Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,301
Wewe unavyoona kuna mwelekeo wa maisha bora chini ya JK? Kama sivyo ni vema tukajiuliza ni nini kilichotuloga kumpa "kula" za kishindo mwaka 2005 ili tusije kufanya kosa kama hilo wakati mwingine! Mimi nionavyo JK alivinunua vyombo vya habari na kuweka mtandao mzito wa kumnadi! Tunaona hadi kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 vyombo vya habari vilimgeuka na mtandao ulisambaratika na kubakia yeye (JK) na familia yake tu, yaani BMW - Baba, Mama na Watoto!
Simple ni mapenzi na imani juu yake ndio iliyomfanya apate ushindi wa kishindo! wakati ule watu walikuwa na imani na JK kama walivyokuwa na imani na Dr Slaa leo hii. Kufeli kwa slogan ya maisha bora na sera kama za elimu na kilimo kwanza ni changamoto as yeye sio mtendaji wala mtunga sera wanaomwangusha ni watu wake kwahiyo labda tuone amewajibikaje kuhusu watu wake kufanya sera zishindwe kufanya kazi. Lakini pia haiwi basi kwa kumkejeli na kumdhihaki yeye ana ndugu ana watoto wanajisikia vibaya mnavyomdhalilisha hivi wewe mjomba wako au baba yako akidhalilishwa utafurahia? pia JK kama alivyo Lipumba, Mbowe, Dr Slaa, Cheyo na kina Mnyika na JK pia ana watu wanaompenda ikiwa leo wanaCDM wanaona uchungu kukejeliwa kwa viongozi wao basi mjue kuna watu wenye mapenzi na JK wanaumia kama nyie mlivyo na mapenzi na kina Lipumba na Dr Slaa na mnaumia mkitukaniwa viongozi wenu.
Napenda kumalizia kwa kusema jambo usliopenda wewe au mtu wako afanyie basi ni busara usimfanyie mwenzio. Lugha zinazotumika kuuliza haya maswali sizo. Tunayo nafasi ya kujirekebisha.
Kuambiana kupo kusikilizana hakupo!!!!