Ni vita: Lowassa, Sumaye, Mwandosya - Madai ya matumizi ya fedha chafu yaibuka; Udini na Ukabila

Wote wawili, Lowasa na Sumaye, hawatufai WATANZANIA kwa nafasi hiyo ya URAIS wa JMT. Ziangalieni hotuba za Mwalimu zinazorushwa mara kwa mara na ITV kuelekea maadhimisho ya kifo chake tarehe 14/10 ijayo.
 
Achilia mbali usahihi wa uchambuzi huu, lakini vitu kama hivi adimu vilipaswa kuwa vinatoka kwa watu kama akina Dr. Bana, sijui Adam Bakari etc. Wao wanaishia kuongea ujinga ambao hata mtoto wa darasa la saba anaujua. Ukisikiliza au kuangalia vyombo vya habari vya nje , utasikia leo tunazungmuza na mchambuzi wa siasa za Irak kutoka Center ya Mahusiano ya Nje chuo kikuu cha ....... ndio utasikia mambo kama hayo ya Aweda...............hongera sana mkuuu
 
Hivi ni kwa nini ni rahisi kusema kwamba ndani ya CCM kuna makundi lakini ni ngumu kusema ndani ya CUF au CHADEMA kuna makundi? Inakuwaje kwenye hivi vyama vingine makundi hayo yawe yanapewa majina ya Mapandikizi? Hamadi Rashid, David Kafulila au Zitto Kabwe wakiwa na wafuasi wao ndani ya vyama vyao yanakuwa ni makundi au wafuasi hao pamoja na viongozi wao ni MAPANDIKIZI??
 
Wote wawili, Lowasa na Sumaye, hawatufai WATANZANIA kwa nafasi hiyo ya URAIS wa JMT. Ziangalieni hotuba za Mwalimu zinazorushwa mara kwa mara na ITV kuelekea maadhimisho ya kifo chake tarehe 14/10 ijayo.

Rais ajaye hawezi kutoka KASKAZINI......Vijana UVCCM Bagamoyo (RITZ1)
 
Mkuu Aweda
Tunashukuru kwa taarifa tujuze makundi ya Chadema au huko shwari makundi hakuna?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Achilia mbali usahihi wa uchambuzi huu, lakini vitu kama hivi adimu vilipaswa kuwa vinatoka kwa watu kama akina Dr. Bana, sijui Adam Bakari etc. Wao wanaishia kuongea ujinga ambao hata mtoto wa darasa la saba anaujua. Ukisikiliza au kuangalia vyombo vya habari vya nje , utasikia leo tunazungmuza na mchambuzi wa siasa za Irak kutoka Center ya Mahusiano ya Nje chuo kikuu cha ....... ndio utasikia mambo kama hayo ya Aweda...............hongera sana mkuuu

Wako wanamitandao wako maprofesa na waandishi wa Habari. Akina Dr Bana wote wako kwenye mitandao, hivyo maoni yao yako biased sana.

 
Wasafi CCM ya sasa hawapo. CHADEMA na vyama vingine msipoteze muda kuwafikiria wagombea wa CCM. Endeleeni na mikakati ya kujiimarisha vijijini kisha mtupatie wagombea bora kabisa.
 
Hivi ni kwa nini ni rahisi kusema kwamba ndani ya CCM kuna makundi lakini ni ngumu kusema ndani ya CUF au CHADEMA kuna makundi? Inakuwaje kwenye hivi vyama vingine makundi hayo yawe yanapewa majina ya Mapandikizi? Hamadi Rashid, David Kafulila au Zitto Kabwe wakiwa na wafuasi wao ndani ya vyama vyao yanakuwa ni makundi au wafuasi hao pamoja na viongozi wao ni MAPANDIKIZI??

Ndani ya Chadema naamini hakuna mitandao kama hii ya CCM. Mitandao ni kinyume na kanuni na katiba ya Chadema.
 
