Ni Zanzibar ipi wanaitaka?

Mtu mzima wacha ujinga ,hivi kuna pasi za Tanganyika ? au ndio wataka tuburuza sie tusio na pasi ?

Mnapenda kusafiria Pasi za Jamhuri ya Muungano wa TAnzania au mnataka Nchi ya Zanzibar iwe na pasi zake za kusafiria? ni swali rahisi ambalo halihitaji kumuitwa mtu mjinga au vyovyote vile.
 
hakuna haja ya ku-panic. Wazanzibar hawataki muunganona Tanganyika, lakini wakikubaliana wanaweza kufanya muungano na Kenya...

haya ni mambo ya makubaliano...WE MISS TREATED ZANZIBARIS ,THAT WAS THE ISSUE...WE TOOK THEM JUST LIKE ANY PART OF TANGANYIKA...ZANZIBAR IS A NATION...We need to learn to accept the facts.

What about us Tanganyikans, we are much more mistreated than our Islands counterparts. We have lost our identity completely, hatuna passport, wimbo wa taifa, bendera, rais, bunge na vitu vingi tu, we are almost nothing. Sasa wanaoleta hoja ya mistreatement hawasemi ukweli. The thing is jamaa wataendelea kulalamika kila siku no matter what. The prefect union between Tanganyika and Zanzibar is one goverment. Zanzibar ni walalamishi siku zote. Watakuja kujifunza siku muungano utakapokuja kufa.
 
Huo Muungano niunavyo kama ushakufa wanaoendesha serikali ya Muungano ni genge tu linalolindana na wanafanya watakavyo.
Hivi nyie waTanganyika mupo upande wa CCM nin ? Maana wao ndio wanaoidhibiti hiyo serikali ,kuwepo kwa serikali hio ndio uhai wa CCM siku serikali hiyo ikizama ndio mwisho wa utawala wa sultan CCM
 
Hivi Zanzibar wangependa kuwa na pasi zao za kusafiria kwenda ng'ambo kwa sababu wao ni nchi vile vile na hakuna sababu ya kutumia pasi ya Tanganyika?
kabla ya muungano walikua na pass zoa na kadi za uraia wa zanzibar...kadi za uraia zimeacha kutumika miaka kama 25 iliyopita...
hizi pass tunazotumia sasa ni za tanzania na sio Tanganyika.... lakini haya mambo yatarudi sio muda mrefu sana...
 
What about us Tanganyikans, we are much more mistreated than our Islands counterparts. We have lost our identity completely, hatuna passport, wimbo wa taifa, bendera, rais, bunge na vitu vingi tu, we are almost nothing. Sasa wanaoleta hoja ya mistreatement hawasemi ukweli. The thing is jamaa wataendelea kulalamika kila siku no matter what. The prefect union between Tanganyika and Zanzibar is one goverment. Zanzibar ni walalamishi siku zote. Watakuja kujifunza siku muungano utakapokuja kufa.
zanzibar have been a nation for more than 5 hundred years...kabla ya muungano Zanzibar ilikua tayari ni Taifa...Wamarekani walishafungua ubalozio Zanzibar mwaka 1800s...Zanzibar walikua wana kiti chao umoja wa Mataifa...Zanzibar walikuwa wana sarafu yao wakati sisi Tanganyika tulikua bado tunauza na kununua kwa kubadilishana bidhaa... Tanganyika iliuliwa na Nyerere...Kwa tamaa ya kuwa ataigeuza Zanzibar kuwa ni sehemu ya Tanganyika ambayo iegeuzwa na kuwa Tanzania... Matatizo ya muungano tumeyafanya sisi Tanganyika kwa kuanza kubadilisha kidogo kidogo makubaliano ya muungano...Mambo ya muungano yalikua 11 hapo awali, sasa yanakaribia 40... kwahiyo kila wanachotaka kufanya Zanzibar wanaambiwa hilo ni la muungano kwahiyo hawana haki...sasa imefikia wakati wamechoka kuburuzwa.
 
