Ni sahihi kwa kiongozi wa mbio za mwenge kuwashambulia wapinzani?

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,769
10,645
Nimemsikia kiongozi wa mbio za mwenge Capt Mwanosi? wakati wa habari za jioni Star TV saa 9, akiwashambulia wale wote wanaopita "kuwadanganya" wananchi kwamba serikali haijafanya kitu. Kwamba hao hao hupita kwenye barabara hizo hizo zilizojengwa na Kikwete, kwamba hata wanapoumwa wakakosa huduma hapa nchini hurudi kuipigia magoti serikali ya Kikwete iwapeleke India, kwamba hata watoto wao wanasoma katika shule za kata zilizojengwa na Kikwete.

Mtazamo wangu: Naona kama haya ni mambo ya kisiasa zaidi na hayapaswi kuzungumziwa na Jeshi kwa vile jeshi letu halihusiani na siasa.
 
inategemea alikuwa wapi maana wengi wanajua ni pesa za ccm hasa wale wasio elimika kwani utasikia mradi huu umekamilishwa kwa pesa za serikali ya ccm.
hawazi ongea hivo mwanza au iringa tunao jua ni kodi zetu wa ccm cuf nccr tlp kila mt hata ukinunua chumvi umechangia
 
Yule nae sijui nimwitaje? Mbona kule Tabora aliweka jiwe la msingi kwenye ofisi isio na kiwango tena kibaya yenye nyufa. Ndio maana tunapinga huu mwenge kuwepo manake hauna manufaa.

Sasa kwani wajibu wa kujenga barabara ni wa nani? Na huu ugumu wa maisha utatatuliwa na hizo barabara? Mijitu mingine inapendaga kuwa furahisha maboss zao mpaka inapitiliza.
 
Nimemsikia kiongozi wa mbio za mwenge Capt Mwanosi? wakati wa habari za jioni Star TV saa 9, akiwashambulia wale wote wanaopita "kuwadanganya" wananchi kwamba serikali haijafanya kitu. Kwamba hao hao hupita kwenye barabara hizo hizo zilizojengwa na Kikwete, kwamba hata wanapoumwa wakakosa huduma hapa nchini hurudi kuipigia magoti serikali ya Kikwete iwapeleke India, kwamba hata watoto wao wanasoma katika shule za kata zilizojengwa na Kikwete.

Mtazamo wangu: Naona kama haya ni mambo ya kisiasa zaidi na hayapaswi kuzungumziwa na Jeshi kwa vile jeshi letu halihusiani na siasa.

Serikali imefanya mambo, lakini si kwa kiwango cha kuridhisha na ndio maana leo hii miaka 51 ya uhuru mtu mzima anazunguka nchini kote na kibatari akiomba michango ya mafuta ya taa ya hicho kibatari.

Dunia ya leo mataifa yanashindana kwa mambo ya maana na sio kufukuzana na vibaratari. Kila jambo na wakati wake. Tuna jumba la makumbusho!
 
Mlitaka aseme nini wakati mwenge wenyewe unatumika kutekeleza ilani ya CCM na yeye anataka U DC? ndiko walikotoka kina Rugimbana wa Kinondoni. Anayemlipa mpiga zumari...
 
Kila shughuli ya kiserikali inawekewa maneno ya kujigamba dhidi ya wapinzani wakati ni wazi kila kitu tunacholetewa sasa hivi bado haki-qualify kuita maendeleo...we are still struggling to get the basic needs. Maji, umeme, Chakula. Yani kujenga lami kuunganisha mikoa (very basic achievement) ndio tunazunguka kujifagilia bila aibu? Tukijenga vyoo mashimo kadhaa kwenye shule zetu basi viongozi utawasikia wanatamba kwenye vyombo vya habari!! Wenzetu nadhani hadi huwa wanacheka wakijisemea...ina maana walikuwa hawana vyoo miaka yote hiyo hadi leo!!?
 
Natumai lzm uwe kada wa ccm ndo uqualify kukimbiza mwenge kwani ata bwana lugimbana mkuu wa wilaya ya kinondoni au ilala alikimbiza mwenge enz izo leo kaaminiwa na kpewa cheo cha CCM, Ivo njaa kali uyo lzm abwatuke
 
Ikifikia hata guest house zinazinduliwa na mwenge, hapo ninaachwa hoi na madhumuni ya mwenge!
 
Huyo CPT Mwanosa ni mpumbafu fulani toka wilaya ya Mpwapwa, ambae kapata kazi ya jeshi baada ya kusots sana na nafikiri alipoajiriwa aliona kama mbingu zimeshuka maana alivyochemuka ni pakubwa maana ajira imemkuta akiwa ni muimba kwaya kanisa katoliki Mpwapwa.
 
ukitaka kulala usingizi mwanana baada ya machovu ya kutwa nzima pitia humu jamvini vry interesting.
 
Tumedanganywa kiasi cha kutosha na ccm, tumenyanyaswa kiasi cha kutosha na ccm, tumepuuzwa kiasi cha kutosha na ccm, tumedharauliwa kiasi cha kutosha na ccm. Sasa kwa pamoja tunasema basi ccm, inatosha! Tumekuacha.
 
InA Maana Kodi zetu tunazopigwa double double kwa Maendeleo yetu CCM ndio wamelipia ?....Pumbavuuuuu

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kama kasema hivyo basi amekosea sana, maana madhumuni ya mwenge yalikuwa...
1: Kuleta upendo palipo na chuki (upendo hadi kwa vyama pinzani)
2: Kuleta Heshima palipojaa dharau(si kudharau vyama pinzani)
3: kumulika hata nje ya mipaka yetu na kuleta TUMAINI.
 
Back
Top Bottom