Ni nini tofauti ya speed katika vyombo vya moto

The Transporter

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
3,391
6,629
Ningependa kujua pikpiki ikiwa speed 100 na gari ikawa speed 100 je hazitaachana zitaenda sawa? Nimeuliza hivyo kwa maana juzi kati nilikuwa nasafiri na gari land cruiser v8 petrol engen yenye speed 180 na kuna mwenzangu na yeye alikuwa na na land cruiser v8 diesel engen yenye speed 220 lakini alishindwa kumkata mwenye speed 180 hii ina maana gani ?
 
Nadhani perfomance za engine ni tofauti. Gari zinaweza kuwa zote ni speed 180 lakini perfomance za engine zikawa tofauti.
Ngoja waje mafundi kukupa majibu sahihi
 
Gari inaweza kuwa Na speed 220 lakini Dereva akawa anaendesha Kwa 120km/hr...

Wakati huo huo gari yenye speed mwisho 180 Dereva akawa anaendesha Kwa 140km/hr.

Hapo lazima anayetembea Kwa 140km/hr atakuwa mbele tu hata kama gari yake ina limit ya 180 against 220 ya mwenzake.
 
Ninachokwambia Huyu mwenzangu wote kulikuwa safari moja na alikuwa anataka kunipita ila alichemka na sio kwamba gari yake mbovu na ndio maana nikaanza kwa kuuliza speed 100 ya Pikipiki ni sawa na speed 100/ya gari
 
Barraza naona amejibu vema kwa mujibu Wa swali lako! Lkn nafikiri maana halisi uliyokuwa unafikiria ni kwamba gari iko speed 100 kph ikapitwa na gari ambayo iko ktk speed 90kph INAKUWAJE HAPO? Kama itakua niko sahihi utanijuza! Hapo ndipo nitakapotoa maoni yangu kwamba ni VIPI?
 
Hii akili au matope, hata kama gari ina speed 500 na nyingine ina speed 100 wa mia atakuwa mbele kama atakimbia spidi 80 na wa 500 akikimbia spidi 50 wa 500 ataachwa mbali sana.
Ninachokwambia Huyu mwenzangu wote kulikuwa safari moja na alikuwa anataka kunipita ila alichemka na sio kwamba gari yake mbovu na ndio maana nikaanza kwa kuuliza speed 100 ya Pikipiki ni sawa na speed 100/ya gari
 
Kwanza tujue speed ni nin.??

Speed ni ratio ya umbali kwa muda, yaan umbali gawanya kwa muda.

Speed inaongelea katika muda wa lisaa moja ametembea umbali gani?

Kama mtu speed yake ni 140km/hr . maana yake katika kila saa moja anatembea kilomita 140,

Hivi vipimo ni vya kimataifa.

Kama wote wata acerelate na kufikia speed moja na waka mantain hiyo speed hadi mwisho basi watatembea sawa
 
Ila kwa pikpik na gari haziwezi kuwa sawa kwani pikpik ni nyepesi kuliko gari! Kwa hiyo kuna wakati itakuwa inagusa kidogo ardhi na kupaa juu! Lkn gari kwa 7bu ni zito nguvu nyingi zitakuwa chini ktk kukanyaga ardhi! Kwa hiyo gari itakuwa mbele ya pikpik japo zote zinasoma speed 100kph kwa wakati huo zinapotembea!
 
Mi siyo mtaalamu saana..ila kwa uelewa wangu ni kwamba kuna factor nyingi zinaweza sababisha mwendo wa gari kupungua..ikiwemo performance ya engine..aina ya body ya gari...uzito wa gari...na aina ya matairi (to mention a few)
Performance ya engine inaweza ikaathiri uwezo wa gari kutembea..vitu kama friction between vyuma n.k ...huweza kulifanya gari lisitembee vizuri..
Uzito wa gari...huweza kuadhiri mwendo wa gari kwa maana ya kwamba gari ikiwa na uzito uliobalance mwendo wake unaweza kuwa mkubwa kuliko gari jepesi kutokana na ukinzani wa upepo pamoja na friction between matairi na ardhi (matairi kukamata ardhi).nafikiri ndiyo maana mabasi huwa yanayembea sana kuliko gari ndogo tho they have the same speed...
Aina ya matairi huweza kuchangia mwendo wa gari...hapa tunaongelea perfomance tairi pana na tairi nyembamba kwenye lami na kwenye vumbi..kwa ambao mmesha experience gari ikiwa na tairi pana sana kwenye lami inakosa mwwndo ukilinganisha na gari hyo hyo ikiwekewa tairi nyembamba..
Uwezo wa dereva...wakati mwingine experience ya dereva huwa inamata kwenye hayo mavitu...
 
Mimi ninavyo jua . Speed ya gari sio lazima uiendeshe max. Speed but. Niongele driving speed iwe ist. Vx spacio. Yutong etc. Basi ikiwa speed 50 itapita ist speed 60 kama upepo. Kwa sababu tai kubwa then 1rotation yake sawa na 1.9 ya ist.hivyo ili iwe na mwendo sawa katika speed sawa lazima same type kama za msafara. Nawakilisha
 
Tofauti ya gari moja na nyingine haiko kwenye speed kama ambavyo unaiona kwenye dash board, bali iko kwenye vitu hivi vikubwa viwili:
Acceleration (Horse Power) na Torque (Uwezo wa kuvuta mzigo/Tela nk).
Gari nyingi za Petrol zina Horse Power nyingi hivyo kuwa na acceleration kubwa lakini pia zina Torque ndogo.
Yani unaweza ukakuta gari Mathalani GX mia ina Horse power (Uwezo wa Farasi 150) Lakini ukiweka ivute tela ya tani moja gari itashindwa kuondoka na huenda ikazimika). Lakini unakuta gari ya diesel mathalani Fuso ina Uwezo huo huo wa Farasi 150 lakini ukiiwekea ivute tela la tani moja italivuta kama mchezo na hata unaweza ukaondokea kwa gia namba tatu.

Ikija kwenye acceleration:
Ukiishindanisha GX mia na Fuso, GX mia itachomoka kama manyoya na itachukua sekunde chache (say 13 seconds) mpaka kufikia mathalani Speed 100 na wakati Fuso hilo hilo linaweza likachukua sekunde ishirini mpaka kufikia speed 100.

Tofauti ya hizo V8 mbili iko hapo...
V8 ya Petrol inachukua sekunde chache zaidi kuchanganya ukilinganisha na hiyo ya Diesel. Yani kama mmeondoka wote mkiwa na Initial velocity (Speed) Uo =0Km/hr na baada ya sekunde 6 ukapima final velociy Uv, utagundua kuwa ile gari ya Petrol ina uwezo mkubwa wa kuunguza mafuta na kubadili nishati ya mafuta kuwa nishati ya mwendo kuliko nishati a Diesel. Mafuta ya Diesel hayaungui haraka kama Petrol na ndio maana gari nyingi za Diesel zinafungwa kifaa kinachoitwa Turbo. Kifaa hichi husaidia kujaza hewa kwenye injini ili kuchochea combustion (moto) katika engine.
Moja ya kitu kinachosababisha diesel iwe na uwezo mkubwa ni kwa vile Diesel inaungua taratibu na inaungua katika joto kali zaidi kuliko Petrol. Kwa hiyo compresiion ratio ya hewa kwenye cylinder ya engine ya Diesel inaweza kuwa 1:10 wakati ile ya Petrol inaweza kuwa 1:7... Yani hii inamaanisha japo diesel inaungua taratibu, ule mgandamizo wa hewa unaweza kuwa mara kumi zaidi ukilinganishwa na hewa iliyoingia kwenye cylinder wakati ile ya Petrol inaweza kuwa na mgandamizo mara saba zaidi... Mngandamizo unapokuwa mkubwa ina maana kuwa lile pigo la cylinder kuizungusha cranck shafti linakuwa ni la nguvu zaidi.

Hapa ni kama vile katoto kadogo kaje kwa nguvu kakuzabe kofi moja alafu Mike Tyson akupige 'kikofi cha mahaba'. Kofi la nguvu la kale katoto kadogo linaweza likakuacha unatabasamu na wakati kofi moja dogo la Tyson linaweza kukufanya upelekwe hosiptali.
Kwa hiyo pigo moja la engine ya petrol ni sawa nakofi la katoto... Kana nguvu nyingi na kanaweza kakakimbia haraka kuja kukuzaba kofi lakini kofi lake halina nguvu sana. Diesel ni kama Tyson, ana nguvu kidogo ya kukimbia kuja kukuzaba kofi lakini akikupiga kofi lake dogo lina kuwa na nguvu nyingi sana.

Hivyo basi utaona mafuta ya Petrol yakitumika kwenye magari madogo na wakati mafuta ya Diesel yakitumiwa kwenye magari makubwa ambayo yanabeba mizigo mizito hata ya tani thelasini, kwenye engine za meli na hata treni...

Wamarekani kutokana na utajiri wao wanapenda wapate vyote.. Horse power na Torque.. Ndio masna utakuta magari ya Mmarekani yanatumia injini za Petrol na yana injini kubwa kama gari za Diesel.. Gari ya Petrol ya Mjapani yenye cc 2000 (rav 4) mmarekani ametengeneza gari kama hiyo na kuiwekea injini ya Petrol ya cc 4,000 (Jeep Cherokee)!
 