Mnapenda kusafiria Pasi za Jamhuri ya Muungano wa TAnzania au mnataka Nchi ya Zanzibar iwe na pasi zake za kusafiria? ni swali rahisi ambalo halihitaji kumuitwa mtu mjinga au vyovyote vile.

wazanzibar wakitumia pass zao itakua nafuu kwao...wao ni kidogo sana uwezekano wa kufanya makubaliona ya visa free na nchi nyengine ni rahisi zaidi...nadhani itakua advantage kwa upande wao...Mw.kijiji unaonekana hajawahi kufika Zanzibar au huijui ...Tanganyika ndio yenye mazonge sio wenzetu.
 
Mkuu Mdondoaji asante kwa jibu lako sasa twende taratibu.

Hizo sehemu mbili nilizo highlight mkuu ndizo zime niinterest sana na zinaonyesha kwa kiasi kikubwa nini nilicho taka kusema. Hiyo sehemu ya kwanza ya umasikini mkuu nakubaliana na wewe ndiyo sababu kuu ya haya yote yanayo endelea. Je hapa hauoni kwamba viongozi na serikali ya Zanzibar imeshindwa kuwa letea maendeleo Wazanzibar kwa hiyo wana tumia kisingizo cha kulaumu umasikini huo kwa muungano ili kutwishwa mzigo wa lawama na kuishushia Muungano? Na ndiyo maana nikasema chakula kikipikwa huwezi jua kime pikwaji na mpishi ana nia gani. In short the Zanzibar government has failed to deliver and they have no other excuse to give it's people except to blame it on the Union.

Kuhusu sehemu ya pili mkuu ya kusema wanavuka bahari na kuona maendeleo huku Bara mkuu with all due respect let's be serious. Tanzania Bara ina maendeleo makubwa kiasi gani kiasi cha kuona wao wameachwa sana? Je wakija Bara ni sehemu gani hizo wanazo tembelea maana ina wezekana hawaja fika Manzese, Kariako, Keko au vijijini huko. Isije ikawa wanaishia Posta au Oysterbayna kuona kieneo kidogo tu waka chukulia hiyo ndiyo hali kote Tanzania bara.

O.k. fair enough kama hivyo ndivyo wanavyo dhani. Kama wanaona Muungano hauna faida yoyote na wana taka kuwa nchi basi kwa nini wana fall short ya kudai uhuru kamili? Kwa nini waji nga'tenga'te kusema wana taka Muungano na kuirekebisha na wengine mnakuja na kusema Muungano hauna maana na mna taka nchi? Hapa ndipo ninapo sema wananchi na viongozi mna nia tofauti hamjui tu maana wananchi wanasema wana taka Zanzibar nchi na Muungano hauna manufaa lakini huto sikia kiongozi wa Zanzibar hata mmoja akiwa that direct.
mimi nimemuelewa vizuri mdondoaji...chengine zaidi nimeishi Zanzibar miaka mingi nawaelewa wazanzibar vizuri sana... tatizo kubwa la viongozi wa Zanzibar wa chama tawala CCM ambacho makao makuu yake yako bara... Mabadiliko ya utawala yakifika ndio wanzanzibari utawasika wazi wazi wanaukana muungano... na hii haina muda mrefu... kwani mara zote zile sera za Nyerere zilikua zinatumika bado dhidi ya viongozi wa CCM Zanzibar ambao wamekua na mawazo tofauti kuhusu muungano. Mambo ambayo yamewafika wengi ni kufukuzwa kazi na bila ya kupewa haki zako...hii imesababisha viongozi waliopo madarakani kuuangalia maslahi yao binafsi...lakini hata hivyo imefikia wakati na wao pia wamechoka... kilicho saida zaidi ni pale Mh,PİNDA aliposema Zanzibar sio nchi, na mafuta ya muungano.
kwahiyo kiongozi wa CCM Zanzibar kama hawezi kutetea mambo haya mawili huyo wanamuita mtumishi wa Tanganyika...sasa imefika wakati wemeungana na wamekua kitu kimoja... ninavyo amini mimi muungano wa serekali mbili haupo tena , ziwe tatu au basi...wanzibari hawataki tena huu muungano wa sasa hivi wamechoka. mambo ya muungano yalikua 11 hapo awali sasa yanakariba 40...wanahisi wamebanwa kupita kiasai na huu muungano.
 
