchumi.

Kwa maana yake, hiyo nyekundu inahoji uwezo wa JK kuomba kuendelea kuiongoza Tanzania. Pia ukiowanisha na majibu yake kuwa hajui kwanini Tanzania ni maskini, jibu kamili linapatikana. Nalo ni kuwa hajui kwanini aliomba/anataka kuendelea kuiongoza Tanzania.
 
......yes majibu sahihi hayo! hata na hivyo nadhani majibu yaliyosahihi zaidi inatakiwa yatolewe come October 31!......Huyu JK hajui anachokityenda, hajui dhana nzima ya uongozi, hotuba yake ilijaaa, ubabe, ujeuri, ufisadi, ufinyu wa mawazo, kukosa michanganuo sahihi and every kosa u could have noted there......! shame on him!
 
vita ya mgaya na kikwete vitaendelea kwa muda mrefu kwani jazba za mwenye nchi zilikuwa juu sana
 
Nimependa Nicolas Mgaya alivyojibu kisayansi kwani hakutumia jazba na hakukurupuka kama JK alivyofanya na bila shaka wenye uelewa wanaweza kuchambua mchele na pumba. Masikini Kikwete sijui atawaambia watu nini kampeni zitakapoanza ! Ningekuwa yeye huu ndio wakati mwafaka wa kuwatangazia wananchi kuwa hali yako ya kiafya inakulazimisha uachie uongozi, tatizo sijui washikaji wake kama wataridhia. Hilo ndilo tatizo la kuwa na ubia katika uongozi kwani maamuzi yako binafsi hayana maana tena mpaka the Azizis, Patels, Sinclairs, Manjis n.k. uwahusishe. He couldnt fight them and so joined them and became one of them or maybe he was one of them all along - kaazi kweli kweli !
 
Ukitaka kumsaidia mtu aliye "uchi" bora umwambie wazi kuwa yupo "uchi" na siyo kumwambia kuwa amependeza huku akiendelea kuadhirika.

TUCTA wamefanya vizuri kumjibu na sasa ni juu ya wananchi kuamua nani mkweli na nani mzandiki.
 
...Yaani haya majibu ni murua...Sasa tunamtaka Rais wetu apime mwenyewe halafu achukue hatua. Ni kama wakati ule Ripoti ya Bunge kuhusu Richmond ilipomtaka Lowassa kupima na kuchukua hatua. Hakika wasaidizi wa Rais ni mamumbumbu na zumbukuku. Jamaa amezijibu hoja zote na kuzifinyanga finyanga.

Tatizo mkulu hana taimu na mambo yanayotokea nchini mwake hivyo hapati wasaa kufanya upembuzi yakinifu. Alipolipata hili, akakurupuka. Ama kwa hakika ni aibu hii.

Waziri mkuu Pinda alipokurupuka na kusema wanaowaua albino nao wauwawe, alikuja kuomba radhi na chozi akalimwaga kwakuwa alivunja sheria. Sasa na hapa mkulu anawatisha wafanyakazi kuwa mgomo ni batili na atakayegoma atapigwa virungu na dola naye anavunja sheria makusudi huku akijua kuwa mgomo ule uliotolewa notisi na ni wa halali. Yapaswa naye atoe chozi hapa.
 
Waziri mkuu Pinda alipokurupuka na kusema wanaowaua albino nao wauwawe, alikuja kuomba radhi na chozi akalimwaga kwakuwa alivunja sheria. Sasa na hapa mkulu anawatisha wafanyakazi kuwa mgomo ni batili na atakayegoma atapigwa virungu na dola naye anavunja sheria makusudi huku akijua kuwa mgomo ule uliotolewa notisi na ni wa halali. Yapaswa naye atoe chozi hapa.

Siku zote Pinda hana kiburi na ni msikivu, tatizo la JK ni kiburi, kutopenda kuwasikiliza watu wenye mawazo tofauti na yake, kupenda sifa za bwerere, mlaini sana jamaa.
 
Duh Bonge la picha ni zuri kweli na nadhani adui (wafanyakazi) wanamshinda stelingi (jakaya) ha ha ha

Lakini wasiwasi wangu mimi ni kuwa hili nalo litasemwaaa weeeeee litapita na watu watasahau kwani mukulu akikaa kimya watanzania watahoji? Ubavu huo ndo bado tumeukosa ilitakiwa kumwambiwa wazi wazi kuwa yeye ndo mzandiki
 
Mkuu alidhani Urais ni ni jinsi ya kuvaa suti na kupakia ndege kila mara. Mimi na mpa pole, Ukitazama Marais wote wa Tanzania, Utagundua kwamba mkulu ndio kashemsha na kujiaibisha kama sio kuaibishwa na watanzania kuliko marais wengine waliopita.

Nadhani hata wale wakina zeutamu hawakuwa wamekosea kipindi kile. Kuwa na viongozi wa jinsi hii ni hasara kubwa kwa watanzania walio wengi.
 
Duh Bonge la picha ni zuri kweli na nadhani adui (wafanyakazi) wanamshinda stelingi (jakaya) ha ha ha

Lakini wasiwasi wangu mimi ni kuwa hili nalo litasemwaaa weeeeee litapita na watu watasahau kwani mukulu akikaa kimya watanzania watahoji? Ubavu huo ndo bado tumeukosa ilitakiwa kumwambiwa wazi wazi kuwa yeye ndo mzandiki

Hili lita leta athari katika utendaji wa kazi na si kama litasemwa tu..Believe me..Hapata mkuu kavaa chupi ya VIP, Itachungulia shingoni muda si mrefu..!
 
