Ni unafiki kumsifia JK hata anapoharibu - Shyrose amwambia Chiligati

dawa yake huyu n kumvizia asimalize ma wake .......mimi nawambia huyu jk atatumaliza anafaa kutapikwa mara moja mtu gani vugu vugu?!!
 
Hizi sasa ni dalili za mtandao wa Lowasa kutapatapa.

Kwanza Shyrose Banji ange declare interest kwamba yupo mtandao wa kumuweka Lowasa IKULU 2015. Then angeongea hiki alichoongea
watu wangejadili wakiwa na picha kamili. Lakini hii janja ya kuhadaa watanzania na kujifanya ana uchungu wa nchi, wakati ana self centered
interests zinazomdrive ni kutufanya watanzania wote mazuzu...ndio MAZUZU!

Sasa ameona NEC inakaribia, kuvuliwa gamba(kama kupo) kumesogea, anatapatapa. Nahisi ana taarifa za ndani zinazomfanya atapetape,
hii sio bure. Miezi 10 iliyopita wakati wa kampeni, hivi mlikua mnatizama post zake huko facebook?... Na nini kilimfanya asiamini yote hayo
anayolalamikia sasa yalipokua yanasemwa na Dr Slaa? Sababu kuu, ni sera ya KUJIVUA GAMBA ilikua haijaasisiwa, na si kero za wananchi kama anavyotaka tuamini.

CCM kwa sasa hakina much choice, wakijivua gamba atleast watafufua matumaini hafifu yaliyobaki, maana hivi sasa wenye nguvu ya pesa (za kudhulumu watanzania) ni kama wamekiteka chama kabisa kuanzia kamati kuu mpaka ngazi ya shina. Wakiamua kutojivua gamba
kwa maana ya kuja kuwahadaa watanzania na maigizo yao, ndio itakua CCM kimesign its own death certificate...2015 wajiandae kukaa kushoto kwa spika.
 
Ni vizuri kama hata makada wa magamba wameona hilo!! Ingawa si habari ngeni kwetu wengi tu humu ndani kwani ndo haya tuliyokuwa tuna-mpinga JK oct 2010.

The good thing amethubutu kusema...
 
Big up kaka sugu kwa kumbadilisha mtazamo huyu dada keep it up kuna wana ccm ukiwaambia hali ya nchi ni mbaya wanataka kupigana kwa kukuita mnafiki kiko waaapiii na 2015 mali zote za riz 1 halali yetu!!
 
Mkapa katili lakini zimetimu. Jeuri lakini alipambana na giza sio kama huyu mpenda uvulana tu
 
Mwisho wa siku tutakao nasa ni sisi, siamini kama hizo kauri ni kwa ajili ya kugombea Ubunge na kupata nafasi za haraka haraka CDM, bali ni kwa ajili ya kujirekebisha pale tulipokosea kama taifa hivyo sitegemea hizo kauri kuja kutumika kama kigezo sahihi cha kusema kuwa sasa huyu ni Kamanda tosha apewe mteremko akale keki yetu Bungeni ama kupitia CCM na hasa kupitia CDM!.
 
Mwana dada Shyrose Bhanji amemtolea uvivu Mzee Johni Chiligati alipo post kwenye ukurasa wake wa faacebook kauli mbiu yao ya

"TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE!"

Mwana Dada Shyrose akamwandikia mzee Chiligati maneno haya



SHYrose.jpg

Hayo ni maneno makali sana kutoka kwa mwanadada Shyrose, ana muona wa mbali sana tofauti na wana CCM wengine ambao hawataki kukubaliana na ukweli kwamba CCM inaelekea kufa.

View attachment 35750
Ninamawazo
 
Shyrose isije ikawa ni visa baada ya kuambulia patupu CCM ,ila kama yanatoka moyoni hongera and keep it up!
Hizi ni dalili za kukiasi chama tawala, CCM. Kutoa malalamiko mbele ya umma tena makali kama haya kwa mwanachama aliyewahi kuomba nafasi ya juu, sipati jibu kabisa. Mhe. Chiligati ana email, saduku la barua na anaofisi. Kwa nini asimfuate huyu mwanadada akaongee naye au asubiri vikao vya chama? Bila shaka anatumiwa kama wanaJF walivyodokea kipindi kilichopita. Hapo ndipo naona kuwa wanawake wakitumiwa, wanakurupuka tu bila kuona madhara yake. Sifikiri kama Tanzania inahitaji raisi Mwanamke kwa sasa kwani huu ndo udhaifu wao mkuu walio wengi. Hama chama ndo ukayaongee hayo hadharani.
 
Ni unafiki zaidi kulalamikia utendaji wa kiongozi wa chama ambacho kinanyanyasa wanyonge na we umo ndani yake. Palipo na nuru hapana giza. CCM wote ni giza tu ndo maana huyu mdada ataishia kupiga kelele gizani na wala hatamnyima usingizi huyu kilaza anayemlalamikia.
 
Jaman huyo shy asijekuonekana msaliti...by the way niliwah kusikia hyo dada anamahusiano na SUGU may b amesha ambukizwa uana harakati.
 
Wakuu zangu,
Msiwe wepesi sana wa kutoa sifa ili hali adui wa maendeleo yetu sio JK bali ni chama cha CCM...Kwa nini hamtaki kuamini kwamba CCM ndicho chama responsible kuleta maendeleo nchini na sii JK, Mkapa au Lowassa!
ShyRose mdogo wangu kama kweli wewe msafi huwezi kuwatetea Magamba na kuona wito wa rais kujivua magamba ni kukivuruga chama..Hupendi maamuzi ya JK kuwavua magamba kina Rostam, Lowassa na Chenge jambo ambalo linaonyesha wazi huelewi sababu hasa ya wananchi kukosa imani na chama chako...Hapa unatafuta mchawi tu kama hulka ya Watanzania wengine.
Makundi ndani ya chama lazima yawepo kwa sababu mna kauli mbiu inayopingana na utekelezaji wa chama..Ni bora muendelee na kauli mbiu zenu kuliko kuendelea kutekeleza sera za Chukua Chako Mapema (CCM)..
 
Hadi ifike 2015 watamkoma rostam. Si walimvua gamba? Yeye atawavua ngozi. Subirini tu
 
Huyo dada kukosa Viti Maalum bado ana kinyongo. Kama amechoka na Magamba ahamie Magwanda haraka. Na kutoa maoni facebook haisaidii, je ni waTZ wangapi wana access internet? Kama ana uchungu aende Jangwani au mwembeyanga akanene hayo.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom