Injinia
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 849
- 26
Ndugu zangu,
Nimeona kule kwa Michuzi kwamba eti Bunge la Tanzania limepewa msaada wa kompyuta, tena zenye thamani ya TShs Milioni 20 tu, toka kwa ubalozi wa Korea ya kusini!!
==============
Korea Kusini yalipatia msaada wa Komputa Bunge
Juu na chini: Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah akipokea msaada wa Komputa 18 zenye thamani ya zaidi ya million 20 toka kwa Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Young Hoon Kim. Komputa hizo zimetolewa na Ubolozi huo nchini kusaidia matumizi mbalimbali kwa waheshimiwa na watumishi wa Ofisi ya Bunge. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge
Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Young Hoon Kim akimweleza katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah namna nchi hiyo inavyokusudia kusaidia Bunge la Tanzania katika maswala ya Teknolojia ya mawasiliano mara baada ya kukabidhi msaada wa Komputa 18 zenye thamani ya zaidi ya million 20 katika Ofisi ndogo ya Bunge Dar es salaam jana. Waliosimama toka kulia ni Mkurugenzi wa Mipango na ICT wa Bunge ndg. Siegfied Kuwite na Msaidi wa Katibu wa Bunge Emanuel Mpanda. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge
========================
Hili jambo limenichekesha pamoja na kunishtua.
1. Hivi kama hadi BUNGE la nchi linapokea msaada, hii nchi inaelekea wapi?
2. Je, ni kweli Bunge kama mhimili mkuu wa serikali, halina uwezo wa kununua kompyuta zake lenyewe?
3. Hizo kompyuta zimepitiwa na wataalamu kuangalia uwezekano wa kuwepo kwa virusi na vifaa/programu za kiuchunguzi (yaani, spying)?
Yaani nimekosa raha kabisa kwa hili jambo. Tunaingiliwa hadi jikoni, tena tunafungua mlango wenyewe!