Ni sahihi kwa kiongozi wa mbio za mwenge kuwashambulia wapinzani?

ukitaka kulala usingizi mwanana baada ya machovu ya kutwa nzima pitia humu jamvini vry interesting.

Kweli mkuu, hata mimi niko hapa naperuzi habari ili nitafute usingizi,JF ni kiboko kwa kuburudisha
 
Hako ka kapteni nakaona ni ka mcharuko jinsi kanavyo onge. Eti barabara za baba rizi! Kwa biashara ipi?
 
Juzi viongozi wa kata wamepita kudai mchango wanataka kujenga jengo la utawala katika shule ya kata yetu. Tena nawajua ni magamba wazuri sana niliwapiga maswali sidhani hata kama watarudi tena nikakumbushia na zile za ujenzi wa shule. Swali langu
kuu lilikua ni kwanini wanatuchangisha pesa then wanakuja kutangaza CCM imejenga? Sasa nawangojea hao wa Mwenge waje wadai hela ya mafuta.
 
Mwenge ni wa kisiasa. Umeandika kwenye makaratasi tu kuwa sio wa kisiasa ila vitendo vya wa uendeshaji wake ni vya kisiasa. Kwa bahati mbaya sana serikali ya CCM huwa inawekeza kwenye upuuzi. Sioni sababu ya msingi ya kukimbiza mwennge kuzindua miradi.

Na yeye kusema kuwa wapinzani wanasema serikali imeshindwa. Hii ni kweli. Sasa kwa akili zake za masafa mafupi anadhani kujenga barabara ndio kipimo cha kwamba serikali imeleta maendeleo? Kwa serikali yoyote ile duniani moja ya jukumu lake la msingi ni kuweka miundo mbinu ya kuwezesha maswala ya kiuchumi kufanyika, hii ni pamoja na kujenga barabara lakini "zenye viwango". Hata mbwa wakiunda serikali yao kujenga miundo mbinu ni jukumu la lazima na wala sio karata ya kisiasa ya kushika wanananchi masikio!

Kusema kweli udogo wa mawazo kama hayo ya mkimbiza mwenge na wanasiasa wengi walio ndani ya CCM ni sawa na baba kujisifia kuwa analisha watoto wake vizuri,kuwa anawapeleka shule na anawalea vyema. Baba wa namna hii ni mpuuzi tu maana hahitaji kujisifu kwa sababu haya ni majukumu yake ya msingi. Kama ambavyo baba huyu hahitaji kusifiwa wala kujisifu,vivyo hivyo ndivyo ambavyo serikali hahitaji kujisifu au kusifiwa kwa kujenga miundo mbinu ya kuwezesha uchumi kwani hayo ndio majukumu yake ya msingi kabisa.

Ila kuna mambo ambayo serikali inaweza kusifiwa. Kwa mfano kama takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka jana serikali ilizalisha ajira 1,000,000 kutoka ajira 400,000 za mwaka juzi ni hivyo kuongeza ajira kwa asilimia 60%,serikali kama hii inasifiwa na inahitaji kujisifu kwa kuwa jukumu hili lipo katika mazingira tofauti.

Haya yote yanatoke kwa kuwa watu nanafanya mambo kwa mazoe,wanafikiri kwa mazoea,na wanaotesha busara za mazoe bila kujali kanuni za msingi zinazojenga mambo haya. Ila ndahani yote haya yanatoka na dharau ya madaraka
 
Back
Top Bottom