Ni njia gani itumike kuelimisha jamii kuhusu katiba iliyopo wakati tunajiandaa na mp?

Fasta fasta

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
1,126
725
Ndugu wanaJF, ningependa kutoa maoni yangu kuhusu katiba iliyopo. Tunajua ya kuwa baadhi yetu sisi watanzania wengi katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hatuijui pamoja na kwamba kuna wanaoijua na kuichambua kwa kina vizuri sana tunawasifu na tunawaomba waendelee kutuelimisha zaidi na zaidi. Mimi kinachonishangaza ni kwamba unakuta mtu anafanyakazi au anawatumikia watu au watu wanaotumikiwa hawajui sheria zinazowalinda watawaliwa na viongozi wao. Sio kwamba hawa watu hawataki kizielewa ila inawezekana ikachangiwa labda na mazingira, upatikanaji wa hiyo katiba, uvivu, muda wa kuisoma, uelewa na msingi aliyowekewa wakati anasoma hapo mwanzo nk.

Sasa ombi langu kwa serikali, wanasheria, wanaharakati wabunge na watanzania kwa ujumla, Serikali itusaidie jambo hili la kuelimisha kwa kutumia vyombo vya habari kwanza, kama Radio, magazeti, TV na ikiwezekana kuwe na vijarida kutokana na sehemu husika. Tukitoa mfano wa gazeti lichukuliwe ukurasa labda mmoja wa katikati lichapishwe kipengele fulani, Radio na TV wao wanasisitiza tu kwamba leo kuna kipengele fulani kataka magazeti ya leo. Serikali itakapo anza mjadala wa kuelimisha jamii itakuta tayari huyu mtu anawazo kutokana na mazingira yaliyomzunguka, kama ni mkulima, mfanyakazi, mfugaji nk. Hii katiba ni muhimu sana kwa mtu yeyote kuielewa hasa wafanyakazi. Na kama hatutabadilika na kuielewa bado Tanzania yetu itaendelea kurudi nyuma na tutaendelea kuyaeneza madhara yaliyopo sasa hivi. Ninadhani kama 60% au 70% wakianza kuielewa hii katiba hakuna viongozi watakaotusumbua. Tunajua mahakama, polisi, Takukuru hivi ni vyombo vya serikali vilivyoundwa kutekeleza panapokuwa na mazingira ya kuvunja sheria.

Mimi nimetoa ombi hili kwa sababu nchi zinazoendelea wameliwekea msisitizo sana hili jambo. Tusimtafute mchawi wa nchi yetu, mchawi mwenyewe ndio huyu katiba.

Kama kuna mtu anaweza kuliboresha zaidi anakaribishwa ndugu zanguni mkikaa kimya na serikili ndio inazidi kukaa kimya. Ni kwa maslahi ya taifa.

MTANZANIA MWENZENU.:rain:
 
Radio na TV ziandae vipindi vya mahakani kila siku kutokana na makesi yaliyopo ikiwezekana warushe moja kwa moja.
 
(Hii nimepost sijui kama imepotea-narudia) Kuelemisha watu walio juu ni muhimu lakini msingi wa uelewa wa katiba unatakiwa pia uanzie chini kwa watoto ambao wapo shule za msingi na kuendelea. Zamani tulikua na somo la siasa (civics) - huu ni wakati wa kuwafanya watoto wakua na kua allegiance nayo na kuitetea popote---ni watu wengi sana ambao hawafahamu hata nini MAANA ya KATIBA!
 
Back
Top Bottom