Ni sahihi/ruhusa kutoka na ex wa rafiki yako?

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,043
21,517
Suppoze una rafik yako wa karibu ambae mnapendana na mnashirikishana kwa kila jambo. Anakutambulisha kwa mpenz wake(shem wako) na urafik wenu unazid kukua. Inatokea rafiki yako na mpenz wake wanagömba na kuachana kabisa na kila m2 kushika lake. Je,inawezekana ukatoka na huyo shem wako baada ya kuachana na rafiki yako? Pili,utamweleza nin rafiki yako? Utamweka wazi au utasubir had aje agundue mwenyewe? Na unahis rafk yako atajiskiaje baada ya kugundua unatoka na ex wake? Mchango wenu muhimu
 
Mweleze kabla hujapiga hatua yoyote. Ikibi mulize kwa nini waliwachana ili usijekurudia makosa yake. Kama walitengana kwa mambo madogo, mueleze dhamiri yako. Akikuruhusu, mbele kwa mbele. Kamwe usiende na huyu dada ikiwa bado unathamini urafiki wenu.
 
Ni kweli but at the sametime,huoni kama inaweza jenga uadui? Kwasababu wanaweza wakawa wameachana but stil kumbe bado anamfeel m2 wake.
 
Hauna sababu ya kuwa na hofu iwapo wewe haukuwa chanzo cha kuachana kwao.
Kikubwa ni kuwa makini. Isije kuwa unakimbilia nyuki wakati mwenzio amewakimbia.
 
Ni ukwel Husninyo maana wahenga walonga Ukipenda Asali Basi Jiandae Kumkwepa nyuki
 
Hivi kuwekeana post za kujaribiana ndo lengo la jukwaa hili? Kama mtu ana tatizo si aseme asaidiwe.... Mzeewaloliondo, hili jukwaa si kama ile central page ya gazeti fulani unapokutaga mada 'ukigundua mumeo anatembea na mamako' au 'siku ukigundua mumeo ni shoga'. Halafu unakuta mijitu inatuma SMS kwa nguvu zote kuchangia topic. Hebu tu-mantain hadhi ya jukwaa!
 
Ha ha ha ha jamaa umekuwa mkali ni wewe nini unachukuliwa ex wako??
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hivi kuwekeana post za kujaribiana ndo lengo la jukwaa hili? Kama mtu ana tatizo si aseme asaidiwe.... Mzeewaloliondo, hili jukwaa si kama ile central page ya gazeti fulani unapokutaga mada 'ukigundua mumeo anatembea na mamako' au 'siku ukigundua mumeo ni shoga'. Halafu unakuta mijitu inatuma SMS kwa nguvu zote kuchangia topic. Hebu tu-mantain hadhi ya jukwaa!

Sasa kwani mlitaka aleteje mada? mbona iko wazi? mbona wote waliosapot wanatoaga mada kimtindo huu hawajiongelei wao bali wanajifanya rafiki yangu mara jirani yangu mbona huw hamjikosoi? acheni hizo kama ameleta ki indirect ni yeye aliamua sie tuchangie na sio kumbeza, na kama mnapenda true story mbona watu humu naweza kuwamention wanaleta mada zinazowahusu wao kabisa still mnawabeza? acheni upendeleo jamani ,ndio hivo
 
that is not good hata kidogo, hata kama ni Ex, put yourself under her shoes na utapata jibu, kama yeye akikufanyia ivo utajisikiaje? ina maana ulikuwa unamtaka huyo shem wako hata kabla ya kuachana na pia anaweza hisi wewe ndo ulikuwa chanzo cha wao kuachana. TAFUTA WAKO BIBI WEEEEEEEE
 
Kwani ni lazima sana utoke nae huyo? kwa nini usitoke na wa kwako kama unampenda rafiki yako? au wewe ndio chanzo cha ugomvi wao? Unajua nini bwana mkubwa, jamaa atajua wewe ndio umesababisha kutoelewana kwao. Ila kama mapenzi yenu ni makubwa sana na unaona huwezi ishi bila huyo demu usijibane pia, mweleze ukweli rafiki yako na uwe tayari kupokea lolote atakalosema inaweza urafiki wenu ukafikia kikomo kabisa.
 
Mie nashanga eti awe muwazi uwazi gani kupita maelezo aliyotoa?

So hivo wangu, unajua unapotoa tatizo kama lako, au la mtu wako wa karibu ni tofauti na unavyosema 'hebu wazia hili', michango ya watu itakaa kuimajini imajini vile vile. Lengo la jukwaa si kupeana challenge za kupotezeana muda, kuna watu wana solution za maana, ila akikuta mambo yenyewe hayako serious anaona ya nini apoteze muda wake wakati hauna msaada kwa yeyote...
 
Kibao kimekugeukia mwana unaona sasa! pole mkuu
 
I have been dating my friend's ex-girlfriend for 5 years. Ila jamaa hajui!!
 
I have been dating my friend's ex-girlfriend for 5 years. Ila jamaa hajui!!
Hongera sana lakini usifikirie 100% kuwa hajui. Kimya chake kina mshindo.
By the way, was/is he your best friend? If YES, hongera nyengine.
 
Hongera sana lakini usifikirie 100% kuwa hajui. Kimya chake kina mshindo.
By the way, was/is he your best friend? If YES, hongera nyengine.

Yes he is one of my best friends. Ila jamaa alimwacha demu akaoa mwanamke mwingine. That is when I became her crying shoulder!
 
Back
Top Bottom