Ni Woga gani huu

Mtaalaamuna

Member
Feb 19, 2011
21
0
Bado naendelea kufikiri jambo lililomfanya mkuu wa nchi kutangaza kuwa anataka kuondolewa madarakani kwa nguvu.

Si jambo la kumwingia mtu akilini kwa Rais kusema jambo zito kama hilo la kuwatisha wananchi kuwa nchi inataka kupinduliwa, ukizingatia kuna vyombo mbalimbali vinavyofanya kazi zake kiufasaha na umakini, na kama ndivyo basi hizo njama za kupindua serikali zingehesabika ni UHAINI na si vinginevyo.

Sidhani pia kama Mtoto akiona baba yake analewa kila siku ilhali yeye hana madaftari ya shule, hajalipiwa ada nk, akimshinikiza baba yake kuwa amlipie ada na kununua vifaa vya shule anakuwa amentusi na kumsaliti.

Ninacho kiona ni WOGA na KUTOJIAMINI kwa Mkuu wa nchi
 
Anafahamu fika kuwa Dr.Slaa ni tishio kwake na tamko lake halina maana anataka Watz wamwonee huruma kuwa anabanwa pasipo sababu na Chadema. Ila yeye ni miongoni mwa viongozi wengi ndani ya serikali wasiolala usingiza kila wakisikia dr Slaa. na bado!!!!!!!
 
Mkuu usimalizie kushangaa ili nami niunganishe mshangao wangu humo humo alaf tuhitimishe mshangao kwa pamoja. Hivi ni vioja vya nchi ya kusadikika ya TZ,hapa usalama wa taifa uko wapi kama watu wanakaa wanapanga kuipindua govt.na watawala wanakaa kuliakulia tu. Wasiri anasimama anakaa na kuueleza uma kuwa cdm wamepewa hela nyingi ili kuipindua nchi! Ivi sheria zinazohusu fedha haramu zimefutwa lini Tanzania?ukisoma Anti Money Loundering Act,ukasoma sheria za uhujumu uchumi,utashindwa kuelewa kama taifa lina serikali,mkuu anadai anapinduliwa,hapa si ndo Lema pia adai tumfanyeje Jk kama ataonekana kulidanganya taifa kuwa kuna wahaini? Kumbuka ikulu chini ya mkurugenzi wa mawasiliano Salva alishalitangazia taifa kuwa Dr.Slaa amezeeka vibaya na ameweuka,je mbona wanaendelea kumuandama?au wameamua kumjibu regardless kuwa ni 'mweu'?je mbowe?naye ni nani sasa! Sophia simba aliwaasa wanawake watunyime Unyumba kama tukìipenda chadema,iyo akili au tope kichwani? Mh.dr.slaa usikate tamaa,kuikomboa taifa ni kazi sana,tulia maana wee ndo mkombozi wetu. Cdm ni chama pekee kinachoweza kunikomboa mimi kama maskini. Nawapongeza cdm,nawashangaa watawala wetu!
 
Ukiangalia historia za africa utagundua, kama nchi ina machafuko au wasiwasi wa kupinduliwa au kuwepo na uasi basi rais wake hathubutu hata kutoa mguu wake kwenye nchi yake hata kwenda kwa jirani yake anaepakana nae, kwa hofu ya kupinduliwa atakubakishwa huko huko nje, Mbona JK tangu alipo toa tamko lake mpaka leo yeye ni kiguu na njia anakwea pipa hajatulia huku wabongo wanahali mbaya ya maisha. Kama maneno yake yangekua na ukweli angetoa mguu bongo TZ???

Moto ule ule Tufanye mikutano na maandamano kwani lengo letu si kupindua nchi bali kutaka GVT ione uchungu wa people wake wana hali mbaya.
 
Anafahamu kuwa aliingia mjengoni ndivyo sivyo, mwenyewe kustahili akitaka kuingia patakuwa hapatoshi.
 
Hana uoga wala nini ni siasa tu. Wananchi hawatishwi nyau sasa hivi. Amani wakati mkono hauendi kinywani?
 
Bado naendelea kufikiri jambo lililomfanya mkuu wa nchi kutangaza kuwa anataka kuondolewa madarakani kwa nguvu.

Si jambo la kumwingia mtu akilini kwa Rais kusema jambo zito kama hilo la kuwatisha wananchi kuwa nchi inataka kupinduliwa, ukizingatia kuna vyombo mbalimbali vinavyofanya kazi zake kiufasaha na umakini, na kama ndivyo basi hizo njama za kupindua serikali zingehesabika ni UHAINI na si vinginevyo.

Sidhani pia kama Mtoto akiona baba yake analewa kila siku ilhali yeye hana madaftari ya shule, hajalipiwa ada nk, akimshinikiza baba yake kuwa amlipie ada na kununua vifaa vya shule anakuwa amentusi na kumsaliti.

Ninacho kiona ni WOGA na KUTOJIAMINI kwa Mkuu wa nchi
Huyo ndio asiye na "Kiherehere"......... ! Na anasema hivyo sasa kuwaambia wafuasi wake waamke maana hata yeye anakosa usingizi siku hizi....! Mbona Dr. Slaa na CDM walikuwa wasingemnyima usingizi?
 
Mkuu usimalizie kushangaa ili nami niunganishe mshangao wangu humo humo alaf tuhitimishe mshangao kwa pamoja. Hivi ni vioja vya nchi ya kusadikika ya TZ,hapa usalama wa taifa uko wapi kama watu wanakaa wanapanga kuipindua govt.na watawala wanakaa kuliakulia tu. Wasiri anasimama anakaa na kuueleza uma kuwa cdm wamepewa hela nyingi ili kuipindua nchi! Ivi sheria zinazohusu fedha haramu zimefutwa lini Tanzania?ukisoma Anti Money Loundering Act,ukasoma sheria za uhujumu uchumi,utashindwa kuelewa kama taifa lina serikali,mkuu anadai anapinduliwa,hapa si ndo Lema pia adai tumfanyeje Jk kama ataonekana kulidanganya taifa kuwa kuna wahaini? Kumbuka ikulu chini ya mkurugenzi wa mawasiliano Salva alishalitangazia taifa kuwa Dr.Slaa amezeeka vibaya na ameweuka,je mbona wanaendelea kumuandama?au wameamua kumjibu regardless kuwa ni 'mweu'?je mbowe?naye ni nani sasa! Sophia simba aliwaasa wanawake watunyime Unyumba kama tukìipenda chadema,iyo akili au tope kichwani? Mh.dr.slaa usikate tamaa,kuikomboa taifa ni kazi sana,tulia maana wee ndo mkombozi wetu. Cdm ni chama pekee kinachoweza kunikomboa mimi kama maskini. Nawapongeza cdm,nawashangaa watawala wetu!

uko dipu ndugu! na mimi naunganisha mshangao wangu na wako na wake.. kwaivo kuna mishangao mitatu...
 
Huwa hana hoja za kujibia hoja, anatafuta huruma kwa kuchezea dhamiri za wananchi, kwa upande mwingine ni dhaifu na mlalamishi kama wale wengine wanaolalamika toka enzi zile.
 
Rais mwoga anatuaibisha haoni wenzake Mbarack, Sadam hadi anatolewa madarakani bado anasema yeye ni rais, huyu kutikiswa kidogo tu analia lia.
 
Back
Top Bottom