Nimebahatika kuingia katika ofisi mbalimbali za serikali na hata baadhi ya mahakama zetu jijini Dar es salaam na nilishangaa kuona matangazo mbalimbali katika kuta za ndani za baadhi ya ofisi hizo yakisema kwa maandishi makubwa "HATUPOKEI RUSHWA".
Jambo la kushangaza ni kuwa hata wakuu wa ofisi hizo wameafiki kuwepo kwa matangazo hayo. Jambo lingine la kushangaza ni kuwa baadhi ya ofisi hizo ndizo zimekuwa zinalalamikiwa sana na wananchi kuhusu ulaji/upokeaji rushwa.
Swali langu ni kuwa je kuna yeyote anayefahamu ofisi ambayo inatangaza kuwa wanapokea rushwa? Ningependa kuitembelea kama ipo!