Zanzibar...oh Zanzibar..! Ulikuwa nchi kamili yenye madaraka yake ni kipi kilichokufikisha hapa ulipo? Zanzibar oh Zanzibar,beautiful island of Africa!Ujamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Mkianzisha Zanzibar nakuja kuomba uraia.Napenda kuishi visiwani mamaaaaaaaaaaaaa...!!!
 
jb02gj.jpg
 
Unajua kiini cha uzanzibari kutaka kutambulika unakuwa driven na umaskini unaoendelea huko zanzibar. Wazanzibari wengine maisha yao na maendeleo yamekuwa yakiporomoka kadiri siku zinavyoenda mbele. Pia hata zile ajira walizokuwa wanazitegemea zimekuwa zikiyoyoma kila siku. In short mzanzibari wa kawaida amekosa matumaini ya kuishi nchini zanzibar. Sasa wakivuka barabara kuja Dar wanaona maendeleo kwa kiwango kikubwa kinachopelekea wajione wametengwa na serikali ya muungano.
Vongozi mara nyingi wanaghiribu watu kwa kutumia matatizo hewa kuonekana kuwa halisi. Katika hstoria wanasiasa wenye 'charisma' ya kusema wamepeleka nchi zao kwenye matatizo makubwa kuliko mwanzo. Km. Hitler na wayahudikuwa matajiri kuliko wajerumani asilia, Habyarimana na interahamwe yake kuhusu watutsi. Sasa huko kuona majengo yanajengwa Dar, masikini na si Tanganyika yote, ndio mtizamo wa uchochezi.
Zanzibar kama wanataka kuwa soverign state kama Monaco na Luxembourg si waseme tu. Tanagnyika itahandle, kwa makubaliano, kwa niaba yao yale wtakayoona hawawezi. Hivyo hatuna sababu ya kuwa na Tanzania tenge. Kama noma naiwe noma ndivyo waimbaji wa taaabu watuambiavyo. Hali ya hewa imeshachafuka.
 
zanzibar have been a nation for more than 5 hundred years...kabla ya muungano Zanzibar ilikua tayari ni Taifa...Wamarekani walishafungua ubalozio Zanzibar mwaka 1800s...Zanzibar walikua wana kiti chao umoja wa Mataifa...Zanzibar walikuwa wana sarafu yao wakati sisi Tanganyika tulikua bado tunauza na kununua kwa kubadilishana bidhaa... Tanganyika iliuliwa na Nyerere...Kwa tamaa ya kuwa ataigeuza Zanzibar kuwa ni sehemu ya Tanganyika ambayo iegeuzwa na kuwa Tanzania... Matatizo ya muungano tumeyafanya sisi Tanganyika kwa kuanza kubadilisha kidogo kidogo makubaliano ya muungano...Mambo ya muungano yalikua 11 hapo awali, sasa yanakaribia 40... kwahiyo kila wanachotaka kufanya Zanzibar wanaambiwa hilo ni la muungano kwahiyo hawana haki...sasa imefikia wakati wamechoka kuburuzwa.
Actually Zanzibar ilikuwa mpaka Oman,Sofala Kilwa Mombasa na Lamu. Sasa ni Zanzibar ipi inayotakiwa leo?
 
Wanaitaka nchi "yao" ya Zanzibar; Wanataka kurudia "utukufu wa Zanzibar" kwa kuwa hapa walipo sasa hawaoni manufaa "yoyote" kwa Zanzibar. Wanasema wanaitaka nchi yao waliyonyang'anywa na Wadanganyika (ati Watanganyika). Wanataka warudishiwe nchi yao waliyonyang'anywa na Nyerere na watu wa bara.

Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?

