Ni sahihi fomu za Polisi, Guest House kuandika kabila?

Mwitongo

JF-Expert Member
Jan 30, 2009
312
360
Ndugu zangu, nimekuwa nasumbuliwa sana na suala la ukabila. Ukiingia Guest House au Polisi kuna kipengele cha kuandika kabila lako. Hili jambo linaniudhi sana. Sijui wengine mna mtazamo gani?
 
Mwitongo tatizo liko wapi, si wanataka wajue wewe ni mwenyeji wa wapi hasa linapotokea tatizo eidha kufia guest na mambo mengine kama hayo.
 
Bila shaka wewe utakua Mtanzania mwenye asili ya Kiasia...hebu andika Gujarat, Han n.k
 
Mwitongo tatizo liko wapi, si wanataka wajue wewe ni mwenyeji wa wapi hasa linapotokea tatizo eidha kufia guest na mambo mengine kama hayo.

Tatizo ninaloliona ni kwamba huwezi leo kumpata Mtanzania kwa kutumia kabila. Sana sana utampata kwa kujua anaishi wapi. Kwa mfano, Mtu akijitambulisha kuwa ni Mmakonde, akafia gesti, utajuwe kuwa anaishi wapi? Tanzania kila kabila lina fursa ya kuishi popote. Nashauri suala la ukabila katika fomu za polisi na gesto hausi lifutwe.
 
Ndugu zangu, nimekuwa nasumbuliwa sana na suala la ukabila. Ukiingia Guest House au Polisi kuna kipengele cha kuandika kabila lako. Hili jambo linaniudhi sana. Sijui wengine mna mtazamo gani?

Je baada ya kumaliza kutaja kabila lako huwa unapata tatizo gani?.Watu wanakucheka? au? Nakushauri just try to change your mindset then you will be free.
 
Mwitongo tatizo liko wapi, si wanataka wajue wewe ni mwenyeji wa wapi hasa linapotokea tatizo eidha kufia guest na mambo mengine kama hayo.
Sioni kama kwa kuwepo na kabila unaweza kujua huyu bwana ni mwenyeji wa wapi!..mfano ukiandika msukuma wanajuaje wewe ni mwenyeji wa wapi ilhali kuna wasukuma zaidi ya mikoa mitano!
 
we unashangaa form za guest house pekee mbona hushangai charge sheet?
ni tatizo bora iandikwe mkoa na sio kabila
 
Back
Top Bottom