Kazi nzuri TUCTA na Mr. Mgaya anastahili pongezi za hali ya juu. Chukua zangu tano, nakuunga mkono 100%

Swali ambalo nimekuwa najiuliza kila siku, kama ufumbuzi wa matatizo ya wananchi kutoka kwa RAIS ndio hayo, (kiburi, vitisho, dharau, kejeli, ulimbukeni, n.k, n.k), tutegemee nini kutoka kwa mawaziri na watendaji wake wa ngazi za chini yake?

By the way: When is the next "Education Gala" in Paris or London?
 
SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limesema Rais Jakaya Kikwete hana ubavu wala mamlaka ya kubatilisha au kuhalalisha mgomo ulioitishwa na shirikisho hilo.

Akitoa tamko la shirikisho hilo kwa waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, Kaimu Naibu Katibu Mkuu Nicholaus Mgaya, alisema chombo pekee chenye mamlaka ya kusitisha mgomo huo ni Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi tu.

“Leo (jana) tumeona ni vizuri tukajibu baadhi ya hoja za Rais Kikwete alizozitoa kwenye mkutano wake na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, tunapenda kumwambia hana mamlaka ya kusitisha mgomo huu isipokuwa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi tu,” alisema Mgaya.

Alisema TUCTA imesikitishwa na kauli ya Rais Kikwete kutangaza kusitisha mgomo huo kwa vile kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria ya ajira na mahusiano namba 6 ya mwaka 2004.

Alisema shirikisho hilo limeshangazwa na kauli ya Rais Kikwete kuwa mgomo huo uliitishwa katikati ya majadiliano kwani haina ukweli wowote.

“Sasa tunashangaa kuona Rais Kikwete anasema mgomo huu umeitishwa katikati ya mazungumzo, jambo hili halina ukweli wowote hata kidogo, kwani tulitangaza kabla ya kurudi kwenye meza ya mazungumzo,” alisema Mgaya.

Alikanusha kuwa mgomo huo ulikuwa ni ajenda ya viongozi wa shirikisho hilo, bali makubaliano yalifikiwa katika kikao cha mkutano mkuu ambacho kilitoa maagizo ya kusitisha mgomo.

“Agizo la kuitisha mgomo shinikizi lake lilitolewa na Baraza Kuu kwa wafanyakazi nchi nzima, haukuwa uamuzi wa viongozi bali ni utekelezaji wa maagizo ya mkutano mkuu, sasa tunashangaa kuambiwa sisi waongo na wanafiki!” alisema Mgaya.

Alisema jambo pekee ambalo Rais Kikwete alitakiwa kulifanya ni kutoa majibu ambayo yangeweza kutatua matatizo sugu ya wafanyakazi ambayo hayakuanza sasa kuliko kutoa vitisho.

Akifafanua kauli ya Rais Kikwete ya kuwafukuza kazi wafanyakazi watakaoshiriki mgomo na kuhimiza waajiri wafanye hivyo, ni kinyume cha kifungu cha 83 (1), (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na 6 ya mwaka 2004.

Alisema akiwa kiongozi na mjumbe wa Baraza la Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO) hakuwahi kuhudhuria kikao chochote cha baraza hilo kikiwemo wa Aprili 14 mwaka huu wala kutia saini katika viwango vipya vya mishahara kama ilivyoelezwa na Rais katika hotuba yake.

Alisema kitendo cha Rais kudai hata wafanyakazi wakigoma miaka nane hawatalipwa ni ya kushtua na ya kukatisha tamaa kwa vile inaonyesha jinsi serikali isivyo na mipango wala mikakati madhubuti ya kuongeza pato la taifa.

Alisema kauli ya Kikwete, imekuwa ikikinzana na matamshi yake kutokana na ukweli kuwa anaposafiri nje ya nchi huwahimiza Watanzania walioko huko warudi nchini kujenga taifa lao wakati anasisitiza serikali haina uwezo wa kulipa mishahara!

Wiki iliyopita, Rais Kikwete aliwaita ‘wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Daimond Jubilee na kuwatuhumu viongozi wa TUCTA kuwa ni waongo, wanafiki na wazandaki kwa kuwapotosha wafanyakazi nchini ili wagome.
 
Kanisikitisha sana rais wangu kuimba taarabu mbele ya wazee wetu wale. Mtu makini alipaswa kuongea na waandishi wa habari na sio wazee wale. Hivi anategemea wazee wale wamuunge mkono wakati vijana wao wafanyakazi ndio anaowakandamiza? Sina majibu!!
 
JK ni wa kumsamehe tu, maana anaandikiwa tu amneno kwenye karatasi, then anaenda kusoma NA KUROPOKA bila hata kuhoji legitimacy yake...Kwa mara nyingine tena anadondoshwa na wasaidizi wake!..AIBU!...Yaleyale ya kufungua hoteliArusha, then kesho yake inabomolewa...Naona aibu hata kuitazama picha yake!
 
Toba! sasa Rais anajisikiaje? kama Rais anaweza kutumia vielelezo feki ili kumponda Mgaya, Je wasaidizi wake si ndo wanatumia vielelezo feki squere? ningekuwa mimi ni Rais kwanza ningewafukuza kazi watendaji wapovu waliosababisha yote haya Pili ningemwomba msamaha Mh. Mgaya!
 
Back
Top Bottom