Ni Paka kweli au jini?

Mkuu mi nakushauri kama ni mara ya pili huyo nyau anakuja basi hapo kuna mkono wa mtu ndugu na kwa nini aje mara ya pili? Sasa nakushauri sali sana kama una imani.
 
angalia usafi wa mazingira ya nyumbani kwako, je? kuna jalala karibu? kama haukutupa siku hiyo mabaki ya chakula jalalani lazima akufuate dirishani, tena wana sauti za kubembeleza kweli, ilishawahi kunitokea. nakuhakikishia huyo ni paka wa kawaida kama paka wengine.
 
dawa yake ni wewe kutokuchagua silaha ktk vita hii. jambo hili ni dogo mno. 1. tubu dhambi yako. 2. tubu dhambi ya huyo anayelia kama paka hapo kwako. 3.sema maneno machache tu ndiyo haya, "Yahu na akukemee ktk jina la Yeshua" basi. mimi kwangu alikuwa akilia chura kwa sauti zote unazozijua. lakini kama wako wawili huenda wanajiandaa kuongeza ukoo wao. kama mmoja sali.
Goodlucky
 
Boflo hama huko uswahilini.......kama vipi tumia mdudu handsome ndio kiboko yao...ile ni jini proof full....no mauzauza
 
mie mnaijeria mmoja aliniambia,yesu alikufa saa tisa ya mchana,hivyo saa tisa usiku ni saa ya giza ya shetani wengi kama wanawanga ndio wanawanga saa hizo...sijui ni kweli au uongo ila siku hizi hata kama nikiota ndoto mbaya ikiwa ni saa tisa usiku mwenzenu sina amani LOL
 
Kabla ya mambo mengine mi nafikiri kwanza uangalie kama kuna samaki au kitu kinachoweza kumvutia huyo paka ambacho kipo hapo ndani kwani huenda kinamfanya asimame dirishani kwa kuvutiwa na harufu hiyo. Pia nakushauri utumie ujasiri wa kutoka na kwenda kuhakikisha huko nje, wakati mwingine unaweza kusema unasikia sauti za ajabu kumbe ni uoga umekuzidi kwani kama ni jini kwa sifa tunazosikia hana haja ya kusimama dirishani ataingia tu.
 
Atakuwa paka jike yupo kwenye heat na hana paka dume wa kumshuhulikia. Tfuta paka dume ikifika mida hiyo mtoe nnje. watamalizana then hutamsikia tena akipiga myau miau dirishani kwako.

Akirudi tena baada ya kushughulikiwa na dume basi sali sana na umwagie dirisha lako maji ya baraka au chumvi yanapatikana kanisani.

huu ni ushauri wa leornado.
 
Kama unafuga pusi na analala ndani inawezekana mmoja kati ya hao yupo kwa heat sasa anapata sign fulani ila anaashindwa kuingia ndani cha msingi wewe kama pusi yupo ndani ikifika mda wa kulala toa hiyo nje.
 
Ikifika muda huousiwe na woga wewe kuwa na imani na Mungu au kama unadini ingine na ukisikia huyo paka na imani yako ya dini sema unamwaga damu ya yesu, na omba roho mtakatifu akulinde na kutake control

Mara nyingi inakuwa ni wachawi ndio zao na either wanakuwinda kwa kitu unaweza kuanza kuona maisha yako yanabadilika au ufanyalo halieendelei kabisa au kuchukua bahati yako au hata kukuua

Lazima ni nguvu za giza hivyo nakushauri usali usali ndugu yangu as ukienda kwa waganga huwa yanaisha pia. Au pia tafuta kanisa ukiona prophet mwenye kuona atakuambia

Pia maji ya baraka au anointing oil kama unayo weka misalaba kona zote za nyumba utaona baraka na mungu atakuonyesha
Ubarikiwe

Wadau leo ni siku ya 3 mfululizo kila inapofika mida kama tisa ya usiku, katika dirisha ninalolala huwa anakuja paka na kuanza kulia kwa milio ya ajabu sana, sauti huwa anaibadilisha badilisha, inakuwa kama ya mtu mzima mara kama ya mtoto na ya ajabu,.

Kuna jamaa 1 nimemuuliza akaniambia huyo si paka ni jini...wadau eti kuna ukweli wowote? Na nichukue hatua gani
 
Boflo usijekuta unalala na sungura pori chenye kutoa harufu ka shombo ya samaki???? Cz paka anapenda sana samaki.
Otw omba yataisha!
 
Back
Top Bottom