  • Zanzibar ya historia ya kale (Zenj - nchi ya weusi?) ambayo ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba bali na mwambao wa Afrika ya Mashariki
  • Zanzibar ya Sultani(ambaye naye utawala wake ulizidi mipaka ya Unguja na Pemba)
  • Zanzibar ya Sultani chini ya Mwingereza
  • Zanzibar ya baada ya Uhuru na Sultani akiwa bado ni Mkuu wa Nchi na serikali ya Mseto
  • Zanzibar ya Mapinduzi kabla ya Muungano
  • Zanzibar "mpya" ambayo haijawahi kuwepo yaani ya baada ya muungano

Ni ipi hasa wanayoitaka? Ni ipi hasa Zanzibar "proper". Isije kuwa ni kama nchi ya ahadi ambayo iko katika fikra za watu tu lakini haijawahi kuwepo; yaani ile nchi imiminikayo maziwa na asali na kwamba watu wa bara na dunia nzima wanataka kuwanyang'anya Wazanzibari. Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa Mzanzibari ni nani hasa?
Hawajui walitakalo, wao ni kupiga makelele tu kwamba wanaonewa............ wanadhurumiwa............ wananyanyaswa................. WAKIACHWA PEKE YAO HAO WATAKUFA KWA KUKOSA UMEME............
 
Hawajui walitakalo, wao ni kupiga makelele tu kwamba wanaonewa............ wanadhurumiwa............ wananyanyaswa................. WAKIACHWA PEKE YAO HAO WATAKUFA KWA KUKOSA UMEME............

zanzibar walianza kutumia umeme kabla ya tanganyika...
 
Hawajui walitakalo, wao ni kupiga makelele tu kwamba wanaonewa............ wanadhurumiwa............ wananyanyaswa................. WAKIACHWA PEKE YAO HAO WATAKUFA KWA KUKOSA UMEME............

Mtasema mchana usiku mtalala ngoma ya sikinde inaendeleaa ,wandugu haya mambo yeshakuwa makubwa kwa kingunge yeyote yule kutoka Dodoma kutokeza pua yake.

Yaani sasa mambo ya Zanzibar ni mbele kwa mbele tu ,machogo mmefuliya bwa ha ha ha :lol:
 
Wanaitaka nchi "yao" ya Zanzibar; Wanataka kurudia "utukufu wa Zanzibar" kwa kuwa hapa walipo sasa hawaoni manufaa "yoyote" kwa Zanzibar. Wanasema wanaitaka nchi yao waliyonyang'anywa na Wadanganyika (ati Watanganyika). Wanataka warudishiwe nchi yao waliyonyang'anywa na Nyerere na watu wa bara.

Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?

  • Zanzibar ya historia ya kale (Zenj - nchi ya weusi?) ambayo ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba bali na mwambao wa Afrika ya Mashariki
  • Zanzibar ya Sultani(ambaye naye utawala wake ulizidi mipaka ya Unguja na Pemba)
  • Zanzibar ya Sultani chini ya Mwingereza
  • Zanzibar ya baada ya Uhuru na Sultani akiwa bado ni Mkuu wa Nchi na serikali ya Mseto
  • Zanzibar ya Mapinduzi kabla ya Muungano
  • Zanzibar "mpya" ambayo haijawahi kuwepo yaani ya baada ya muungano

Ni ipi hasa wanayoitaka? Ni ipi hasa Zanzibar "proper". Isije kuwa ni kama nchi ya ahadi ambayo iko katika fikra za watu tu lakini haijawahi kuwepo; yaani ile nchi imiminikayo maziwa na asali na kwamba watu wa bara na dunia nzima wanataka kuwanyang'anya Wazanzibari. Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa Mzanzibari ni nani hasa?

Zanzibar inayozungumzwa ni kama ilivyoanishwa na katiba yetu mpya na kama ilivyo katika mkataba wa muungano.Simple as that!

@Kibunango
Nenda kasome tena historia kama unajidanganya kuwa Zanzibar haikuwa nchi ilikuwa ni sehemu ya Tanganyika.Nadhani fuatilia zaidi historia ili ujue taifa la Tanganyika lilianza lini na taifa la Zanzibar lilianza lini.Ukimaliza hapo nadhani utagundua kuwa Tanganyika si nchi yenye natural boarders. Haswa upande wa kaskazini karibu na wamasai utaona ni mstari ulionyooka umepigwa na mzungu na kukata kabila ya la wamasai kati-kati.

