Ni vita, Rage amvaa Mnyika

Mkuu hiyo heading yako inakosa mshiko kidogo,maana kusema ni vita kati ya Rage na Mnyika sidhani kama uwezo wa Rage kiakili unaweza kufananisha na Mnyika....kwa kila kitu,michango bungeni,hotuba na kuwajenga watanzania kifikra,Rage yupo mbali sana huyu msomali....nadhani akashindane na watu wengine na sio Mnyika kwenye hoja....kama tunakubaliana kuwa ni vita,basi ni kama kusema vita kati ya Somalia na NATO halafu utegemee kuwa Somalia watashinda.........

Rejea mchango wangu kuhusiana na heading.
Nadhani ulijipambanua vya kutosha.naomba urejee page zilizopita.
 
Lema hakukaa jela, alikua 'selo' tu, so hajui vema ndugu.
Kama wajua weka hadharan maana naona umeguswa sana

Mkuu, hii ni forum tunachangia wote tu, unataka kuniambia "Selo" ni salama?
 
Hakuna mtu huwa simtilii maanani kama Rage but katika hili la Mh Rais kumteua Lubuva yuko sahihi na tunapaswa kukubali maana katiba/mamlaka iliyomuongoza Jk ni hii hii ambayo haijabadilishwa,sasa aache kuteua? Ni mpaka hapo katiba itakap[obadilishwa na kuelekeza tofauti katika jambo la tume ya uchaguzi na upatikanaji wa viongozi wake

Mmbangifingi,

Alichokisema mbunge wetu ni JOHN MNYIKA: Majina mapya bila mfumo mpya hauwezi kutuhakikisha ufanisi wa tume wala kuwa na chaguzi huru na za haki . Rage alipaswa kuzijibu hoja zake badala ya kuanza kumshambulia binafsi.

serayamajimbo
 
Mkuu hapo sawa. Maada ilivyowasilishwa ni kama Mnyika alipinga uteuzi wa Rais kumbe.alipinga mfumo. Hapo safi kabisa sina tena ubishi Rage alitakiwa kuzungumzia mfumo. Nilikuwa nashangaa yaani Mnyika akurupuke na kupinga uteuzi ambao upo kikatiba badala ya kuikemea katiba.
 
Mkuu, hii ni forum tunachangia wote tu, unataka kuniambia "Selo" ni salama?

nlicho manisha ni kwamba 'selo' si hatari kama jela mkuu.
Afu uki compare rage na Lema, utagundua kua Rage alika ndani mda mrefu so anauzoefu mkubwa,
nadhani umenipata ,ritz.
 
Rage ni msomalia, ni gaidi, fisadi wa FAT=TFF, anatembea na pisto utafikiri yupo kwao somalia hata kwa wapigaji kura wake, na amshukuru kikwete bila yake asingelipata huo ubunge, tusubiri 2015 kama atarudi mjengoni? Mnyika yuko sahihi kabisa na ni mtetezi wa wanyonge!
 
Thank you very much mkuu!
 
Matatizo yaliyopo Tabora mjini na ambayo Rage ameshindwa kuyasimamia ni Mengi,miaka 50 ya uhuru maji Tabora ni issue kubwa' manispaa ya Tabora imezungukwa na barabara mbovu ajabu,aache kumjadili Mnyika ajadili matatizo ya jimbo lake!
Kwani ni kitu gani Mnyika amekifanya kwenye jimbo lake kitakumbukwa?Unataka kutuaminisha kwamba Mnyika anafanya vizuri ndani ya jimbo lake?Je ameshakamilisha ahadi ngapi alizoahidi wakati wa kampeni wacheni bana kutetea na kumuosha mtu kwa manukato yanayonuka!!
 
MBUNGE wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM) amemjia juu Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) akimtaka kuacha kuubeza uteuzi wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni. Badala yake, amemtaka afahamu kuwa, yote yanayofanywa na Rais Kikwete yamo ndani ya mamlaka yake kikatiba.

