Ni wakati wa tanzania kusikia sauti ya MUNGU

kasyabone tall

JF-Expert Member
Sep 13, 2009
254
59
Kwa hali ya nchi sasa ambayo imelemewa na misukosuko kuanzia kwenye chama hadi serikalini. Nchi imekumbwa na ufisadi wa kupita kiasi, ukandamizaji, uongo na kukithiri kwa uroho wa madaraka. Kwa sasa tanzania ina uvumilivu lakini ukweli ni kuwa hakuna amani.
Leo tunashuhudia watu wako benki kuu ya tanzania wanacheza dili la kuiba hela, mawaziri wanaingia mikataba kwa lengo la kupata pesa nyingi, mahakimu wanakula rushwa. Mapolisi usiseme. Chombo kama TAKUKURU ambacho kina kazi ya kuzuia rushwa kiongozi wake Hosea ni mtuhumiwa. Mwanasheria mkuu wa serikali ambaye tunategemea awe mtetezi wa serikali ndio anasimamia kuitafuna nchi. Rais kiongozi wa serikali ambaye tunategemea atoe dira ya taifa naye anazungushwa na wanaomzunguka. Wanachama wenzie wameona mambo hayaendi shwari na sasa wanapanga kumpokea kijiti 2010. yeye mwenyewe alisema hizi ndi mbio za kupokezana kijiti. japo ninawasiwasi kama atakubali kupokewa. Ni wakati wa kutokuwa na shingo ngumu ni wakati wa kusikia sauti ya mungu.
Sasa tusikilize kilio cha wanachi wajenga nchi hii, watanzania waliomaskini wakulima, wao hawana pa kuiba. Kazi yao ni kujenga nchi hii. Mtu aliyekaribu na wananchi hawa, na anyejua hali halisi ya watanzania ni kanisa. Maana matumaini yao sasa wameyaweka kwa mungu. Askofu na mchungaji anaweza kumuwakilisha vizuri mtanzania kuliko mwanasiasa yeyote. Yeye anajua umaskini wa watanzania kwa hata kuangalia mapato ya makanisa yao ya vijijini. Hawa wananetwork mpaka vijijini. Nimekwenda kanisani ambalo ukiangalia waumini ni wengi zaidi hata ya 50. lakini mapato ya sadaka yalipotangazwa nilishtuka kwani ni shilingi 5000 tu. Na mimi wa mjini nilitoa noti si shekere lakini pale mjini ninapoabudu mapato yao ni makubwa sana. Sasa hii niliona ni kali ya mwaka.
Kwa hali hii mchungaji au askofu wa kijijini anapata makali ya maisha pamoja na watanzania maskini wa huko kijijini. Sasa kama ni hivyo na huku akienda mjini na asoma mgazeti anajua jinsi nchi hii inavyotafunwa. Sasa akiamua kubuni njia za kumkomboa mtanzania maskini ni lazima kuanza kupiga vita vyanzo vya umaskini. Kwanaza ni kwa kumuelimisha muumini ili awatambue maadui (mafisadi). Kisha kupambana nao ni kuwanyima kura wasichaguliwe wakaendelea kutafuna nchi. Sasa kama hata mchungaji atafundishwa cha kuubili kanisani huyu mchungaji atakuwa anafanya kazi ya wanadamu wala si ya mungu. Walaka kuandika ni njia ya kufikisha ujumbe kwa wauminin lakini hata wakisoma biblia hairuhusu kuchagua mafisadi. Sasa kama walaka unaleta tabu wanaweza hata kuhubili kwa maneno moja kwa moja kwa waumini ili wasichague mafisadi. Bado ujumbe ukawafikia waumini. kwa kupiga marufuku walaka ambao mimi naamini ndio unawakilisha ujumbe wa watanzania walio wengi ni kujenga uadui mkubwa kati ya viongozi na watawaliwa.
Mimi naamini sauti ya mungu kwa taifa ili ni kukemea maovu yaliyopo katika jamii. Mchungaji yeyote ambaye hata pinga ufisadi hatendi kazi yake vyema. Mchungaji asiewaambia waumini wasichague mafisadi si mchungaji wa mungu. Kwani mbona hata polisi wanaomba wachungaji wawasaidie katika kujenga maadili katika jamii. Yaani waambie waumini waache uizi, unzinzi nk
Sasa kuwambia wasichague mafisadi et ni kugawa taifa? Hakuna walaka unaosema chagua mkistro au muisilamu. Sasa wanaposema baada ya uchaguzi wakristo au waisilamu watasema wetu kashindwa au kashinda kutatoka wapi? Jamani kwa kuwafunga mdomo wachungaji ni kukataa kusikia sauti ya mungu. Ni kukatalia watanzania wasisikie sauti ya mungu. Na kiburi cha kusikia sauti ya mungu,gharama yake muulize petro aliyetumwa ninawi kuubiri injili. Kutowasikiliza watumishi wa mungu ni kutafuta balaa kwa taifa. Waacheni wahubili wahubili kweli na hio kweli itaiweka tanzania huru!!!
 
Back
Top Bottom