Hili la natural boarders ndio haswa tatizo la watu wa Tanganyika kutokufahamu.Hivyo kesi ya mtanganyika kutokukuona umuhimu wa kupotea taifa lake ni logic hapo, kwani taifa lenyewe halikuwapo tokea awali kama si wazungu.

Aidha kwa Zanzibar ni tofauti, hadi leo mimi sitaki hata kusikia neno linaitwa Tanzania.Bado nimebakia mzanzibari, na nitakufa mzanzibari.Huo muungano munaopigia kelele, kwanza nadhani mungelianzia na kutafuta ratification documents kutoka Zanzibar.Mukiweza pata ushahidi huo kuwa Zanzibar ilikubali muungano, then ndio tuendelee hapo.

Lakini kwa Mwanakijiji na wengi ambao ni short-minded, hutaka kuanzia na katiba mara Mapinduzi!.Acheni kujichanganya, Mapinduzi yalifanywa na Nyerere akipatikia watu kutoka pale Tanga kupeleka watanganyika kupindua Serekali halali ya watu wa Zanzibar.

Sasa hapo watakuja wengine na kudai ni dhana za ubaguzi.Naona wengi wenu munazungumza pumba tupu, inawezekana hata hamujawahi kufika Zanzibar.Mumeisoma Zanzibar kwenye kitabu cha Nyerere :confused2:

Anyways, long story short kwa mtazamo wangu Zanzibar haina matatizo yoyote...Wenye matatizo ni watanganyika, na ndio tatizo liliopo.Tokea asubhi Tanganyika inakodolea macho visiwa hivyo kuwa ni sehemu yake...but thats just a dream of yours I guess!
 
Wanaitaka nchi "yao" ya Zanzibar; Wanataka kurudia "utukufu wa Zanzibar" kwa kuwa hapa walipo sasa hawaoni manufaa "yoyote" kwa Zanzibar. Wanasema wanaitaka nchi yao waliyonyang'anywa na Wadanganyika (ati Watanganyika). Wanataka warudishiwe nchi yao waliyonyang'anywa na Nyerere na watu wa bara.

Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?

  • Zanzibar ya historia ya kale (Zenj - nchi ya weusi?) ambayo ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba bali na mwambao wa Afrika ya Mashariki
  • Zanzibar ya Sultani(ambaye naye utawala wake ulizidi mipaka ya Unguja na Pemba)
  • Zanzibar ya Sultani chini ya Mwingereza
  • Zanzibar ya baada ya Uhuru na Sultani akiwa bado ni Mkuu wa Nchi na serikali ya Mseto
  • Zanzibar ya Mapinduzi kabla ya Muungano
  • Zanzibar "mpya" ambayo haijawahi kuwepo yaani ya baada ya muungano
Ni ipi hasa wanayoitaka? Ni ipi hasa Zanzibar "proper". Isije kuwa ni kama nchi ya ahadi ambayo iko katika fikra za watu tu lakini haijawahi kuwepo; yaani ile nchi imiminikayo maziwa na asali na kwamba watu wa bara na dunia nzima wanataka kuwanyang'anya Wazanzibari. Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa Mzanzibari ni nani hasa?

Zanzibar iliyo huru na choyo na hasada za wale wasio na utaifa!!!

Zanzibar........... Date of birth= long time ago

Tanzania........... Date of birth= 1964.

Hesabu hii ndio tatizo!!
 
..sasa Maalim Seif kadai akichaguliwa ataimarisha muungano!!

..mimi nadhani wanasiasa wa Zenj wanawachezea akili wapiga kura wao.

..kwanini suala la kuwa na muungano, ama la, halikupigiwa kura ya maoni, sambamba na suala la kuundwa kwa serikali ya mseto?

..Muungano wa serikali tatu haufai kwasababu Tanganyika is too big compared to Zenj.

..muungano huu ni bora ukavunjwa na badala yake tushirikiane na wa-Zenj kupitia EAC.

NB:

..kila siku wanadai wanashughulikia kero, sasa kero ya Zenj kuwa ndogo mno, na Tanganyika kuwa kubwa kupita kiasi, wataishughulikia namna gani?
 
Back
Top Bottom