Ni uongo gani mkubwa uliowahi kuambiwa utotoni?

"Kwa wale Wakatoliki" ukienda kushiriki mkate wa Bwana kama una dhambi (huja ungama) utawaka Moto mbele ya Altare.

Baada ya kuvunja ungo mtoto wa kike, usikae au kumshika mwananume yoyote utapata mimba.

Wengi tumefuga manyoya ya Tausi katikati ya daftari na kuyalisha mabaki ya kuchonga Penseli, tukiamini yatazaliana.
 
Niliambiwa usikubali mwanaume akufunue utachapwa kiboko na Mungu, nikawa makini kweli hata tukicheza kombolela nikawa nacheza kwa wasiwasi kweli ,, ila ilinisaidia kweli maana nimekuja kufunuliwa na mwanaume nikiwa chuo, thanks mama vitisho vyako vimenisaidia sana huenda nisingemaliza shule ,
Mababu zetu, Wazee wetu wana busara sana, uongo wao ni kwa ajili ya maadili mema.

Tofauti na sasa, utandawazi unaharibu kila kitu.

Mtu kashika ujauzito, anajifotoa mapicha na kuyatundika INSTA, tumbo likiwa wazi, na mtu huyo huyo ana Watoto wadogo pengine umri wa miaka mitano, sasa hapo Mtoto kila kitu anaona kawaida.

Ndio maana sasa hivi Mapenzi wanawahi mapema sana, na wanajua kila kitu, huwezi kuwadanganya Mtoto ananunuliwa
 
Niliambiwa usikubali mwanaume akufunue utachapwa kiboko na Mungu, nikawa makini kweli hata tukicheza kombolela nikawa nacheza kwa wasiwasi kweli ,, ila ilinisaidia kweli maana nimekuja kufunuliwa na mwanaume nikiwa chuo, thanks mama vitisho vyako vimenisaidia sana huenda nisingemaliza shule ,
Siungesubir mpaka uolewe ndo ufunuliwe
 
Baba yangu alikuwa Kiboko.... Ukiwa na Muhindi wako mnakula anakuambia umpe akutengenezee Njia ya Kwenda Kijijini maana tulikuwa hatupajui basi unaahikisha anatengeneza Njia muhindi Mzima.. :D:D:D
Hata sasa hivi watu wanatumia hiyo njia ili kuomba Muhindi.

Utasikia, "hebu ngoja nikuoneshe njia ya Kawe"
 
Mimi nakumbuka nlikuwa na rafiki yangu msomali nkamuuliza nywele zako huwa unafanyann mpaka zinakuwa nzur hivyo?....jamaa akanijibu huwa na sugua na kijiwe kwa maji ya moto ...basi nilikuwa nikiingia kuoga sipoozi maji nasugua nywele kwelikweli lakin wap....nikikumbuka huwa nacheka sana..
 
Alikuweza
 
Baba alikuwa anapenda kunywa kahawa usiku...sasa nilivokuwa naitamani akaniambia nikinywa kahawa usiku nitakuwa nachechemea!
 
enzi za utoto dada wa rafiki yangu alituambiaga alikuwepo enz za yesu, mpka siku anapaa kwenda mbinguni alikuwa nae akawa anamng'ang'ania waende wote :D:D

Na tukamuamini kabisaa
 
"Kwa wale Wakatoliki" ukienda kushiriki mkate wa Bwana kama una dhambi (huja ungama) utawaka Moto mbele ya Altare.

Baada ya kuvunja ungo mtoto wa kike, usikae au kumshika mwananume yoyote utapata mimba.

Wengi tumefuga manyoya ya Tausi katikati ya daftari na kuyalisha mabaki ya kuchonga Penseli, tukiamini yatazaliana.
umenikumbusha sie tulikua na rafiki zetu wakatoliki, wakatuambia ukienda kuchukua ule mkate mkononi na wewe sio mkatoliki hapo hapo linageuka bwawa la maji linakuzunguka.
 
tuliamini albino hawafi ila wanakua wafupi mpaka wanapotea... kwahyo tulikua tukiwaona tunafunua nguo kifuani tunatemea mate ili usipate mtoto albino..!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom