PSI Factor
Member
- Apr 21, 2011
- 32
- 143
Wakuu,
Nina tatizo moja ambalo sijui kama binadamu wenzangu mnalo. Tatizo hili ni tangu nikiwa mtoto (miaka ya 70) na nimeendelea kuwa nalo.
TATIZO:
Nikikiangalia (au kusikiliza) kitu kwa muda mrefu huwa napata sura zaidi ya 4 ya kitu hicho. Sipendi hii hali na inaninyima raha sana.
Mifano:
Nikiiangalia picha moja naweza kukuonyesha hata vingine ambavyo wewe kama mwangaliaji hukuviona kwa haraka. Nikimwangalia mwadamu mwenzangu usoni wakati anaongea naweza kusahau kusikiliza nikaendelea kumwangalia kwa kama dakika 10 nikaweza kujua kama ni mwongo, mkweli, anafanya ushirikina n.k.
Nimeoa, nikimwangalia sana mke wangu huwa najiuliza sana nini kilinisababishia nikaoana na mtu huyu, lakini nikiondoka kwenye concentration ya kuangalia basi namwona wa kawaida na anapendeza kweli.
Hata kusikiliza hali ipo vilevile, nikisikiliza sauti ya mtu au mnyama napata hisia mbaya kiasi nafikia kusikia kama wanyama wanaongea, hii hunisaidia hasa nikikutana na mbwa au paka, nikikaa na mbwa hata kama ana kichaa huwa hanisumbui, wananikimbilia.
Nakumbuka wakati JK anaanguka Jangwani nilikuwa namwangalia kwenye TV, aliposema "I see" nikamwambia jamaa yangu pembeni 'anaanguka' hata haikuchukua dakika akaanguka. Niliona kama ameanza kulegea, sikuwa namsikiliza nilikuwa namwangalia usoni.
UTOTONI: Niliwahi kuiangalia picha nikaona kama inatoa machozi, picha hii ilikuwa ya Bikra Maria (mimi mkristo), lakini nilipomwambia marehemu mamangu yeye alisema ni hisia tu, akasema labda nilihadithiwa kuwa Maria analia. Tatizo ni kuwa niliiangalia sana picha ile kwakuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona sanamu kubwa kiasi kile. Sikuwa nimehadithiwa kama mama alivyofikiri.
UKUBWANI: Niliwahi kuhudhuria semina moja ya kusoma body languages, hii haimaanishi kuwa ndiyo imeniletea tatizo hili, hata mwalimu aliyekuwa anatoa semina hii nilikuwa nikimwangalia sana niliona alikuwa hajiamini. Nilipomwambia kwa nje kuwa kuna vitu alitwambia lakini alionekana kutokuwa na uhakika navyo alikiri ni kweli.
OMBI:
Niliambiwa na rafiki yangu ninayefanya naye kazi ofisi moja kuwa nikiwauliza waungwana hapa kutakuwa na wataalam wanaoweza kunisaidia. Naomba msinichukulie kiutani mwenzenu, ni tatizo linaloninyima raha. Ningependa kujua ni tatizo? Chanzo ni nini? Nifanye nini? Kuna dawa ya kuzuia hali hii?