kibavu
Senior Member
- Oct 15, 2008
- 136
- 82
Umekua ni utaratibu kwa viongozi mbalimbali wa kuteuliwa na kuchaguliwa kuapishwa kwa kushika vitabu vya dini/madhebu yao na kuapa kwamba watailinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini watu hao hao wakifanya makosa na kukiuka kiapo chao hushitakiwa kwa mujibu wa sheria zilizotungwa kulingana na katiba ya Jamhuri. Hoja yangu ni kwamba kuna haja gani ya kuapa kwa kutumia vitabu vya dini, na watu wanapokosa wanashitakiwa kwa kutumia sheria za jamhuri? Na je ni kwa nini wasiape kwa kutumia katiba ambayo wanaahidi kuilinda? Najua kuna watu wanaapa kwa kutumia katiba, Kwa nini isingekua hivyo kwa wote kwakua wote wanatumikia katiba ya Jamhuri na si madhehebu/dini zao?
Nawasilisha.
Nawasilisha.