Ni nini kilichomuondoa Ezekiel Kamwaga Mwanahalisi?

mudavadi

Member
Apr 19, 2011
53
14
Ezekiel Kamwaga. Ni yule mwandishi mahiri wa gazeti la Mwanahalisi ambaye hapa majuzi imeripotiwa kwamba ameajiriwa kama Afisa Habari wa Klabu ya Simba. Mwandishi huyu amesitisha ajira yake katika Gazeti hili huku kukiwa na maswali juu ya sababu halisi za kuondoka kwake. Wako wanaomshutumu Kubenea kwa kujenga mazingira ya kuondoka kwa Kamwaga lakini kuna wale ambao wanadai Kamwaga alikuwa ameshaanza 'kuchafuliwa'.

Je, kilichomuondoa Kamwaga Mwanahalisi ni nini?
 
Nafikiri sababu ni kupata ajira Simba kama afisa habari.
Simba walimwondoa Ndimbo, pamoja na mengine, ni kwa kuwa alikuwa afisa habari Simba na anafanya kazi kwenye radio station, hivyo Kamwaga lazima aachie Mwanahalisi kama amekubali kuwa mwajiriwa wa Simba.
Hizi sababu nyingine unazozitafuta zaweza kuwa majungu.
 
Ezekiel Kamwaga. Ni yule mwandishi mahiri wa gazeti la Mwanahalisi ambaye hapa majuzi imeripotiwa kwamba ameajiriwa kama Afisa Habari wa Klabu ya Simba. Mwandishi huyu amesitisha ajira yake katika Gazeti hili huku kukiwa na maswali juu ya sababu halisi za kuondoka kwake. Wako wanaomshutumu Kubenea kwa kujenga mazingira ya kuondoka kwa Kamwaga lakini kuna wale ambao wanadai Kamwaga alikuwa ameshaanza 'kuchafuliwa'.Je, kilichomuondoa Kamwaga Mwanahalisi ni nini?
Usitushirikishe katika majungu staili yako!
 
Free movement of labour in search of green pastures. nadhani hakuna tatizo. zingine ni hisia zako tu unless una some more facts
 
Kamwaga na Kubenea si wapo hapa JF? kwa nini asijibu mwenyewe hili suala badala ya kuanza speculation zisizokuwa na maana.
 
Mie nilidhani tutamjadilii mtu kwa maslahi ya Nchi ? Mie hata kumjua simjui sasa leo nitafute sababu za kazi gani ? Je kuondoka kwake kumeathiri kumletea Mtanzania masikini maisha bora ? Kama hapana basi tuachane naye tusijaze nafasi bure hapa .
 
His Good perfomance during the interviwe with Simba SC, akachaguliwa kuwa ndio kilichomwondoa. Full stop.
 
Lakinui baada ya majibu ya kudhalilisha yaliyotolewa na rage baada ya Ndimbo kuachia ngazi, sikutarajia waandishi waende huko tena... yakimkuta ya kumkuta huyo Kamwaga asimlalamikie mtu
 
Mwanzisha thread ni mzushi!! Inaelekea wazi sababu anazijua. Si atuambie tu??
 
Simple, Kamwaga ni anakula Kitimoto, Kubenea ni hali kabisa.

Huu sasa utata. Mimi nafikiri mtu mpaka anauliza swali, basi inawezekana exit ya Kamwaga ni zaidi ya kupata ajira Simba. Wanaomfahamu Kubenea watusaidie kumpata tujue maana Kamwaga alikuwa na mchango wake kutokana na uandishi wake mahiri.
 
Taariza zilizopo ni kwamba Kamwaga alikuwa nakwenda kukutana na mmoja wa watoto wa mapacha watatu na kuchukua mshiko kutoka kwao in return for leaking of secrets of that relate to Mwanahalisi's conduct of business. Jamaa aliposhtukiwa aliambiwa ajiondoe mara moja au afukuzwe kwa aibu. Akaomba apewe mwezi mmoja ili atafute ajira, ndipo akapata ajira ya Simba baada ya intense lobbying.
 
Ezekiel Kamwaga. Ni yule mwandishi mahiri wa gazeti la Mwanahalisi ambaye hapa majuzi imeripotiwa kwamba ameajiriwa kama Afisa Habari wa Klabu ya Simba. Mwandishi huyu amesitisha ajira yake katika Gazeti hili huku kukiwa na maswali juu ya sababu halisi za kuondoka kwake. Wako wanaomshutumu Kubenea kwa kujenga mazingira ya kuondoka kwa Kamwaga lakini kuna wale ambao wanadai Kamwaga alikuwa ameshaanza 'kuchafuliwa'.

Je, kilichomuondoa Kamwaga Mwanahalisi ni nini?

Tatizo la watu wambea huwa wanadhani wengine nao ni wambea kama wao. Yeye mwenyewe ameshatuambia kuwa huyo Kamwaga amepata ajira mpya huko Simba sasa unauliza ili upatiwe jibu gani? Pia kwenye red hapo ndo panaonyesha umbea wa huyu bwana. Kama kuna kitu unataka tukijue kuhusiana na Mwanahalisi basi utuambie kuliko kutupotezea muda wetu.

Naungana na mwanajamvi mmoja aliyesema kuwa kuondoka kwake kuna tija gani kwa watanzania? Tujitahidi kuweka thread zenye maana wanajamvi!
 
Back
Top Bottom