Niache, nina mawazo yangu!

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Wasalaam,

Mimi ni kijana mwenye familia ya mke mmoja na mtoto. Sijwahi kuwa na ugomvi na mke wangu isipokuwa tangu mwezi uliopita, amekuwa yuko kimya sana (amepoa sana) na hachangamki hata ukimsemesha au kumtania. Jibu lake limekuwa "Niache bwana, nina mawazo yangu!". Nimetafakari mwenendo wangu kwa muda mrefu hauna mashaka yeyote.

Najiuliza tatizo ni nini maana hali yake hii inanisikitisha na kuniyumbisha kisaikolijia. Naomba mawazo na ushauri wenu wa dhati ndugu zangu kuhusu nini cha kufanya ili nijue tatizo lake. Wenzangu wake zenu wamewahi kuwajibu hivyo? Mlifanyaje?

****** Imetumwa na Johnson, Mara Musoma ********
 
Ki ukweli dunian kila mtu ana mawazo yake, cha msingi kaa chini mueleweshe unavyoumia unapomuona yeye yupo vle na akuambie tatizo nn? Unaweza ukaona upo correctly bt nt as u knw dat no body's perfect
 
Kuna vitu binadamu hua tunavyo na ni vya kawaida tu.
Mfano kuna wakati hua binadamu huhitaji a lonely place , atafakari yaliopo kichwani mwake, na si lazima kila kilicho kichwani mwa mtu akidhihirishe.
 
Aisiiiii!! hili ni la kiundani zaidi... ningeweza kukuuliza maswali lakini tayari yamejibiwa kwenye ujumbe wako maana unasema mwenendo wako hauna mashaka... Tu je unahakika kuwa vile unavyoona kuwa mwenendo wako hauna mashaka ndivyo mwenzio anavyoona pia? isije kuwa wewe ndo unaona halafu yeye anakutilia shaka!!
Kifupi ni kwamba lipo jambo, mimi na wewe hatujui.. hebu jitoe siku moja, mvizie wife akiwa katika mood nzuri, msuprise na kazawadi kokote ka kimahaba, na akiwa katika furaha wakati anapokea, mwombe utoke nae out na umwambie kuwa una mazungumzo nae!! mpeleke mahali penye hadhi kubwa kidogo, namanisha pazuri na patulivu, iwe hotelini au ufukweni ambapo mtapata chakula na kuongea mengi, mkumbushe jinsi mlivyokuwa mmeanza mahusiano na vitu vingine ambavyo vitamfanya afurahi na kutabasamu
mkiwa katika maongezi mwambie kwa upole na unyenyekevu kuwa unaona tatizo katika ndoa kwa mida hii, ila usimlaumu yeye, useme tu unajisikia vibaya na ungependa mzungumze ili mpate suluhisho la pamoja nae, naamini atafunguka na utajua nini kinamtatiza.
Ukiona zaidi ya hapo hataki basi ujue ana gubu tu na si rahisi kumbadili
 
Songíto;3456491 said:

Hili nalo neno!
 
ndugu
hayo ni matatizo ya kawaida kabisa katika ndoa,jaribu kumtoa mkeo weekend hii muende mbali na myumbani tena mlale hukuhuko ili mpate muda wa kuzungumza katika mazingira tofauti,sometimes mazingira ya sehemu moja nayo yanaweza kuchangia,pia angalia sehemu anazopendelea kwenda mkeo ndio umpeleke,oda vyakula na vinywaji anavyovipendelea and things like that, natumai mtaongea vizuri na atakueleza
 
Ungemwambia kuwa: "Mwanamke anapaswa kufanya anachoambiwa na mke wake" maana hicho ndicho unaamini.

Sasa sisi tushauri nini hapo!
 
Ungemwambia kuwa: "Mwanamke anapaswa kufanya anachoambiwa na mke wake" maana hicho ndicho unaamini.

Sasa sisi tushauri nini hapo!