“Jamani, mwambieni Mnyika aache kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kupinga kila kitu. Hivi Rais amekosea wapi Alichokifanya si kimo ndani ya katiba ya nchi ambayo ilimpa rais kuteua tume iliyosimamia uchaguzi mkuu uliopita na ambao Mnyika alishiriki na kushinda?” alihoji.

Rage, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Tabora, alisema Mnyika na viongozi wengine wa kambi ya upinzani wanatumia nguvu nyingi kubeza mchakato wa kuelekea kupatika kwa katiba mpya, badala ya kuhangaika kutatua kero za wananchi.

Alisema kiongozi wa kweli ni yule anayeguswa na matatizo ya mwananchi, na si anayetumia muda mwingi kupinga kila jambo, hata ambalo mwananchi wa kawaida halimgusi sana.

Chanzo: Jambo leo
Huyu jamaa hewa! Na ndio maana alizomewa kule Tabora,anakurupuka tu na isitoteshe mnyika na watanzania wengine tuna uhuru wa kutoa mawazo kwani raisi ni raisi wa nani na anawatumikia akina nanni,hewa! Sio kila jambo analofanya raisi na wasaidizi wake ni nzuri wao sio malaika
 
Kwani ni kitu gani Mnyika amekifanya kwenye jimbo lake kitakumbukwa?Unataka kutuaminisha kwamba Mnyika anafanya vizuri ndani ya jimbo lake?Je ameshakamilisha ahadi ngapi alizoahidi wakati wa kampeni wacheni bana kutetea na kumuosha mtu kwa manukato yanayonuka!!

Mmm! Heshima mkuu,
Hili nalo neno...
 
MBUNGE wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM) amemjia juu Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) akimtaka kuacha kuubeza uteuzi wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni. Badala yake, amemtaka afahamu kuwa, yote yanayofanywa na Rais Kikwete yamo ndani ya mamlaka yake kikatiba.

“Jamani, mwambieni Mnyika aache kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kupinga kila kitu. Hivi Rais amekosea wapi Alichokifanya si kimo ndani ya katiba ya nchi ambayo ilimpa rais kuteua tume iliyosimamia uchaguzi mkuu uliopita na ambao Mnyika alishiriki na kushinda?” alihoji.

Rage, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Tabora, alisema Mnyika na viongozi wengine wa kambi ya upinzani wanatumia nguvu nyingi kubeza mchakato wa kuelekea kupatika kwa katiba mpya, badala ya kuhangaika kutatua kero za wananchi.

Alisema kiongozi wa kweli ni yule anayeguswa na matatizo ya mwananchi, na si anayetumia muda mwingi kupinga kila jambo, hata ambalo mwananchi wa kawaida halimgusi sana.

Chanzo: Jambo leo
John Mnyika
Nachukua fursa hii kuwatakia heri katika sikukuu ya noeli na heri ya mwaka mpya wenye upendo, furaha na mafanikio. Kwa waumini siku hii ni kumbukumbu ya kwa mkombozi hivyo inapaswa kuleta mabadiliko ya kuzaliwa upya kiroho na kimaisha. Leo (25/12) nimealikwa kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la nyimbo za injili na Xmas Landmark Hotel Ubungo kuanzia saa 8 mchana na kesho (26/12) nitakula chakula cha mchana na waathirika wa maafuriko Mabibo Loyola Jimbo la Ubungo. Naomba wenye zawadi yoyote tujumuike kwenye boxing day kwa ajili ya waathirika wa mafuriko; mnaweza kuja kuzitoa kesho au kama mna ratiba zingine mnaweza kutupatia kabla kupitia kwa Julius Mgaya (0715745874 au 0768503331) wa ofisi ya mbunge. Mwisho wa mwaka ni wakati wa kumshukuru Mungu na kurudisha kwa umma; tujumuike na familia pamoja na waliokumbwa na matatizo mbalimbali katika jamii wakiwemo waathirika wa maafa ya maafuriko yaliyotokea Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi yetu.
Nape kaalikwa wapi?

Back
Top Bottom