Nicholas E. Mgaya amjibu JK

Umeridhishwa na majibu ya Mgaya dhidi ya JK?


  • Total voters
    65

Rayase

Member
Jun 12, 2009
82
3
Ndugu wana JF nimepata taarifa kupitia blog ya Michuzi kuwa Nicholas Ernest Mgaya ajibu tuhuma za JK Kwa msaada wa mdau Lyangalo wa hapa JF naambatanisha:
tucta.JPG


tucta+%281%29.JPG
tucta+%282%29.JPG


Kwa zaidi chukua hapa (kwa msaada wa Leon - JF Member)
 
Hata akijibu mapigo hakuna msaada kwani mwenye kaya alisema serikali haitapandisha mshahara kufikia 315,000 kutoka sasa hadi 2018 kwa maana kuwa hata rais wa 2015 ataendeleza libeneke,Hii ndiyo bongo
 
Hata akijibu mapigo hakuna msaada kwani mwenye kaya alisema serikali haitapandisha mshahara kufikia 315,000 kutoka sasa hadi 2018 kwa maana kuwa hata rais wa 2015 ataendeleza libeneke,Hii ndiyo bongo

kujibu mapigo ni kumueleza Kikwete kuwa maneno yake aliyoyaongea Juzi yalijaa upupu, utumbo na udwanzi mwingi, yaani ni kumpa somo kuwa aache kukurupuka.
 
Ndugu wana JF nimepata taarifa kupitia blog ya Michuzi kuwa Nicholas Ernest Mgaya ajibu tuhuma za JK

mwenye habari kamili atujulishe tafadhari

Anakuja kumuomba radhi RAISI
 
NI muhimu Kujibu mapigo ili kulinda heshima ya Wananchi...Jamaa aliyachukulia haya mambo too personal..that is why alikuwa anamention jina la mgaya kila wakati...! Nadhani hajajua kuwa wananchi wanao uwezo wa kumwondolea madaraka hata kama atatumia vyombo vya dola? Mkumbusheni kuwa..hata hao askari anaojitapa kuwatumia kuua wafanyakazi wakati wa mgomo..ni wafanyakazi pia..na wanalipwa 104,000....!
 
MgaYa angetulia tu!..Maana zile nyaraka alizotoa Rais wa TUCTA mbona zilitosha kuthibitisha Uzushi na Ubabe
na Udhushi wa Mwenye Kaya?...
Kujibu tuhuma ni sawa na kuendelea kumdhalilisha Mwenyekaya na wambea wake waliomdanganya......:angry:
 
Mwenye data ya alicho ongea Mgaya atumwagie wakuu,

Kwa ufupi Mgaya CV kaisha pandisha, na yuko juu, na Mkulu hakujua kwamba kwa kumponda kwakutumia data feki kwa mrindimo wa mipasho ndo kaisha mpaisha jamaa, vijana wa leo wanasema hiyo ilikula kwa JK Yaani sasa hivi Mgaya yuko juu ile mbaya!
 
Mbegu imeshapandwa! Tutake tusitake mmea utaota tu! Na watakuja pia wa kuulinda mmea ukuapo! Utafikia hatua ya kuwa mti na Utazaa matunda!

Nakupenda Tanzania nchi ya Mama yangu!
 
yaa inawekekana akajiubu kweli lakini je itasaidia?//// kwani kima cha chini hakimhusu jk yeye ni mtu wa kima cha MAJUUUUU..........................hizi naamini ni kelele za chura tu......lakini tuendelee kupigana naamini ipo siku tutafanikiwa tusikate tamaa wajomba eeee
 
Majibu anayotakiwa kujibu Mgaya ni mawili tu.
1.Tarehe fulani tunagoma
2.Mgomo umepeleruka.
zingine hizi watanzania tunapenda sana kusikia mbwembwe zisizo na tija.
 
Kasemaje na wapi? leteni habari kamili, sasa hii breaking news gani? ama hatuelewi maana ya breaking news? hata news alert huwa zinajitoshereza ama kwa kutoa link yenye habari kamili! sasa sisi hata kitu hakijaiva hao tayari tushakurupuka JF taratibu wajameni!
 
Lazima ajibu ni kwa nini jamaa aisakame tucta na alitaje jina la mgaya kana kwambwa mgaya ndio mwenye tucta, nayeye mgaya ana moyo wa nyama si wa chuma
 
JK anasikitisha sana, wasaidizi wake wanamfanya kama babu yao,..au paka wanamchezea sharubu tu, maana walimuingiza chaka kwenye kukabidhi cheki, wakamwingiza chaka kwenye kukabidhi gari la wagonjwa,..na kama haitoshi sheria ya uchaguzi chaka,,. kwenye tucta kadanganywa kuhusu muda, maskini JK...
 
Tamko la TUCTA juu ya hotuba ya Mh. Rais...
 

Attachments

  • UFAFANUZI WA TUCTA JUU YA HOTUBA YA MH RAIS ALIYOITOA TAREHE 03 5 2010.doc
    300.5 KB · Views: 291
Back
Top Bottom