Ni unafiki kumsifia JK hata anapoharibu - Shyrose amwambia Chiligati

gwambali

JF-Expert Member
May 10, 2011
230
76
Mwana dada Shyrose Bhanji amemtolea uvivu Mzee Johni Chiligati alipo post kwenye ukurasa wake wa faacebook kauli mbiu yao ya

"TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE!"

Mwana Dada Shyrose akamwandikia mzee Chiligati maneno haya

@Mhe. John Chiligati. kauli mbiu kama hizi ndizo zinazoturudisha nyuma. Tazizo moja kwenye Serikali ya CCM tunaongoza kwa kauli mbiu lakini utekelezaji ndiyo kasheshe...huu siyo tena wakati wa mbwembwe za kauli mbiu, ila kikubwa kinachotakiwa ni utekelezaji. Mimi naomba nikwambie ukweli kuhusu mtazamo wa watanzania leo juu ya chama chetu CCM...

Wananchi wengi sana wameanza kukosa imani na CCM kutokana na fitna, majungu, unafiki wa kumsifia Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete hata pale anapoharibu. Ni ukweli usiopingika kwamba leo hii CCM iko katika hali mbaya kimtazamo mbele ya macho ya jamii. Je unalifahamu hili Mhe Chilligati? Je unafahamu kwamba wananchi wameanza kuichoka CCM? Je unafahamu kwamba Rais JK ndiyo kiongozi anayechangia kwa kiasi kikubwa sana kukigawa hichi chama chetu

hivi mnamwambia ukweli wa mambo au mnampotosha kwa kutomwambia ukweli? Nitashukuru sana ukimfikishia ujumbe wangu JK kwamba style yake ya uongozi ndani ya chama chetu na akiwa kama mkuu wa nchi inalalamikiwa sana huku mitaani, hata na mwananchi wa kawaida...kila mtu anauliza JK yuko wapi? mbona yuko kimya sana? Mwambie wananchi wanataka kuskia kauli yake nchi inapoelekea kwani kila kikicha kuna matatizo lukuki...kwa leo ni hayo tu Mhe. Chilligati...naomba kuwasilisha!

SHYrose.jpg

Hayo ni maneno makali sana kutoka kwa mwanadada Shyrose, ana muona wa mbali sana tofauti na wana CCM wengine ambao hawataki kukubaliana na ukweli kwamba CCM inaelekea kufa.

Attachments

• SHYrose.JPG
SHYrose.JPG
62.3 KB · Views: 130
Haya mambo yameanza kuzungumzwa na watu toka siku nyingi sana wewe ulikuwa wapi?

Napata wakati mgumu kukuamini kwani tulipokuwa hasa tukiangaika usiku na mchana mwaka jana kujaribu kumuangusha kwenye uchaguzi wewe hukuwepo that was a critical moment for anybody with love for this country to stand up and be counted.

Ulikuwa unashambulia kutokea upande wa pili leo ghafla umeamka kutoka usingizini umegundua kuwa JK hafai lakini JK huyu ndiye yule yule uliyekuwa ukimshangilia mwaka jana hajabadilika nina wasiwasi na usingizi huu wa ghafla ulioamka nao inawezekana unalo lako jambo inawezekana kuna watu wanakutumia au wana mpango wa kukutumia baadaye.

kwa nchi yetu inabidi jasiri sana kuongea haya, refer Ulimwengu, Muro, Kolimba, Katabaro n.k
Lakini bila watu jasiri hatutaenda mbele, thanks Shyrose, nitakugongea "like" facebook.

sawa kanena je hatua za kujirekebisha zitafuatwa au ni mbwembwe tu za kujitafutia like fb na kwenye mitandao ya kijamii, alipaswa kumuambia mbele yake na vile vile ampe ukweli vasco da gama kuwa anaboa nasio kuishia kwenye mtandao ambao anaweza kujifanya hajaona..

angalizo..
hapa utasikia shyrose anaambiwa anakisaliti chama na anajipendekeza kwa wapinzani subirini muone kinacho fuata. na pia asisahau kumwambia na kaka nape naye kuhusu lalamiko hilo..