Nape anacheza karata zake kati ya JK na Sitta - yuko kote kuwili kwa siri sana. Hilo liko wazi. Kwa JK analinda unga wa watoto. Kwa sitta analinda unga wa 2015 akiamini mtandao wa JK utashindwa na yeye hamwamini JK.
Lowasa akiwa mwenyekiti wa ccm Nape lazima atakufa njaa Lowasa kwa visasi ataanza na Nape kisha katibu mkuu mkama
 
Hivi mkuu Mikael P Aweda inawezekana kweli Mzee Mwinyi akawa hayupo pamoja na Jk? Sounds a bit strange to me. Funguka zaidi basi.
 
Last edited by a moderator:
Ndani ya Chadema naamini hakuna mitandao kama hii ya CCM. Mitandao ni kinyume na kanuni na katiba ya Chadema.

Mkuu unarudia hadithi zilezile za malaya na kahaba kweli kupenda kubaya; hivi unajua tofauti ya matendo yao?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Magazeti mengi toka jana hadi leo bado yanaipa uzito habari za kuanguka kwa Sumaye kwa kiwango kisicho cha kawaida. Kupewa uzito huko kwa habari hizoio una msukumo wa kimakundi ndani ya ccm. Na mimi sijui ni kundi lipi kati ya makundi hasimu.

Leo mwananchi imekuja na habari za Lowasa kudai kwamba Monduli ni msuli wake wa kisiasa. Kauli hiyo ni dongo kwa Sumaye kwamba yeye hana Msuli wa Kisiasa Hanang na Kwamba nitakushinda 2015. Na hapa analengwa Sumaye na kundi lake aka mtandao wake.

Wote wawili Sumaye na Lowasa hakuna aliyetangaza nia ya kugombea Urais lakini inafahamika wote ama wanautaka Urais ama wanasukumwa na wapambe wao au mitandao yao ili wagombee. Wote pia wanatoka katka makundi makubwa mawili hasimu. Kwa mujibu wa magazeti kadhaa ya Leo Sumaye yuko tayari kupambana na waliomwaga fedha Hanang za kumwangusha yeye iwe ndani ya ccm au nje ya ccm ( mgombea binafsi). Taarifa zilizoenea Hanang ni kwamba Nagu alifadhiliwa na ama kundi la Lowasa au JK.

Mpambano huu sasa unazidi kunoga kufuatia habari zinazoendelea kuvuja ktk magazeti ya leo kuwa Sumaye sasa anataka kuunganisha nguvu na kundi la Sitta ktk kujipanga kwao.

Hiyo ina maanisha kwamba makundi makubwa sasa ni hilo la Lowasa lenye fedha nyingi na likiwahusisha pia wahindi wengi wenye shekeli nyingi.

Kundi la pili ni hilo la Sumaye na (sitta?) na wastaafu wengine akiwepo mkapa ( taarifa isiyo rasmi) ambao sasa wanataka kuunganisha nguvu na Samweli Sitta. Membe na Sitta wanaelewana sijui kama anaunganisha nguvu kwa sitta au anataka ajitegemee bado. Mkapa hana ugomvi na Lowasa lakini hana imani kama atashinda.

oKuna la tatu ni la Mkuu wa Nchi, ambalo linataka kutumia keti ya zamu ya wanawake ( Asha Rose Migiro). Hili ndilo kundi linaloungwa Mkono na wakuu wa wilaya, mikoa wengi na wakurugenzi – wote wateule wa JK. Baadhi ya taarifa zinasema JK pia ameahidi kumsapoti Membe huku Membe akiamini kuwa JK anamuunga mkono A. Migiro.