Kaunga haujaeleweka aisee, huyu Bwn Johnson wa Musoma anaomba ushauri na sidhani kama hapa atakuwa amekuelewa!
 
Achunguze na marafiki za mkewe. Asijichunguze mwenyewe tu. Huenda kuna jambo kaambiwa kumhusu lisilofaa. Watu sometimes wana wivu na amani ya wenzao.
 
Wasalaam,

Mimi ni kijana mwenye familia ya mke mmoja na mtoto. Sijwahi kuwa na ugomvi na mke wangu isipokuwa tangu mwezi uliopita, amekuwa yuko kimya sana (amepoa sana) na hachangamki hata ukimsemesha au kumtania. Jibu lake limekuwa "Niache bwana, nina mawazo yangu!". Nimetafakari mwenendo wangu kwa muda mrefu hauna mashaka yeyote.

Najiuliza tatizo ni nini maana hali yake hii inanisikitisha na kuniyumbisha kisaikolijia. Naomba mawazo na ushauri wenu wa dhati ndugu zangu kuhusu nini cha kufanya ili nijue tatizo lake. Wenzangu wake zenu wamewahi kuwajibu hivyo? Mlifanyaje?

****** Imetumwa na Johnson, Mara Musoma ********
Baada ya kujaribu ushauri mwingi ulopewa na wachangiaji mbalimbali, hebu kaa chini ufikirie hayamaswali yafuatayo: Wanawake wengi wanapenda kuwa na security ya maisha. Je mnaishi mjini? Je mtoa thread anaishi na wazxazi wake au hawa wazazi wako mbali na mji mnaoishi? Kama wazazi wa mwanaume wanaishi mbali na mji mnaoishi, je umeshapata kumpeleka mkeo huko kuwaona wazazi? (wakwe wa mkeo) Je mahusiano yako(mleta thread) na wazazi wa mkeo yakoje? Kama mahusiano na wakwe(pande zotembili) hayako sawa, linawafanya wanawake wengi kukosa amani.
 
dondosha kipigo kwanza cha suprise lazima ataongea kinachomsibu tu kwa hasira na utakuwa tayari umejua...
 
Kwa namna nyingine inawezekana mkeo ana 'victim psychological disorder' ambayo huchangiwa na inferiority complex ambayo anayo(yani ndo alivyo/tabia yake). Sasa mtu wa aina hii anapenda kujiona/kuonekana victim(muathirika) kwenye kila jambo(especially ugomvi), ugomvi mwingine umeisha, au anaelewa kabisa cyo issue na mara nyingine anaelewa kuwa hata wewe umekuathiri ila yeye anataka umbembeleze, ujue yeye ndio kaumia sanaaa na matendo yako. Kwa kifupi hawa watu hujulikana pia kama drama queens(kama unawotch futbol mwangalie luis nani wa man u-nimmojawapo wa hao. akiguswa kidogo2 shida!). Madhara ya hii tabia ni makubwa, kwa sababu watu wakikuzoea hata kama ukiathirika kiukweli hawatokuchukulia serious(kasome habari ya 'the boy who cried wolf!-au just google it'). Sasa kwa hapa hili siyo dogo la kukaa mara1 mmalize, kaa naye mara kwa mara mueleweshe madhara ya hiyo tabia (ukianza kila mazungumzo na mke wangu nakupenda sana na ni baraka kuwa na mke kama wewe...)
NB: wasichana wengi sana wako hivi
 
Kama si mja mzito
Basi lipo jambo ambalo yeye au amelihisi au kuambiwa na mtu au ameona mabadilko fulani kwako

Pata muda mkiwa na maelewano mazuri hasa kwa wewe kushuka ili afunguke kidogo kwako ndipo utaweza kumsaidia na wewe kuwa kwenye furaha ya kawaida ya ndoa yako

Kila raha huwa na gharama yake , usiogope gharama ya kutafuta amani ya ndoa yako
 
Back
Top Bottom