Mhhh!!ShyRose..ShyRose...ShyRose!!!!in the current CCM,the one which neither belongs to the workers nor to the peasants,the one which was denied by its founder Mwalimu JK,to hold a such big stand of correcting your Chairman and the CC,to me you are no longer validy to remain the member to the party,none of your leaders wishes to be corrected not only in public manner but even at his home except for the man who is now lying burried at Butiama

You indeed have good ideas however the party politics wouldn't like to allow it out of your mouth,watch it my sister!!Korimba,A.Chifupa,Dr.A.Juma and the like were once living but today have gone,be ready,get on your knees,stand firm....with God's mercy

oh gal, im proud of ur daring attitude. hebu anza mazungumzo ya chinichini kuhamia chadema. unajua ni aibu kwa kijana kuwa frontier wa ccm! u ar nt a brownnoser, u made my day! i will drink to that aisee!

sawa kanena je hatua za kujirekebisha zitafuatwa au ni mbwembwe tu za kujitafutia like fb na kwenye mitandao ya kijamii, alipaswa kumuambia mbele yake na vile vile ampe ukweli vasco da gama kuwa anaboa nasio kuishia kwenye mtandao ambao anaweza kujifanya hajaona..

angalizo..

hapa utasikia shyrose anaambiwa anakisaliti chama na anajipendekeza kwa wapinzani subirini muone kinacho fuata. na pia asisahau kumwambia na kaka nape naye kuhusu lalamiko hilo..

Mkuu una demand too much from her. At least yeye amekuwa na ujasiri wa kukosoa directly tena kwa kutumia jina lake moja kwa moja pasipo kificho.

Hivi huyo Shyrose bhanji, kaishalifanyia nini taifa letu au ana msaada gani! naona kila siku Pro-CDM-JF, mnaangaika nae.
Mnatoa umbea kule FB mnaleta JF, Magwanda bana au kwa sababu shemeji yenu demu wa Sugu

Shyrose amejitahidi kuwa mkweli kwa uongozi wa chama chake as well as serekali ya chama chake,kitu ambacho ni wanamagamba wachache wenye uthubutu huo,anastahili kuungwa mkono hadi hapo alipofikia.
Kwakuwa viongozi wake hawatafutrahishwa na mtazamo wake huenda akafanyiwa zengwe na kuvuliwa gamba,ingawa kwa silka ya mwenyekiti wake anaweza asimchukulie hatua kwakuwa ndo udhaifu wenyewe unaozungumzwa.
Mwisho namshauri shyrose, it's high time afanye maamuzi sahihi na makini kwa kujiunga na wapiganaji wa kweli CHADEMA ili kwa pamoja agenda yake iweze kupata uungwaji mkono.

Shyrose hongera kwa kunena japo too late. Yafaa ujue umenena wakati chama chako kina fall from a cliff in slow motion, it cant reverse, only time will tell lini kitafika chini. Unafiki wa wana CCM umeifikisha hapo,hawakusoma alama za nyakati, na zlikua wazi kwa kila mwenye kutaka kuziona. Bye bye chama chetu.

unauliza ameifanyia nini nchi hii? kuthubutu kumwambia mbayuwayu ukweli huo tayari amethubutu, ni ccm wangapi wamethubutu kumwambia vasco da gama ukweli huo? wengi wanajipendekeza na hawamwambii hali ilivyo huku site, keneth kaunda alipitia hali kama hii kwani waliomzumguuka walimpa maneno aliyokuwa anapenda kuyasikia kuwa watu bado wanakikubali chama cha UNIP kumbe hali site haikuwa hivyo kwa kuwa hawakutaka kumuudhi mzee, sa nyie endeleeni kumdanganya jk mtapata majibu 2015, kama kaunda alivyopata majib
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-anapoharibu-shyrose-amwambia-chiligati.html

Mwana dada Shyrose Bhanji amemtolea uvivu Mzee Johni Chiligati alipo post kwenye ukurasa wake wa faacebook kauli mbiu yao ya

"TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE!"

Mwana Dada Shyrose akamwandikia mzee Chiligati maneno haya

Hayo ni maneno makali sana kutoka kwa mwanadada Shyrose, ana muona wa mbali sana tofauti na wana CCM wengine ambao hawataki kukubaliana na ukweli kwamba CCM inaelekea kufa.

