Ni utani tu...!

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Katika pitapita zangu mitaani mji wa ZnZ, siku moja nilipata bahati ya kuwasikia ndugu zangu wa kule Pemba.

Walikuwa wakijadiliana kuhusu kipindi kilichokuwa kimerushwa na runinga, kipindi kilikuwa kinahusu haki za wanyama. Mazungumzo yao yalikuwa hivi...

M: “Makame wajuwa weyeee... hawa jamaa sasa wan-zidi. Kama kweli wateteya haki za wanyama mbona wanyama wanao wataja ni mapaka na majibwa tu. Sija ona hata mmoja akinteteya kombamwiko na mbu na mapanya. Ikizidi wao ndiyo mwanzo kuwauwa.”

S: “Ehe lakini wajuwa weye... hawa akina kupe na mbu na mende huleta maradhi ati.”

M: “Aaah tafadhali bwana... Hata hawa akina mbwa na paka huleta magonjwa piya. Hebu lete paka hapa nyumbani halafu mwangaliye Nkeo kama atakuwa n’zima. Ataanza kuchechemuwa utasema ampewa ugoro wa kichonyi.”

W: “Vipi tena mbona mwantiya kundini tenaaa?” (sauti ya kike toka uwani)

M: “Aah kwani urongo shemegi. Weye si una waleg'jii... (allergy) nasikia. Waweza kuturuhusu tulete paka na mapanya hapa?”

W: “Siwezi zuwiya ntu miee, lakini Shekhe weye si ulikuwa mazungun'zo yako ni juu ya makombamwiko na kupe na mbu. Unlenga nini yaani wataka kuanza utetezi wao?

M: “Nami shemegi naona nianzishe chama cha kutetea makombamwiko na kupe… alafu nione ntu akiuwa mende kama sijanpeleka kwa sheha...

W: Lakini shemegi weye si kafuu... na kafuu kazi yao si kutetea makomba mwiko na mapanya atiii!, au kafuu inkushinda tena?

M: Shemegi sasa huko usende kama wataka mengie basi nchokozee kafu yangu....!

Nikaona hapa sasa yatakuwa mengine nikajisogeza zangu taratibu kuelekea nilikofikia...

Wakati narudi toka shamba njiani nikakuta Roli la la abiria, limepinduka na bwana mmoja wa kutoka mashamba akawa anatoa ushahidi kwa askari wa barabarani. Jinsi ya mazungumzo yake tu, nikajuwa kuwa ni mara yake ya kwanza kupanda gari maana jinsi anavyo eleza nilibidi nijizuiye nisipasuke kwa kucheka. Mazungumzo yake yalikuwa kama ifuatavyo:

”kwanza wakati safari yaanza tu nkajua kuwa huyu ntu si dereva! kuna lijiti akikazana kuling’oaaa”(wakati dereva anabadirisha gia),

”halafu akawa hatulii mikono ikintetema (akizungusha usukano (?!!) duh! usukano.... si ndo Steering wheel au sio?) kama apandisha kibuki vile (mashetani)”.

”Njiani ikawa ni mbio tuuu...! Twafukuzana na miti....

Miti yenda na sie twenda...

Nliposikia puuu! nkajua tayari ivooo!

Miti ishatugonga au sie tushaigonga miti...
 
XP Umezibuka,

Hao Wapemba kama vile nawaona enzi za TVZ vile.Kuna lahaja huko utafikiri Ngazija, mara nyingine unaweza kuhitaji mkalimani.
 
x paster kunlegeka.

heee heeee

mwenzetu kuntumwa au kuntumiliwa?
hasa ww mwanangwa wa nani?
 
Nimecheka hadi sina mbavu..yani mi hu2wa nikiwasikiliza wakiongea najizuia sana kuangua kicheko kwa lafudhi yao hii
 
Hii imetulia sana:
Nyingine hii hapa..... "Sie nyumbani leo kunansiba, tumefiliwa na ntu nkubwa"
Tehe tehe tehe tehe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom