Ni nini tofauti ya speed katika vyombo vya moto

Ili kuelewa swali hili inabidi ukasome Physics ndio utaweza kujibu, au jiulize kidogo tu Kwanini Toyota Alteeza ya mashindano inakimbia zaidi kuliko Alteeza ambayo si ya mashindano
Maswali yako ni ya kitoto. Kwani hujui gari aina moja zinaweza kuwa na injini tofauti?

Mfano kuna Toyota brevis moja ina CC2500 na nyingine 3000
 
Ningependa kujua pikpiki ikiwa speed 100 na gari ikawa speed 100 je hazitaachana zitaenda sawa? Nimeuliza hivyo kwa maana juzi kati nilikuwa nasafiri na gari land cruiser v8 petrol engen yenye speed 180 na kuna mwenzangu na yeye alikuwa na na land cruiser v8 diesel engen yenye speed 220 lakini alishindwa kumkata mwenye speed 180 hii ina maana gani ?
Hiyo 180 km/h na 220km/h hizo ni top speed, unaweza ukamiliki gari wakati wote na usiweze kutembelea top speed, unaweza ukawa unaishia 100, au 120, kwa hiyo hats gari yenye dashboard yenye top speed ya 260 ikawa inaenda Morogoro kwa speed ya 80km/h lazima itapitwa na pikipiki inayokwenda kwa 100km/ h kwa sababu hiyo Mwenye gari kaamua tu kwenda spidi ndogo, kwa hiyo kama nyinyi mlikuwa na landcruisser ya petrol kwa kumaliza zote 180 yawezekana mwenzenu wa mliokuwa mnafuatana alikuwa anatembea 140.
 
Mimi ninavyo jua . Speed ya gari sio lazima uiendeshe max. Speed but. Niongele driving speed iwe ist. Vx spacio. Yutong etc. Basi ikiwa speed 50 itapita ist speed 60 kama upepo. Kwa sababu tai kubwa then 1rotation yake sawa na 1.9 ya ist.hivyo ili iwe na mwendo sawa katika speed sawa lazima same type kama za msafara. Nawakilisha
Kama yutong inaenda max speed ya 50 na ist inaenda 60 ist haitapitwa,hivyo ni vipimo standard, ni Sawa na MTU kusema kilo moja ya mawe ni nzito kuliko kilo moja ya pamba. Speed meter ni instrument iliyotengezwa kwa umakini sana wazungu hawabahatishi,kama unavyoona mizani, rula, saa nk, labda tu hiyo instrument ipate matatizo ya kiufundi inaweza kusoma tofauti.ndiyo maana hata tochi za trafiki ziko standard.si kwa gari dogo wala kubwa.
 
Mwepesi kufeli! Hivi unadhani kwanini speed signs za barabarani zimekuwa aina moja kwa vyombo vyote!?

Speed 100 kwenye dashboard ni lazima iwe sawa na mwendo kasi wa barabarani, bila kujali ni chombo gani!
Well said
 
Tofauti ya gari moja na nyingine haiko kwenye speed kama ambavyo unaiona kwenye dash board, bali iko kwenye vitu hivi vikubwa viwili:
Acceleration (Horse Power) na Torque (Uwezo wa kuvuta mzigo/Tela nk).
Gari nyingi za Petrol zina Horse Power nyingi hivyo kuwa na acceleration kubwa lakini pia zina Torque ndogo.
Yani unaweza ukakuta gari Mathalani GX mia ina Horse power (Uwezo wa Farasi 150) Lakini ukiweka ivute tela ya tani moja gari itashindwa kuondoka na huenda ikazimika). Lakini unakuta gari ya diesel mathalani Fuso ina Uwezo huo huo wa Farasi 150 lakini ukiiwekea ivute tela la tani moja italivuta kama mchezo na hata unaweza ukaondokea kwa gia namba tatu.

Ikija kwenye acceleration:
Ukiishindanisha GX mia na Fuso, GX mia itachomoka kama manyoya na itachukua sekunde chache (say 13 seconds) mpaka kufikia mathalani Speed 100 na wakati Fuso hilo hilo linaweza likachukua sekunde ishirini mpaka kufikia speed 100.

Tofauti ya hizo V8 mbili iko hapo...
V8 ya Petrol inachukua sekunde chache zaidi kuchanganya ukilinganisha na hiyo ya Diesel. Yani kama mmeondoka wote mkiwa na Initial velocity (Speed) Uo =0Km/hr na baada ya sekunde 6 ukapima final velociy Uv, utagundua kuwa ile gari ya Petrol ina uwezo mkubwa wa kuunguza mafuta na kubadili nishati ya mafuta kuwa nishati ya mwendo kuliko nishati a Diesel. Mafuta ya Diesel hayaungui haraka kama Petrol na ndio maana gari nyingi za Diesel zinafungwa kifaa kinachoitwa Turbo. Kifaa hichi husaidia kujaza hewa kwenye injini ili kuchochea combustion (moto) katika engine.
Moja ya kitu kinachosababisha diesel iwe na uwezo mkubwa ni kwa vile Diesel inaungua taratibu na inaungua katika joto kali zaidi kuliko Petrol. Kwa hiyo compresiion ratio ya hewa kwenye cylinder ya engine ya Diesel inaweza kuwa 1:10 wakati ile ya Petrol inaweza kuwa 1:7... Yani hii inamaanisha japo diesel inaungua taratibu, ule mgandamizo wa hewa unaweza kuwa mara kumi zaidi ukilinganishwa na hewa iliyoingia kwenye cylinder wakati ile ya Petrol inaweza kuwa na mgandamizo mara saba zaidi... Mngandamizo unapokuwa mkubwa ina maana kuwa lile pigo la cylinder kuizungusha cranck shafti linakuwa ni la nguvu zaidi.

Hapa ni kama vile katoto kadogo kaje kwa nguvu kakuzabe kofi moja alafu Mike Tyson akupige 'kikofi cha mahaba'. Kofi la nguvu la kale katoto kadogo linaweza likakuacha unatabasamu na wakati kofi moja dogo la Tyson linaweza kukufanya upelekwe hosiptali.
Kwa hiyo pigo moja la engine ya petrol ni sawa nakofi la katoto... Kana nguvu nyingi na kanaweza kakakimbia haraka kuja kukuzaba kofi lakini kofi lake halina nguvu sana. Diesel ni kama Tyson, ana nguvu kidogo ya kukimbia kuja kukuzaba kofi lakini akikupiga kofi lake dogo lina kuwa na nguvu nyingi sana.

Hivyo basi utaona mafuta ya Petrol yakitumika kwenye magari madogo na wakati mafuta ya Diesel yakitumiwa kwenye magari makubwa ambayo yanabeba mizigo mizito hata ya tani thelasini, kwenye engine za meli na hata treni...

Wamarekani kutokana na utajiri wao wanapenda wapate vyote.. Horse power na Torque.. Ndio masna utakuta magari ya Mmarekani yanatumia injini za Petrol na yana injini kubwa kama gari za Diesel.. Gari ya Petrol ya Mjapani yenye cc 2000 (rav 4) mmarekani ametengeneza gari kama hiyo na kuiwekea injini ya Petrol ya cc 4,000 (Jeep Cherokee)!
Ahsante kwa jibu zuri sana mkuu
 
Basi wewe ndio haujaelewa swali langu vizuri nilianza kweli kuuliza hivyo niaelezea japo na mie naelewa kama hivyo ila kilichokuwa kinanichanganya ni kuhusu v8 ya petrol yenye speed 180 na v8 ya diesel yenye speed 220/kushindwa kuipita ya petrol japo yenyewe odo inasoma 220 soma vizuri swali utaelewa na ndio maana Kodofan amelielezea kwa kirefu
 
Tofauti ya gari moja na nyingine haiko kwenye speed kama ambavyo unaiona kwenye dash board, bali iko kwenye vitu hivi vikubwa viwili:
Acceleration (Horse Power) na Torque (Uwezo wa kuvuta mzigo/Tela nk).
Gari nyingi za Petrol zina Horse Power nyingi hivyo kuwa na acceleration kubwa lakini pia zina Torque ndogo.
Yani unaweza ukakuta gari Mathalani GX mia ina Horse power (Uwezo wa Farasi 150) Lakini ukiweka ivute tela ya tani moja gari itashindwa kuondoka na huenda ikazimika). Lakini unakuta gari ya diesel mathalani Fuso ina Uwezo huo huo wa Farasi 150 lakini ukiiwekea ivute tela la tani moja italivuta kama mchezo na hata unaweza ukaondokea kwa gia namba tatu.

Ikija kwenye acceleration:
Ukiishindanisha GX mia na Fuso, GX mia itachomoka kama manyoya na itachukua sekunde chache (say 13 seconds) mpaka kufikia mathalani Speed 100 na wakati Fuso hilo hilo linaweza likachukua sekunde ishirini mpaka kufikia speed 100.

Tofauti ya hizo V8 mbili iko hapo...
V8 ya Petrol inachukua sekunde chache zaidi kuchanganya ukilinganisha na hiyo ya Diesel. Yani kama mmeondoka wote mkiwa na Initial velocity (Speed) Uo =0Km/hr na baada ya sekunde 6 ukapima final velociy Uv, utagundua kuwa ile gari ya Petrol ina uwezo mkubwa wa kuunguza mafuta na kubadili nishati ya mafuta kuwa nishati ya mwendo kuliko nishati a Diesel. Mafuta ya Diesel hayaungui haraka kama Petrol na ndio maana gari nyingi za Diesel zinafungwa kifaa kinachoitwa Turbo. Kifaa hichi husaidia kujaza hewa kwenye injini ili kuchochea combustion (moto) katika engine.
Moja ya kitu kinachosababisha diesel iwe na uwezo mkubwa ni kwa vile Diesel inaungua taratibu na inaungua katika joto kali zaidi kuliko Petrol. Kwa hiyo compresiion ratio ya hewa kwenye cylinder ya engine ya Diesel inaweza kuwa 1:10 wakati ile ya Petrol inaweza kuwa 1:7... Yani hii inamaanisha japo diesel inaungua taratibu, ule mgandamizo wa hewa unaweza kuwa mara kumi zaidi ukilinganishwa na hewa iliyoingia kwenye cylinder wakati ile ya Petrol inaweza kuwa na mgandamizo mara saba zaidi... Mngandamizo unapokuwa mkubwa ina maana kuwa lile pigo la cylinder kuizungusha cranck shafti linakuwa ni la nguvu zaidi.

Hapa ni kama vile katoto kadogo kaje kwa nguvu kakuzabe kofi moja alafu Mike Tyson akupige 'kikofi cha mahaba'. Kofi la nguvu la kale katoto kadogo linaweza likakuacha unatabasamu na wakati kofi moja dogo la Tyson linaweza kukufanya upelekwe hosiptali.
Kwa hiyo pigo moja la engine ya petrol ni sawa nakofi la katoto... Kana nguvu nyingi na kanaweza kakakimbia haraka kuja kukuzaba kofi lakini kofi lake halina nguvu sana. Diesel ni kama Tyson, ana nguvu kidogo ya kukimbia kuja kukuzaba kofi lakini akikupiga kofi lake dogo lina kuwa na nguvu nyingi sana.

Hivyo basi utaona mafuta ya Petrol yakitumika kwenye magari madogo na wakati mafuta ya Diesel yakitumiwa kwenye magari makubwa ambayo yanabeba mizigo mizito hata ya tani thelasini, kwenye engine za meli na hata treni...

Wamarekani kutokana na utajiri wao wanapenda wapate vyote.. Horse power na Torque.. Ndio masna utakuta magari ya Mmarekani yanatumia injini za Petrol na yana injini kubwa kama gari za Diesel.. Gari ya Petrol ya Mjapani yenye cc 2000 (rav 4) mmarekani ametengeneza gari kama hiyo na kuiwekea injini ya Petrol ya cc 4,000 (Jeep Cherokee)!
Mkuu umefafanua vzr sana... Ila hapo kwenye 2000cc za mjapan na 4000cc za mmarekani... Hiyo ingine ya 4000cc tena ya petrol mafuta yake si ni balaa..
 
Hapana.. Unajua injini inapokuwa kubwa inakuwa inazunguka kidogo kidogo lakini mwendo unakuwa mkali.. Kama wewe ni wa cku nyingi utakumbuka kulikuwa na Phoenix za 'jembe kubwa na jembe dogo'. Phoenix ya Jembe kubwa unanyonga kidogo lakini inatoka nduki balaa na wakati ile ya jembe dogo unanyonga sana ila haikimbii na badala yake unaweza ukapakia gunia tatu za mkaa na bado ukapandisha mlima bila kusimamia.
 
Big up Mkuu kwa swali nzuri,Pikipiki ikiwa kwenye speed 100 na gari ikawa kwenye hiyo hiyo speed hazitaenda sawa zitaachana either gar au pikipiki itakuwa mbele.Kuhusu gari aina ya land cruiser v8 petrol engine speed 180 na land cruiser v8 diesel engine speed 220 hapo mkuu inawezekana hiyo cruser inayotumia diasel ina tatizo kwa sababu hizo gari zote engine zina cylinder 8(v8) ila tofauti ipo kwenye fuel (petrol light fuel &diesel heavy fuel)vilevile kwa speed ya 220(land cruser v8 diesel engine) itakuwa imemzidi power(Hp) hiyo land cruiser v8 petrol engine, nahisi shape ziko sawa .......Kwann ameshindwa kukupita inawezekana anajua hali ya gari lake haliko vizuri,ameogopa kwenda na speed kali.
 
Back
Top Bottom