Ni sahihi serikali kutumia chenji ya rada bila kuidhinishwa na bunge?

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Wandugu.

Nimesoma kwenye baadhi ya magazeti kwamba serikali ya tanzania imeingiziwa chenji yake ya rada katika akaunti yake iliyopo London. Taarifa hiyo imeambata na tamko la Waziri wa fedha, Mustafa Mkulo kukiri Tanzania kupokea pesa hizo na kwamba tayari serikali yake imepanga kupeleke pesa hizo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili kukabili matatizo mbalimbali yanaikabili sekta ya Elimu nchini.

Nijuavyo mimi ni kwamba kazi ya serikali ni kupanga matumizi then bunge linayaidhinisha. Je ni sahihi serikali kujipangia na kujiidhinishia matumizi bila baraka za Bunge?
 
Mimi naona bora hivyo tu, kuliko kupeleka kwenye bunge la Bi. Kiroboto ambako watapitisha azimio la kuzipiga pasu na kujiongezea posho, eti kwakuwa maisha yao pale Dom yanakuwa magumu bila hela nyingi!
 
Bunge la bibi kiroboto inachekesha hiyo, mbona Watanzania kazi tunayo hadi 2015!!!!!!
 
Wandugu,
Nimesoma kwenye baadhi ya magazeti kwamba serikali ya tanzania imeingiziwa chenji yake ya rada katika akaunti yake iliyopo London. Taarifa hiyo imeambata na tamko la Waziri wa fedha, Mustafa Mkulo kukiri Tanzania kupokea pesa hizo na kwamba tayari serikali yake imepanga kupeleke pesa hizo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili kukabili matatizo mbalimbali yanaikabili sekta ya Elimu nchini.

Nijuavyo mimi ni kwamba kazi ya serikali ni kupanga matumizi then bunge linayaidhinisha. Je ni sahihi serikali kujipangia na kujiidhinishia matumizi bila baraka za Bunge?

Ukitaka usiumwe kichwa fanya kama hujasikia hiyo habari. Nje ya hapo kanunue kopo la panadol, ndo uanze kufatilia upuuzi wa serikali yenu!!!
 
Wandugu,
Nimesoma kwenye baadhi ya magazeti kwamba serikali ya tanzania imeingiziwa chenji yake ya rada katika akaunti yake iliyopo London. Taarifa hiyo imeambata na tamko la Waziri wa fedha, Mustafa Mkulo kukiri Tanzania kupokea pesa hizo na kwamba tayari serikali yake imepanga kupeleke pesa hizo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili kukabili matatizo mbalimbali yanaikabili sekta ya Elimu nchini.

Nijuavyo mimi ni kwamba kazi ya serikali ni kupanga matumizi then bunge linayaidhinisha. Je ni sahihi serikali kujipangia na kujiidhinishia matumizi bila baraka za Bunge?

Matatizo ya pesa kama hizi ambazo hazikupangiwa bajeti uwa ni uchakachuaji tu....tazama pesa za EPA walipeleka pale TIB zikatafunwa na wahuni...baadae yule Director wa ile benki alisema wazi yeye afahamu kuhusu ujio wa hizo pesa...ni bora zingeenda bungeni zikawekewa mikakati ambayo at the end you will be in the position moderate matumizi yake..vinginevyo hizo zinatumika kwenye uchaguzi wa NEC 2012 na General election 2015....
 
yaani shukuru walau hata umesikia wamesema kuwa watazipeleka huko...wamejitahidi sana...mi wasiwasi wangu ulikuwa ni hata huko kusema tu wanampango nazo gani wasingesema tungeishia kusikia tu zimerudishwa afu basi...maana kama kuliwa ni swala lililo wazi kuwa zitaliwa tu..
 
Bunge la ndiyooooooooooooooo hata ufanyeje wale maslahi yao kwanza .Rada ilinunuliwa kupitia Bungeni ? Mbona wabunge walienda kudai pesa kama rada haikupitia huko ?Na pesa imekuja inaishia nje haijaingia bungeni ?
 
Kwani nchi hii kuna Bunge? Acha ziende wizara ya elimu kama njia ya kugawana tu, si ulisikia pesa za epa, bodi ya pamba na nyinginezo.
 
Another CHADEMA strong agenda,ni kukosa umakini tu pesa ambayo haikuwemo kwenye bajeti inapangiwa matumizi bila kupitishwa na Bunge,huu ni ufisadi mwingine!
 
Wizara ya elimu ni kituo cha kufanyia mgao! Wameamua kutupumbaza eti pesa zinaingizwa elimu kutokana na matatizo yaliyopo.
Hivi nchi hii wizara yenye matatizo ni moja tu, imesemwa mara ngapi kuhusu hali mbaya za mahabusu na magereza kote nchini, vp kuhusu kuchechemea hospitali za mikoa, wilaya na hata vituo vya afya na wimbo usioisha wa ukosefu wa dawa na watenda kazi?
Kwa uchache karibu wizara zote ziko na shida chungu mzima, ila wanjanja wachache wameshauri kituo cha kugawana mshiko kiwe MOEVT, kila la kheri!

Kwenu mafisadi na wapambe wenu mliomo humu JF na kwingineko, siku inakuja ambapo madhila yote mlotenda yatageuzwa hati za mashtaka yenu! Nasema kwa sasa hamuwezi kuelewa mioyo ya watanzania jinsi ilivyobakiza sehemu ndogo sana ya uvumilivu..
Endeleeni kijidanganya hivyo hivyo huku mkishushia na mvinyo kuwa hao mnawaongoza bado ni mbumbumbu..., Siku inakuja na wala si mbali kama mnavyodhani.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom