Elections 2010 Ni rais wa CCM au wa Tanzania?

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,247
342
Nimeangalia picha ya watu waliohudhuria sherehe za kuapishwa Jk kama Rais wa Tanzania. Picha hizo zilinishtua pale nilipoona watu wamevaa mavazi ya CCM na kubeba bendera za CCM. Nikajiuliza, hivi watu wanaelewa kwamba wako wapi na wanafanya nini? Viongozi kutoka nchi zingine wanatutambua kama Watanzania na wamealikwa kuja kushiriki sherehe za kuapishwa rais wa Tanzania (hata kama anatokana na CCM), bendera ya CCM inatambulisha nini? Mbona Jk hakuwa amevaa nguo za CCM? Au watu wameishiwa na nguo hivyo wanavaa hizo za mgao wa CCM? Au ndo yale matatizo ya kusombwa na malori kwenda kwenye kampeni za CCM bila kufikiri kampeni zimeshaisha.

Hayo ni matatizo makubwa ambayo yanapaswa kurekebishwa katika vichwa vya watu hasa kwamba tuone utaifa wetu unazidi Vyama vyetu. Tukiweza kufika mbali kidogo tunaweza kutambua kuwa maslahi ya taifa ni makubwa kuliko ya Chama.
 
ni kweli tunahitajika kubadilika kama kweli tunataka kuifikisha Tanzania sehemu,,,; watu wetu na viongozi wetu bado elimu na uelewa wao kiujumla ni mdogo sana HUWEZI KUHUBIRI UMOJA WA KITAIFA WAKATI unachokifanya in real sense hakiashirii umoja,,,,,
 
Wana CCM wanawanaona chama chao ni zaidi ya Tanzania. Vile vile uelewa wa wanaccm ni mdogo katika mambo mengi. Ni watu wa kufuata propaganda kuliko hoja.
 
Jibu ni gumu. Tungejua alipata kula halali ngapi ingekuwa rahisi kutoa jibu. Saa hizi ni guess work. Inawezekana akawa au asiwe na bahati mbaya hatutapata kujua so kuwa safe side enenda na uongo wa NEC na kumtambua kama Rais wakati ukimwomba Mungu akufunilie kujua kama ndiye au la!
 
Back
Top Bottom