Wana Jf alichokisema Shyrose si jambo la Kubeza,mimi Binafsi Ni Mwana CCM JK anaendasha Nchi kwa Matukio Toka ameingia madarakani nchi yetu imekua ikiendeshwa si kwa kuangalia matatizo yanayokabili Taifa wananchi wake Jamaa huyu ametumia style ya Kutufanya busy tukijadili na Kulumbana juu ya mambo yasiyokuwa na TIJA.

Toka mwaka 2008 nitaorodhesha chini hapa Matukio ambayo kama Taifa tumetumia muda mwingi huku yeye akienda kutembea ulaya na kutupatia ahadi na kauli mbiu ambazo hazitusaidii.

2005 aliingia na MOVIE inaitwa Maisha Bora kwa Kila Mtanzania na Kuleta mabilioni ya JK.No impact to the economy and Common Wananchi.

2007/2008.Akaleta sinema inaitwa Kupambana na Rushwa na Matumizi Mabaya ya Madaraka Tukasikia EPA ambayo ilimuingiza yeye madarakani,Tukasikia kina Mramba,Kina Mgonja,Kina LIUMBA wakifunguliwa kesi mpaka leo zinaendelea na liumba yupo jela.

Tukaletewa Movie ingine RICHMOND na ili aendelee kupatta Umaarufu akamtosa waziri Mkuu wake akidai hajui RICHMOND wakati ilikuwa CABINET decission.

Tumeimba Richmond,Lowasa weeeeeeee yeye anaendelea kupeta wananchi tukasahau kuhoji mambo ya msingi ya nchi yetu tukawa Bar,Majumbani,ktk Madaldala,Mashuleni,Hospitalini,Na kila sehemu mjadala ni huo huo.

Akatutengenezea Sinema Inaitwa TINDI KALI la KUBENEA katumia Idara yake ya Usalama wakachukua Tindikali wakchakachua kamwagiwa Kubenea Nchi nzima tukahamia hiyo sinema kesi akamuuzia Lowasa tukawa busy na hilo hamna kujadili maendeleo.

2010 ukawa mwaka wa uchaguzi hapo kavuka Term ya kwanza salama kwa kutugawa kama Taifa na ndani ya Chama chake akawagawa wananchama wake wakawa Makundi yakipambana yeye anakula kuku Ikulu leo Serengeti kesho marekani.

2011,Zikaanza movie zingine BABU WA KIKOMBE loliondo,tukawa busy na babu nchi nzima hatuhoji maendeleo.

Mara Movie Ingine GAMBA limetuchukua muda Muda Mrefu tukaletewa Stering anaitwa Nape hapa nchi nzima ikawa Sinema ya magamba weeeeeeeee hatujadili maendeleo.

Ikawepo pia Muda tunajadili DOWANS ilipwe isilipwe nchi nzima mjadala ni huo hakuna kujadili maendeleo.

Mnaweza kuongezea matukio,Nchi ikageuka Nchi ya matukio na kujadili matukio kila kukicha jamaa anatengeneza tukio kumsaidia kusogeza siku bila kujali wananchi maisha yao yako vipi uchumi unahali gani.

Matokeo yake.

Leo Shilingi Inaporomoka.

Bei ya Sukari kwetu Bkb ni 2900

Chumvi aloacha Mkapa Tsh 50kifuko kidogo leo Tsh 500.

Umeme Haupatikani

Mafuta shida Tupo kumbe CCM ina share OILCOM

Bei ya Vyakula imepanda kwa asilimia 100

Uchumi wa Nchi unayumba

Dola leo 1640

Mafuta ya Taa leo 2000

Mpaka ameacha Reserve za kutosha leo hatuna Reserve hata ya kutumia miezi Mitatu.

Mkapa ameacha makusanyo ya Ndani ni bn 250 na dola ikiwa Tsh 1100 leo makusanyo ni bn 400 wakati Dola ni 1600.

Mfumuko wa Bei umeongezeka mpaka wamebadili Formula.

Wana Jf jamaa ametuendesha kisanii Tazama lack of Seriousness Mramba na Mgonja wapo mahakamani kutokana na makosa yaliyotokana na sheria mbovu ambayo inampa mamlaka waziri kusamehe kodi yoyte yule kosa ambalo leo anaweza kulifanya mkulo hatujasikia sheria hiyo ikibadilishwa.

Richmond hatuna sheria inayo simamia swala la Dharura na kutokana na makosa hayo leo tunaweza kurudia kosa lile lile.

Tazama usanii leo wameleta Mitambo ya Megawati zaidi ya 200 inatumia Mafuta kama IPTL wakati huo huo IPTL wanashindwa kuzalisha megawati 100 kwa ukosefu wa mafuna na mwaka 2008 waliweka mitambo ya Megawati 60 kule mwanza ya Mafuta wakashindwa kupeleka mafuta tukalipa Capacity charge kwa Alstrom kipindi chote cha Mkataba mpaka jamaa walipoondoka,leo Tena Aggreco kapewa Tenda hiyo hiyo apeleke Mtambo wa Mafuta mwanza sijui kipi kimebadilika leo tuweze kupeleka Mafuta hayo mwz ambapo mwanzo tulishindwa.

Sasahivi nchi inaongozwa kwa Msingi wa Majungu ole wako ugombane na Ridhwani waulize Bashe na Masauni watakueleza,leo mtoto anafanya Dili zote kuanzia kusafisha Vyoo Mpaka kusafirisha Madini,

Usipomuona Rizy ktk Dili utamuona 2nd First lady Alkhuroos Rahma kaibuka hapa mara Pale ,Kampeni za CCM zilitengwa Bilioni 6 kwa ajili ya Familia Ccm kina makamba wakawa wanapiga kelele hapa hapa Dar,chama kimekufa Nchi iko HOI jamaa anaongea Ngonjera Mara nitajenga viwanja vya Ndege,Mara Meli,Mara mnataka Ngeleja abebe Maji kwenye ndo apeleke Mtera?mara matatizo mwl Nyerere alishindwa hata mm siyawezi.

Katufanya watu wa Matukio kuanzia ktk chama mpaka serekalini 2015 ifike aondoke sana Tupo anajisifia shule za kata wazee wetu waliuza kuku,mbuzi,mazao kila kitu wao wameshindwa kuleta waalimu inaudhi basi tu.

Ongezeeni matukio mengine.Kila jambo Inaundwa tume ,ichunguze sasa wanataka kuchukua na UDA yetu .

Shyrose Banji(chotala wa kihindi),amekuwa msaka madaraka sana ndani ya magamba lakini bahati mbaya sana amekuwa akipigwa chini,si ubunge wa kuchaguliwa Kinondoni,si viti maalum wala ukuu wa wilaya hajaambulia.Yeye ni mrembo na mzuri wa kujirusha hata na watoto,hivyo alijua Mr. Bean JK angenasa haraka na mambo yake yange nyooka ndani hata ughaibuni that's why she gave him a lot of support just then.

Ni kweli ni mpambanaji mzuri hasa katika maswala ya mass com,lakini huangushwa na tabia zake zisizokuwa na haiba ya nidhamu(kuendeleza mapenzi ya kitoto na scandal za mbali mbali za ufuska).Hii ni tabia ambayo inaweza kumu-outsmart kiongozi yeyote wa kisiasa hasa mambo yanapokuwa wazi wazi sana.

Namuunga mkono kumkosoa JK tena sana tu lakini siungi mkono kilichopo moyoni mwake kwani kinaweza kuwa so personal kuliko tunavyodhani.Namshauri atumie mijadala ya wazi kama TV na vikao vyao vya chama kumkosoa JK na sio katika fb ambapo tunaosoma ni wachache,hivyo wengi hawajui anasema nini!

Hivi huyo Shyrose bhanji, kaishalifanyia nini taifa letu au ana msaada gani! naona kila siku Pro-CDM-JF, mnaangaika nae.
Mnatoa umbea kule FB mnaleta JF, Magwanda bana au kwa sababu shemeji yenu demu wa Sugu

Mkuu hapo kwenye RED! Huyu mdada kwa kuweza kutoa hayo mawazo mbele ya Jamii bila kujificha kama wengi wafanyavyo nathubutu kusema kalifanyia taifa makubwa kwa sababu uende wana-ccm wakaamka na kutuondolea matatizo ya taifa letu!

Tatizo kwa wengi wa watanzania ni kudhani marais, mawazi, makatibu wakuu n.k ndiyo wanalitendea taifa hili mambo mema na ya kukumbukwa! Huu ni mtazamo potofu kabisa!!!!!!!!!!!!

Shyrose isije ikawa ni visa baada ya kuambulia patupu CCM ,ila kama yanatoka moyoni hongera and keep it up!

Back
Top Bottom