Ni Nini Mantiki ya Sherehe za CCM 2012 Kama si kuhangaika na Upinzani?

Profesa

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
905
624
Kama Ni miaka ni 35, Haiji kichwani! Ni nini Jubilee gani hii...
Kama ni Watu mablimbali maarufu wa Chama simuoni yeyote anaehusiana na tukio hili!
Ni moja tu, Publicity against Upinzani (Kujitangaza dhidi ya upinzani)
Nakumbuka sherehe za miaka iliyopita zilitusumbua sana kupata fedha na hazikunguruma ki hivi.
Kwanza hongereni kwa mkakati huu, itawaweka mahali fulani pazuri kwa wengi wa Watanzania.
Kwa maoni yangu ni Wastage ya resources (Matumizi Mabaya ya rasilimali), mngeweza kuwa na mkakati mzuri zaidi kuelekea shughuli hii, katika kuelezea mazurio na mipango kabambe ya CCM (sio sisasa za baadhi ya viongozi wenu za kizembe, majungu, vijembe, fitina, kubeza) mikakati inayoonyesha busara na upeo wenu na mrengo mnaosimamia, huku mkiimarisha matawi na kuwa positive on your own side bila kuangalia vijembe vya upinzani na vurugu zao (ambazo wengi mmeingia mkenge na kuanza kuconsentrate huko badala ya kusimamia busara za CCM).

Kumbukeni Obama hakushinda kwa sababu ni Mweusi, alishinda kwa sababu Umma ulitizama ukaona hekima na Busara za hali ya juu kabisa haijapata kutokea, kampeni bila kujibu ubaya, majungu au kupanic kwa aajili ya kashfa za upinzani lah! Bali kwa kuangalia hoja iliyopo mbele bila kufanya reference kwa hoja tata na za uchochezi za upinzani. Kusimamia habari njema kwa watu waliokata tamaa na mipango kabambe ya kuwakwamua katika maisha, kwa kusimamia sera ya uchumi wa kijamaa, uzalishaji unaokidhi haja, na kuweza kujitegemea badala ya kuwa tegemezi.
Viongozi mkiwa na positive thinking na kuangalia kutoka kwenye mafanikio na mipango chanya iliyopo, na kuachana na kupambana na upinza kwa mbinu za "Kiswahili" hakika uhai wa Chama utarudi.
Natamani kauna CCM iliyokuwa na watu wenye hotuba kemkema na kusisimmua kama Muasisi wenu, akizungumzia yanayojiri ulimwengunia na tunavyojizatiti kuendelea, yanayojiri kijijini, mijini na jinsi ya kujiimarisha kimaendeleo. Badala ya kuhangaika na matusi ya upinzani. Waacheni wananchi wapime.
Na mnaomwandikia Hotuba Mwenyekiti Taifa zingatieni haya, wekeni vionjo vya kimapinduzi maana chama kinaonekana sicho kile tulichokijua. Misemu ya kuhamasisha, kusisimua, kuinua harakati na kuzungumzia taifa sio sisi CCM na wao sijui akina nani...
 
Back
Top Bottom