Barraza naona amejibu vema kwa mujibu Wa swali lako! Lkn nafikiri maana halisi uliyokuwa unafikiria ni kwamba gari iko speed 100 kph ikapitwa na gari ambayo iko ktk speed 90kph INAKUWAJE HAPO? Kama itakua niko sahihi utanijuza! Hapo ndipo nitakapotoa maoni yangu kwamba ni VIPI?
Unapotosha maana halisi ya mada, 100kph na 90 kph logical n practically mwenye 100kph atakuwa speed zaid
 
Tofauti ya gari moja na nyingine haiko kwenye speed kama ambavyo unaiona kwenye dash board, bali iko kwenye vitu hivi vikubwa viwili:
Acceleration (Horse Power) na Torque (Uwezo wa kuvuta mzigo/Tela nk).
Gari nyingi za Petrol zina Horse Power nyingi hivyo kuwa na acceleration kubwa lakini pia zina Torque ndogo.
Yani unaweza ukakuta gari Mathalani GX mia ina Horse power (Uwezo wa Farasi 150) Lakini ukiweka ivute tela ya tani moja gari itashindwa kuondoka na huenda ikazimika). Lakini unakuta gari ya diesel mathalani Fuso ina Uwezo huo huo wa Farasi 150 lakini ukiiwekea ivute tela la tani moja italivuta kama mchezo na hata unaweza ukaondokea kwa gia namba tatu.

Ikija kwenye acceleration:
Ukiishindanisha GX mia na Fuso, GX mia itachomoka kama manyoya na itachukua sekunde chache (say 13 seconds) mpaka kufikia mathalani Speed 100 na wakati Fuso hilo hilo linaweza likachukua sekunde ishirini mpaka kufikia speed 100.

Tofauti ya hizo V8 mbili iko hapo...
V8 ya Petrol inachukua sekunde chache zaidi kuchanganya ukilinganisha na hiyo ya Diesel. Yani kama mmeondoka wote mkiwa na Initial velocity (Speed) Uo =0Km/hr na baada ya sekunde 6 ukapima final velociy Uv, utagundua kuwa ile gari ya Petrol ina uwezo mkubwa wa kuunguza mafuta na kubadili nishati ya mafuta kuwa nishati ya mwendo kuliko nishati a Diesel. Mafuta ya Diesel hayaungui haraka kama Petrol na ndio maana gari nyingi za Diesel zinafungwa kifaa kinachoitwa Turbo. Kifaa hichi husaidia kujaza hewa kwenye injini ili kuchochea combustion (moto) katika engine.
Moja ya kitu kinachosababisha diesel iwe na uwezo mkubwa ni kwa vile Diesel inaungua taratibu na inaungua katika joto kali zaidi kuliko Petrol. Kwa hiyo compresiion ratio ya hewa kwenye cylinder ya engine ya Diesel inaweza kuwa 1:10 wakati ile ya Petrol inaweza kuwa 1:7... Yani hii inamaanisha japo diesel inaungua taratibu, ule mgandamizo wa hewa unaweza kuwa mara kumi zaidi ukilinganishwa na hewa iliyoingia kwenye cylinder wakati ile ya Petrol inaweza kuwa na mgandamizo mara saba zaidi... Mngandamizo unapokuwa mkubwa ina maana kuwa lile pigo la cylinder kuizungusha cranck shafti linakuwa ni la nguvu zaidi.

Hapa ni kama vile katoto kadogo kaje kwa nguvu kakuzabe kofi moja alafu Mike Tyson akupige 'kikofi cha mahaba'. Kofi la nguvu la kale katoto kadogo linaweza likakuacha unatabasamu na wakati kofi moja dogo la Tyson linaweza kukufanya upelekwe hosiptali.
Kwa hiyo pigo moja la engine ya petrol ni sawa nakofi la katoto... Kana nguvu nyingi na kanaweza kakakimbia haraka kuja kukuzaba kofi lakini kofi lake halina nguvu sana. Diesel ni kama Tyson, ana nguvu kidogo ya kukimbia kuja kukuzaba kofi lakini akikupiga kofi lake dogo lina kuwa na nguvu nyingi sana.

Hivyo basi utaona mafuta ya Petrol yakitumika kwenye magari madogo na wakati mafuta ya Diesel yakitumiwa kwenye magari makubwa ambayo yanabeba mizigo mizito hata ya tani thelasini, kwenye engine za meli na hata treni...
Perfect answer....
 
Ningependa kujua pikpiki ikiwa speed 100 na gari ikawa speed 100 je hazitaachana zitaenda sawa? Nimeuliza hivyo kwa maana juzi kati nilikuwa nasafiri na gari land cruiser v8 petrol engen yenye speed 180 na kuna mwenzangu na yeye alikuwa na na land cruiser v8 diesel engen yenye speed 220 lakini alishindwa kumkata mwenye speed 180 hii ina maana gani ?
Kilo moja ya pamba na kilo moja ya mawe ipi nzito?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom