Ni sahihi kulazimisha kumjua babako?

Ni sahihi kumlazimisha Mama yako kukwambia Baba yako ni nani kama yeye mwenyewe hajisikii kufanya hivyo?

Hapa namaanisha kwa yule aliyezaliwa nje ya ndoa au baada ya kuzaliwa ndoa ikasambaratika akiwa bado mdogo.

...naamini ni haki ya mtoto kuambiwa Ukweli!

Kwanini kina mama wengi (single mums) hawapendi kuwaambia watoto baba zao?

Kuficha ukweli kunapelekea kuwabebesha mizigo watu baki kwenye malezi ya baadae ya hawa viumbe.

Badilikeni!
 
Mimi nafikiri kumfahamisha mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa baba yake ni nani wakati baba huyo hakutaka mtoto bali starehe - ni kumtesa mtoto.Fikiria mtoto anayezaliwa na mama hohehahe wakati baba ni kigogo fisadi.Fisadi huyo hataki kujihusisha na mama wa mtoto kwa vile wako dunia mbili tofauti....Kulazimsha kumjua baba yako kunaweza kukupa msongo wa mawazo na akili bureeee...bora wakae na mama zao tu.
 
...hapana, kulazimisha maana yake kutaka kujua ukweli whatever the consequences!

Jinsi mtoto atavyo u handle huo ukweli ni yeye na maisha yake. Naweza kukubaliana na kina mama wanaosubiria mtoto angalau afikishe umri muafaka wa kuambiwa ukweli kulikoni yule ambaye anakwenda na siri yake kaburini!

msiwanyime haki zao watoto, kosa la mzazi/wazazi lisimhusishe mtoto kujua/kupata haki yake.
 
Kumjua baba ni haki ya mtoto, tena haki msingi kabisa. Kumbe mama ana wajibu wa kumwambia mtoto baba yake ni nani: Hii pia inamsaidia mtoto kujua nasaba yake na identity yake. Bila kumjua baba kunaleta psychological imbalance ndani ya mtu. Akimjua baba mtu anatulia.
 
...kabisa bana, huyo mama asingemjua aliyempa mimba angetulia?
 
Back
Top Bottom