Ni password au anatafuta sababu?

Kuitaka password yako kwa nguvu ni moja ya kigezo cha kukutafutia sababu ili mshindwane
Kutokana na maelezo yako, mwanamke mwingine na amegundua unalifahamu hilo, hivyo nae amehisi umeshapata mwanaume mwingine na mawasiliano yanafanyika kwenye emails. Jambo la msingi muulize taratibu kisa cha kuitaka password ghafla ni nini? Je yeye yuko tayari kukupatia ya kwake?....yeye akitumia vitisho vya kukata mawasiliano ili umpe hiyo password kubaliana na maamuzi yake.
 
Hana lolote anatafuta sababu ya kuondokea tu, labda huyo mwanamke mpya amempa password, mko kwenye mahusiano miaka 4 hajawahi omba password why leo?
 
Anaomba kinguvu pasword muulize hivi "unajua kubonyeza kompyuta?
 
Mkubwa mimi sim-support huyo mtu wako kwa hilo analofanya, ila ninalo jambo kama si kijambo!!!

Mtu haanzi from no where kuomba password, so badala ya kujionyesha kwetu kuwa wewe u mtakatifu na kuwa yeye ndo ana matatizo, ni afadhali useme umemfanyia nini mpaka aonyenshe dalili za kutokukuamini? naamini lipo jambo na bora uliseme ili wanajamvi wakushauri ipasavyo ilasivyo kumbuka kuwa "mficha maradhi......"
 
kama huna issue za kuficha mpe, halafu yy usimwombe yake.

Ukimwomba utaonekana ww ni mtu wa visasi, kwa maana nyingine aki cheat na ww uta-cheat.

Usipomwomba yake kama anaakili roho itamwuuma sana coz ataona kuwa ww unamwamini ila yy ndo mkorofi.
mpe alafu mwambie aseme na kingine.
ONYO PW ATM NEVER TRY AT HOME.
 
Na huyo mwanamke alienae amemwambia amegombana na mim cku nying kwamba hatarajii kurudiana na mimi, though hajui km mim nimeshajua hlo kwamba ana m2..
 
Hapo kuna mawili yawezekana kuna kitu amehisi kuhusu wewe sasa anataka kuchunguza na ametumia gia mbaya kwani kama ni uchunguzi basi kesha haribu sehemu ya ushahidi kwani hata kama lilikuwepo tayari unaweza kwenda kufuta.

La pili inawezekana ni WIVU, wivu ni jambo kubwa sana katika mapenzi na wivu unaweza kumsukuma mtu kufanya jambo la ajabu sana, ili kupata nenyendo zako anaanza kukaba, kwa hiyo wala usimlaumu yawezekana na wivu.

NB: Ushauri wangu kama wewe ni mfanyakazi na kama yeye shida yake ni kusoma Email zako Log in kisha muachie asome kwani kumkabidhi password yako wakati bado hamjaoana kama kuna mambo nyeti ya kazini ambayo ni confidential inaweza kuwa hatari ila kama hakuna mambo mengine ambayo ni ya kiusalama zaidi katika Email yako mtoe wasiwasi mpatie.
Kwanini jambo dogo liwagombanishe bwana.
 
Ni marufuku kuandika kwa style uliyotumia mleta mada, fanya editing kabla mods hawajaifuta nyuzi yako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom