Nibeebe nibeebe nibembeleze unibeebe…

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Jamani hii miito mingine kwenye simu inatuponza..!!! Jamaa mmoja alikuwa anapata kinywaji sehemu, akaenda msalani akaacha simu kwenye meza aliyokuwa amekaa.

Ghafla simu yake ikaanza kuita…..”NIBEEBE NIBEEBE NIBEMBELEZE UNIBEEBE… NICHUKUE UNIBEEBEE…” mtu mwingine akawa anapita kando ya meza hiyo akaisikia, akaibeba kweli….. nani wakulaumiwa…???
 
Haaa Haaa haaa! Naona uko kwenye fani yako King'wendu! Inabidi tuombe waanzishe jukwaa la vichekesho! we unafaa kuliongoza!

Hakuna wa kulaumiwa coz jamaa nae alitimiza alichoambiwa!
 
Hizi zinawaumbua wengi sana mpaka misikitini utazisikia na maustadhi wengine wamepigwa sababu ya rimg tune hizo kwani simu unakuta inaanza kuita katikati ya sala wakati kainama na watu wote wapo kimya!
 
jamani hii miito mingine kwenye simu inatuponza..!!! Jamaa mmoja alikuwa anapata kinywaji sehemu, akaenda msalani akaacha simu kwenye meza aliyokuwa amekaa.

Ghafla simu yake ikaanza kuita….."nibeebe nibeebe nibembeleze unibeebe… nichukue unibeebee…" mtu mwingine akawa anapita kando ya meza hiyo akaisikia, akaibeba kweli….. Nani wakulaumiwa…???


huyo jamaa hata hajaiba, katekeleza wito aloambiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom