Ni urahisi wa Tigo kwa gharama??

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,047
452
Jamani hodi nabisha,jamvini kukaribishwa,
changu ni kima cha insha,japo kuja kupaishwa,
nilipata badilisha,tigo ilipoanzishwa,
Ni urahisi gharama,tigo inapotumiwa?

mwanzoni ilitikisa,neno tigo kimaana,
mkichwa ilinitesa,tigo yake maana,
wengi jama huwatesa,wakijaribu ka suna,
ni urahisi gharama,tigo inapotumiwa,

tigo inapotumiwa,ujumbe wake hufika,
jamani niliambiwa,nata hutojanasuka,
tofauti yake huwa,voda ni gharama fika,
ni urahisi gharama,tigo inapotumika,

wengi wao wana mbili,tigo voda hutumia,
hawa eti wanajali,kidai soko huria,
wewe ulie ngangali,kote wataka pigia,
ni rahisi gharama,tigo inapotumika?

tamatini ntaishia,upasuaji ukinijia,
zantel voda tumia,sawa kunako nokia,
mambo kuyaingilia,tigo kwa mtanzania?
tigo inapotumiwa,watumiaji hujisikiaje?
 
Nimelisifu shairi lako, ila sijajua unamaanisha tigo kama kampuni ya simu au tigo kama mambo mengine ya jbau ambayo vijana wanayabariki siku hizi? maana kila kitu kwa kiswahili kinatafsirika lugha ya ngono tu!
 
Sadly...its the other meaning
 
Jamani,tufike mahali tuwe wastaarabu.Mbona maudhui ya shairi yako wazi?Tunahitaji kutiana moyo kwa ubunifu,siyo kukatishana tamaa.Hongera Magulumangu.
 
Jamani,tufike mahali tuwe wastaarabu.Mbona maudhui ya shairi yako wazi?Tunahitaji kutiana moyo kwa ubunifu,siyo kukatishana tamaa.Hongera Magulumangu.

Sanaa ya ushairi inahitaji tafsiri na huwa ni nyingi kwa uhuru wa shabiki....
 
Back
Top Bottom