Ni vitu gani vinakuvutia mahali unapoishi?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,395
Nimekuwa nikijiuliza, ni vitu gani vinavutia katika maeneo tofauti hapa duniani. Je ni kitu gani chenye kuvutia kukiangalia na labda ukawa unatamani kwenda kukiona mara kwa mara, inaweza ikawa ni katika eneo unaloishi, wilaya, mkoa au hata nchi.

Inaweza ikawa ni lugha inayozungumzwa hapo, milima na mandhari, mito na mabonde, sherehe za kimila zinazofanyika kwa msimu kwa mfano kule Zanzibar wana sherehe za Mwakakogwa, au kitu chochote ambacho uliwahi kukiona mahali fulani kikakuvutia.................

Kwa mfano, niliwahi kumtembelea rafiki yangu kule Lushoto Tanga, niliyapenda sana mandhari ya kule milimani, hali ya baridi, chemchem na vijito vidogo vidogo natamani sana kama vekesheni yangu ya mwezi huu ningeenda kule.................

MLALO 2.JPG MLALO 3.JPG MLALO 4.JPG MLALO.JPG

LUSHOTO.JPG SONGE KILINDI.JPG

Navutiwa na mtaa anakoishi rafiki yangu...mtaa wenyewe siwezi kuutaja hapa, wengi mnaufahamu. Umezungukwa na guest houses kila kona! Basi haiishi wiki bila fumanizi!!
 
Navutiwa na mtaa anakoishi rafiki yangu...mtaa wenyewe siwezi kuutaja hapa, wengi mnaufahamu. Umezungukwa na guest houses kila kona! Basi haiishi wiki bila fumanizi!!

Mzee mwenzangu Rejao, kwa hiyo kinachokuvutia sio Guest Houses, bali fumanizi zinazotokea hapo mara kwa mara......................Au?
 
Mzee mwenzangu Rejao, kwa hiyo kinachokuvutia sio Guest Houses, bali fumanizi zinazotokea hapo mara kwa mara......................Au?
Napenda mazingira ya huo mtaa..movements za watu usiku na mchana, kuwaona watu ambao hutegemei kuwaona katika mazingira hayo, vilio, makelele na miguno yenye kuleta hamasa!!! Kwa kifupi uwepo wa hizo nyumba za wageni ndiko kumesababisha hayo yote
 
Mzee mwenzangu kumbe huwa unapiga Chabo..............!
 
The peace and quite manake I really lov my privacy and haven of peace. Sipendi vurugu na movements kila wakati. Kingine usafi, kuanzia wa mitaa ninayokata kufikia kwangu na kutokuwepo matakataka. Lushoto ni ideal place for vacation, u will reconnect with ur innerself.
 
mi napapenda kwangu aisee..napenda sana kuwa home na familia yangu hata nikiwa mwenyewe..mazingira ya home kwangu yananivutia tu..ndo maana wikiends na ninapowahi kutoka job najitahid nirud zangu home tu nikaenjoy!!
 
Kinanifanya nipende haya maeneo nayoishi
idadi kubwa ya watu
nyumba zenye msongamano
umbea wa mtaa kwa kufuatiliana taarifa za kila mmoja
vibaka walojaa kila mahali wakionesha individual talent
kukosekana kwa maji na barabara
lakini mtaa umejaa upendo full shangwe
 
asante mkuu mtambuzi,
kwanza umeamkaje,
je ulisoma vichwa vya habari vya gazeti la udaku la jf,

mimi ninapoishi navutiwa sana na chumbani kwangu, rangi nyeupe iliyopakwa naipenda sana.
 
Kinanifanya nipende haya maeneo nayoishi
idadi kubwa ya watu
nyumba zenye msongamano
umbea wa mtaa kwa kufuatiliana taarifa za kila mmoja
vibaka walojaa kila mahali wakionesha individual talent
kukosekana kwa maji na barabara
lakini mtaa umejaa upendo full shangwe
duh..sasa vibaka waliojaa na individual talent na umbea wa mtaa ....huo upendo utakuwepo hapo kweli!!??
 
Mie napenda mazingira yenye kijani ya asili, miti na maua ni kivutio kwangu, hivyo huwa napenda Likizo niwepo kijijini kwetu, ambako kuna hali ya hewa nzuri.
 
Mie napenda mazingira yenye kijani ya asili, miti na maua ni kivutio kwangu, hivyo huwa napenda Likizo niwepo kijijini kwetu, ambako kuna hali ya hewa nzuri.
wapi huko..!? isije kuwa maeneo ya makumbusho..na pale si kuna kijiji?
 
Back
Top Bottom