ni pesa au dhahabu zinazopelekwa BOT,kwenye maroli yenye container?

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
8,314
13,279
jamani kuuliza sio vibaya,nimepita hii mitaa ya bank kuu ya tanzania(BOT)nikielekea ocean road,nimekuta njia imefungwa kuna polisi kama 30!wenye siraha,huku kuna malori kama 6 yenye makontena yanaingia BOT!na kwa kweli kama utatokea uvamizi hapa balaa yake sio ndogo,ndio maana ikabidi nibadilishe njia mapema,kwani hawachelewi kukwambia taarifa za kintelijensia zinakushuku wewe!!sasa zile ni pesa au dhahabu au nini?na mbona malori yenyewe yamechoka choka sana?
 
hayo yamepita hata hapa dodoma midahii ya saa 9 yapo mawili na ving'ora kwa wingi sana,inaelekea yanatokea somewhere kanda ya ziwa!
 
Nakumbuka cku moja wanajeshi walikuwa wanatoka kuchukua noti zao walivyofika ubungo kukata kuelekea sam nujoma likachomoka sanduku moja la noti aisee kilichotokea ni balaa la ajabu zilipigwa risasi hewani nyingi tu watu wakakimbia pakawa peupe ghafla wakachukua hela zao wakaondoka kama kweenye video vile!
 
ni pesa zinatoka mikoani, hio inaitwa precious cargo na ulinzi wake unakua km wa kijeshi
 
mkuu zile ni hela na zinakua zinatoka airport,kuna ndege ambazo zinazileta kutoka mikoani then yale malori chakavu ndo yanazipeleka BOT.
 
ni mzigo wangu nimeutunza kwa benno ndulu nitauchukua weekend, msiogope wazawa wenzangu, benki kuu ni yetu wote
 
jamani kuuliza sio vibaya,nimepita hii mitaa ya bank kuu ya tanzania(BOT)nikielekea ocean road,nimekuta njia imefungwa kuna polisi kama 30!wenye siraha,huku kuna malori kama 6 yenye makontena yanaingia BOT!na kwa kweli kama utatokea uvamizi hapa balaa yake sio ndogo,ndio maana ikabidi nibadilishe njia mapema,kwani hawachelewi kukwambia taarifa za kintelijensia zinakushuku wewe!!sasa zile ni pesa au dhahabu au nini?na mbona malori yenyewe yamechoka choka sana?

Nini kama si raha? taabu?
 
Back
Top Bottom