Ni pombe gani ya kienyeji unaikubali kupita zote?

Aisee ukute umepata hapo kitochi ya MBEGE na mbusi ya kuchoma yenye pilipili nyingi ukiwa umekaa kwenye kipande cha gogo la mkerewiria kama saa tisatisa hivi jioni acha banaaaaaa!!!
 
10 bora ya Pombe nzuri za asili:
1. KOMONI
2.ULANZI angalizo:Uupate ule MKANGAFU au MDINDIFU (sio MTOGWA)
3.KIMPUMU
4.MCHUJO
5.MBEGE
6.KYINDI
7.WANZUKI
8.KIJOTI
9.GONGO (ya mbeya)
10.GONGO (ya bukoba )
Gongo la Kagera hasa kutokea Karagwe na Kyerwa ndo pombe ninayoikubali inaitwa ENGULI/KALINYA kuna namba yake inaitwa EMBANDULE (Super)hii km huna kerosene unaweza washia kibatari/chemri. Duu,nimeimiss kinoma
 
Gongo la Kagera hasa kutokea Karagwe na Kyerwa ndo pombe ninayoikubali inaitwa ENGULI/KALINYA kuna namba yake inaitwa EMBANDULE (Super)hii km huna kerosene unaweza washia kibatari/chemri. Duu,nimeimiss kinoma
Naamini ipo siku hii gongo itakuja kuwa branded na serikali Kwan ndo gongo ambalo viongozi wengi kutokea mkoa Kagera wanalipigia sound liwe kwenye soko la kitaifa kwan ni pombe ambayo inasafirishwa kimagendo kwenda Rwanda,Burundi, Uganda,Congo drc, nk. So serikali inakosa pato bila sababu za msingi kabisa,karibia mikoa yote ya kanda ya ziwa inategemea pombe hii toka Kagera ambapo huitwa Kaitaba.Wenyeji wa kagera waishio Dar ndo vinara wa kuagiza hii mali wanayoimiss sana.Baada ya krismass zile private cars toka huko ni lazima wabebe package ya kutosha km zawadi kwa ndugu na marafiki waishio Dar/Dom
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom