Mimi mpaka sasa sija amini kama kweli wabunge wote wameona hii ni sawa!!!Yaani hakuna namna nyingine kuzuia uchakachuaji zaidi ya kupandisha bei ya nishati hiyo muhimu kwa watu wa chini???Kweli?Yaani wenzetu toa ushuru kwenye mafuta ya taa sisi tunaongeza eti kuondoa uchakachuaji!!Kweli serikali yetu iko out of touch na maisha yetu halisi, wanajua wote tunapikia gesi na na tuna majenereta!Inauma sana!Nimesoma kwa masikitiko makubwa mojawapo ya magazeti ya leo kuwa kodi ya mafuta ya taa itapanda toka toka sh 52 hadi kufikia sh 400 kwa lita hivyo wamachi watarajie kununua lita moja kwa wastani wa shilingi 1900 sawa na bei ya petroli,sababu hasa ya kupandishwa ni kuzuia uchakachuaji wa diesel unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara!my take: kweli uyu mtu wa ewura hapo ndio mwisho wake wa kufikiria namna ya kuwabana watu hao... Amejaribu hata kuwaza ni watanzania wangapi wanatumia mafuta hayo pengine kuliko hata watumiaji wa dieasel yenyewe? HIVI kweli ni akili hii...........nakuuliza wewe mtu wa ewura na hali hii ya uchumi kuwa ngumu,hatuna umeme tunategemea mafuta hayo umetafakari vyema kweli?hivi tunaelekea wapi jamani...tutaendelea kulia hivi hadi lini,....lini tutaingia barabarani....naona bado freedom ipo mbali sana!!nimeandika kwa uchungu nikiwaza wazazi wangu kule kijijin wanotegemea mafuta hayo kwa taa na kajiko ka mchina ....omg
KWA KWELI NIMELIPOKEA HILI KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA KWA SABABU WANASEMA ETI WAMEPANDISHA KODI ILI KUDHIBITI UCHAKACHUAJI WA MAFUTA SASA HII SERIKALI HAIONI NIKUMKANDAMIZA MTANZANIA WA KIPATO CHA CHINI?KWA HIYO EWURA WAMESHINDA KUWADHIBITI WACHAKACHUAJI WA MAFAUTA?SASA KUNA UMUHIMU GANI WA KUWA NA EWURA NA TBS?MIMI NADHANI MTU AKICHAKACHUA MAFUTA HUYU NI MUHUJUMU UCHUMI ANATAKIWA KUFUNGWA JELA MIAKA 30 NA KUFILISIWA.jE KWA HILI LIKITENDEKA KUNA MTU ATACHAKACHUA AU WACHAKACHUAJI NI WATU WA SYSTEM NDIO MANA WANAOGOPWA NA WANALINDWA ILI KUMTESA MTANZANIA WA KIPATO CHA CHINI?UKIENDA KIJIJINI NISHATI INAYOTUMIKA KAMA TAA NI MAFUTA YA TAA HATA HAPA MJINI WATU WALIO WENGI WANAPIKIA MAFUTA YA TAA.SAS JE MITI ITATUNZWA KWELI?WAKATI BEI YA GESI IPO JUU,.
Mkuu, unaongelea wabunge hawa wa ccm! Wao kila jambo linalokuja toka serikalini wanaliunga mkono kwa asilimia 100, wanaogopa wakihoji watavuliwa gamba.Mimi mpaka sasa sija amini kama kweli wabunge wote wameona hii ni sawa!!!Yaani hakuna namna nyingine kuzuia uchakachuaji zaidi ya kupandisha bei ya nishati hiyo muhimu kwa watu wa chini???Kweli?Yaani wenzetu toa ushuru kwenye mafuta ya taa sisi tunaongeza eti kuondoa uchakachuaji!!Kweli serikali yetu iko out of touch na maisha yetu halisi, wanajua wote tunapikia gesi na na tuna majenereta!Inauma sana!
Kwa wenye ufahamu vizuri naomba mnisaidie ktk hili swala nililosikia kuwa serikali ilipandisha bei/kodi ya mafuta ya taa ili kuzuia uchakachuaji?
Hainiingii akilini kuwa kupandisha bei ya mafuta taa on expense ya watumiaji ili kuzuia makosa yanayofanywa na wengine...naomba mnifahamishe kwa uzuri sijalifahamu jambo hili linawezekana vipi? Pla JF
Imenikumbusha siku moja, nilimwona baba mmoja akiwa amebeba mtoto kumsaidia mkwewe wakiwa wametoka hosiptali wanakatiza mitaa ya Upanga kwa miguu. Ghafla akatokea mbwa anawabwekea akimfuata yule baba. Baba wa watu akahamaki kuwa mbwa atamdhuru. Baba akamtupia mbwa Kitoto huku akisema 'wachaaa'.Hawa watu tuliowaweka huko mbele watuongoze wame'behave' kama huyu baba. Wananusuru mashangingi yao kwa kuwatosa walala hoi. Maskini Watanzani!Kupanda kwa bei ya mafuta kulikotangazwa na serikali ili kuendana na na mafuta mengine kwa kisingizio cha kuwabana wachakachuaji,inaelekea kumuumiza zaidi mwananchi hasa wa kipato cha chini,ambaye lita moja huitumiakwa siku maka mbili tu na kwa bei ya sasa Tshs 2000+,itambidi angalau kwa mwezi awe na 15,000/ kwa ajili ya nishati hiyo.Je wanasiasa na watunga sera tutafika kweli?Maisha yanazidi kuwa magumu jamani.