The bottom line is kuna makundi hayo makubwa matatu Sitta/sumaye, Lowasa na Jk + makundi mengine madogo.
Kila kundi linategemea jambo Fulani.
Kundi la Lowasa linategemea sana Pesa – wako vigogo kama Rais mstaafu Karume.
Kundi la Sitta linajinadi kwa maadili – wapinga ufisadi ( Japo maadili yao yanahojika) – Hawana pesa nyingi.
Kundi la Sumaye/sitta ( ambalo linataka kuunganisha nguvu na sitta +sumaye) linategemea majina zaidi. Hapa kuna marais wastaafu akiwepo mkapa, viongozi wa Chama wenye majina makubwa na heshima ndani ya Chama kama akina Mangula. Kuna taarifa pia kuwa Mwandosya na Mwakyembe baada ya uchaguzi huu wa ndani ya Chama wakizidiwa watajiunga na kundi hili.
Kundi kubwa la tatu la JK linategemea mamlaka. Nguvu yao kubwa ni wakuu wa wilaya na mikoa ambao ni wajumbe wa kamati ya siasa wa ngazi zao. Kundi hili pia lina fedha na linauwezo wa kupata fedha kutoka kwa wafanyabiashara wasiotaka matatizo na dola. Hata hivyo, kadri siku zinavyoenda wafanyabiashara wakisoma upepo watawagomea.
Kundi hilo ndilo linatumia vizuri mamlaka yake ndani ya Chama na Serikali na kushinikiza mabadiliko ya katiba ili kushinda. Hapa JK alilenga yafuatayo.
a) Kubadilisha katiba ili kubadili muunda wa kupata wajumbe NEC. Lengo ni kuondoa hawa waliopo ambao wengi ni kundi la Lowasa – Hapa anadhibitiwa ni Lowasa zaidi.
b) Wameweka marekebisho ya kuondoa marais wastaafu ndani ya Kamati kuu kwa sababu marais wastaafu wote ( karume, Mkapa na Mwinyi) hawako katka kundi la JK.
Hitimisho.
Kwa kuwa uhasama kati ya makundi haya umefika kiwango cha juu cha kutoa kauli ya kupambana ndani na nje ya chama.(Kauli hii wakati Nyerere inatosha kumwajibisha mhusika) Na,
Kwa kuwa m/kiti wa ccm ameshindwa kabisa kuongoza Chama na kuwa sauti ya Chama kama ilivyokuwa wakati wa Nyerere. Na,
Kwa kuwa, kiwango cha kukataliwa kwa ccm kimezidi kupanda kila kukicha. Na
Kwa kuwa baadhi ya makundi yako tayari chama cha upinzani (chadema) kichukue dola kuliko kundi pinzani ndani ya Chama, Na,
Kwa kuwa, baadhi ya makundi yanafanya mazungumzo yasiyo rasmi na baadhi ya vyama vya siasa ili kuhamia huko mambo yakiwazidia Na,
Kwa kuwa kundi la Lowasa ndilo lenye nafasi kubwa kushida kwa kutegemea nguvu ya fedha huku ikiwa halikubaliki kabisa kwa umma wa watz ambao hawataweza kuwahonga (Pasco wa JF upo?).
Hivyo basi,
Naomba kuhitimisha kwamba;
kama Chadema itamaliza uchaguzi wake wa ndani vizuri mwaka kesho, na
Na kama Chadema watakuwa tayari kumuunga mkono mgombea wao mmoja bila kuvurugana wenyewe ktk kura ya maoni ya ndani mwaka 2015,
Njia ya Chadema kushinda 2015 iwepo katiba mpya au ya zamani ni nyeupe mno. Hii ni kwa sababu, hata kama hakutakuwa na kundi litakalohamia chadema kati ya makundi hasimu (Naamini wako watakaokimbia) hakuna siri itafichika ambalo haitajulikana na Chadema ikiwepo mipango ya kuchakachua kura – hakuna ushindi bila uwezo wa kutunza siri.
NB; Nadhani nimepunguza sana ushabiki wa kisiasa na kuweka ukweli mtupu.


Ushauri wa bure apumzike siasa ale pensheni Yale maisha ni zaidi ya siasa.
 
Mkuu mikael.P.Awenda,
2015 kwa vyovyote vile magamba wanakuwa wapinzani, kitakachowatoa ni namna wanavyozidi kushindwa kumkomboa mtanzania dhidi ya maadui sugu watatu, kila kukicha umasikini na ugumu wa maisha unazudi kuongezeka, kushindwa kwao kwa 50 years ndio makundi yao na ndio kushindwa kwao wasimtafute mchawi, hali ni mbaya watanzania wamechoka wanataka matumaini mapya! CHADEMA waandae safu ya kuongoza nchi 2015,
 
Back
Top Bottom