Ni njaa tuu inayofanya tuipigie kampeni CCM nyakati za uchaguzi

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,447
630
Mpiga kampeni maarufu wa CCM nyakati za Uchaguzi anaye julikana kwa jina la Mama Ashura wa hapa Temeke Kilikala amesema ni njaa tuu inayowafanya wakipigie kampeni CCM nyakati za uchaguzi, kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akisikikitishwa na upandaji wa bei wa bidhaa muhimu, ndipo alipogeuka na kulaani CCM.

Hali hiyo ilimfanya muuza duka kumuliza" si wewe mwenyewe Mama Ashura wakati wa uchaguzi ulikuwa unakipigia debe kulikoni sasa unalaani" ndipo aliposema kuwa ilikuwa njaa tuu kukipigia kwa vile alikosa kazi ya kufanya ambayo ingempa fedha. Ndipo muuza duka alipomwambia kuwa zile fadha mwenzetu ulichokuwa sasa umerudisha mara mia na kutufanya wote tuteseke.

Nami kwa vile nilikuwa jirani niliaanza kutoa elimu ya uraia kuwa " CCM haina miguu,masikio, mdomo wala mikono kwa wakati ule wa kampeni wewe ulikuwa mikono,miguu, masikio na mdomo wa CCM hivyo na wewe CCM hivyo unapaswa kujilaani mwenyewe"
Mama Ashura alijibu Nimejifunza.

MTAZAMO: CCM INATUMIA UMASKINI WA MTANZANIA KAMA DILI HASI KISIASA, kwa namna nyigine CCM ni rafiki wa UMASKINI, UJINGA na MARADHI.



 
Hilo linajulikana tangu zaman na ndiyo maana hawatoi elimu ya uraia,
Hebu ona upumbavu huu serikali ndoo ina kauli ya mwisho na sio wananchi!
 
Back
Top Bottom