Ni ndugu wapi ambao hawaruhusiwi Kuoana?

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Nadhani katika Ulimwengu mzima hakuna watu wanaooana Kaka na Dada na sababu kuu ambayo imekuwa ikielezwa ni ya kibayolojia kwamba iwapo kuna udhaifu katika kizazi hicho, wakioana udhaifu huo utazidi zaidi.

Kwa Waafrika Weusi zuio hilo linaenda hadi kwa watoto wa Baba na mama wadogo, Wajomba na Shangazi n.k. Lakini kwa wenzetu Waarabu huko ni ruksa. naweka hoja zifuatazo kwa ajili ya mjadala:
1) Katika ulimwengu wa sasa ambao tumechanganyikana ni upi ukomo wa ndugu kuoana, au kwa lugha nyingine, ni ndugu yupi ambaye haifai kuoana naye?
2) Ukomo huo uko kisheria au ni kimila?
 
Kwa sharia ya dini ya Kiislamu, ndugu wa tumbo moja baba na mama (Baba na Mama huyo huyo), ndugu kwa baba (Watoto wa Baba kwa Mama wa kambo) au ndugu kwa mama ( Watoto wa Mama kwa Baba wa kambo). Hao ndio ndugu wasioruhusiwa kuoana.

Ama mtoto wa Baba Mkubwa au Baba Mdogo Ruksa. Mtoto wa Mama Mkubwa au Mama Mdogo Ruksa na Mtoto wa Mjomba au Shangazi wote hao ni Ruksa. Haya ni kwa mafundisho ya dini ya Kiislamu.

Sijui mafundisho ya Dini nyenginezo kama Wakristo, Baniani na wengineo. Hali kadhalika kuna sheria za Kimila ambazo hukatazana japo dini kuhalalisha.
 
Kwa waIslam, awe wa kontinenti, taifa, nchi, rangi au kabila lolote lile muongozo wa wepi wanaofaa kuoana tunaupata katika Qur'an kama ifatavyo:

Q. 4:23. Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu. (Pia mmeharimishwa) wake wa watoto wenu walio toka katika migongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili isipo kuwa yale yaliyo kwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

Natumai ni crystal clear.
 
Ndugu kuoana ni mbaya lakini vipi kwa wale wasiojuana kama ni ndugu?

Kuna dada kaoana n akaka yake waliyeshangia baba bila kujuana maana mama zao walipata mimba halafu wakaolewa na watu wengine na mimba hizo zikawa za wababa waliowaoa yani waliwabambika watu wengine, walivyokuwa wakubwa, hao watoto wamepisha na miaka saba yaani mvulana kamzidi msichan miaka saba sasa walivyooana, mama zao kila mmoja kwa wakati wake akaamua kumwambia mwanae ukweli kwamba huyu siyo baba yako kila mmoja bila kujuana akamweleza mwanae ukweli na akampa maelekezo mahali baba yake alipo na jina, wakafunga safari mpaka hicho kijiji wakaenda kwanza kumtafuta baba wa msichana kufika yule msichana alishtuka yani huyo baba na mume wake wamefanana utafikiri mapacha mume wake ana kovu usoni na huyo baba analo, bai wakakribishwa yule dada akajieleza akamtambulisha mume wake sasa yule mwanaume akashangaa majina ya baba zao yanafanana si ikabidi na yeye ajieleze baba yao akawaomba msamaha akasema endeleeni tu maana mmeishafunga ndo na mlikuwa hamjuani sisi ndo wenye makosa.
sasa hapo kuna makosa kweli? na wale wamama walivyojua wakawaambia watoto wanyamaze maana wakisema ndoa zao zitavunjika kwa hiyo wanaendelea.
 
Swala la kuoa au la kuolewa linaambatana na swala la tendo la ndoa (SEX) hapa Biblia ina sema hivi.Levictus 18:7-20;
" Do not dishonor your father by having sexual relationith your own mother, your fathers wife for those polygamists,Do not have sexual relation with your sister,either your fathers daughter,whether born in the same house or else where. Your son's daughter oryour daughter's daughter.Your father's sister,your mother's sister, and many more read the entire verses.
 
Swala la kuoa au la kuolewa linaambatana na swala la tendo la ndoa (SEX) hapa Biblia ina sema hivi.Levictus 18:7-20;
" Do not dishonor your father by having sexual relations with your own mother, your fathers wife for those polygamists,Do not have sexual relation with your sister,either your fathers daughter,whether born in the same house or else where. Your son's daughter oryour daughter's daughter.Your father's sister,your mother's sister, and many more read the entire verses.
 
Tunavyoamini dini zote ni kwamba Mungu alimuumba Adamu halafu akampa usingizi mzito na baadaye kumfanya Mwanamke (Eva/Hawa) kutoka kwenye ubavu wa Adamu. Kwa maaana hiyo walikuwa wawili tu, lakini kwa sasa katika ulimwengu huu tuko mamilioni ya mwanaadam. Je huo uharamu haukuwakumba kizazi cha awali cha Adam na Eva/Hawa?
 
Ukiacha undugu wa damu, sheria pia inakataza kuolewa na mume wa mama au kuoa mke wa baba!

WOB,

Hili suala tukija kwenye masuala ya kisheria, sheria ya makosa ya jinai [Penal Code] ya Tanzania imeweka bayana kabisa ni kosa la jinai kufanya mapenzi na nduguyo awe kaka, dada, nusu kaka/dada, mama mzazi, mjukuu. Kwa maelezo soma vingigu vya hii sheria hapo chini:

Ukija kwenye masuala ya ya afya wanasema watoto wanaopatikana katika mfumo huu wanakuwa na matatizo ya utindio wa ubongo kutokana na masualaya inbreedings. Jaribu kufanya reserach kwenye jamii zile zinazooza ndugu wa karibu ( huwezi kokosa watoto wenye upungufu wa ukuaji wa akili)
Kwenye masuala ya utabibu na mengineyo kuhusu hii ‘dhambi’ soma hapa: http://en.wikipedia.org/wiki/Incest

158.—(1) Any male person who has carnal knowledge of a incest by female person, who is to his knowledge his granddaughter, daughter, sister or mother, is guilty of a felony, and is liable to imprisonment for five years: Provided that if it is alleged in the information or charge and proved that the female person is under the age of twelve-years, the offender shall be liable to imprisonment for life.
(2) It is immaterial that the carnal knowledge was had with the consent of the female person.
(3) If any male person attempts to commit any such offence as aforesaid he is guilty of a misdemeanor.

159. On the conviction before any court of any person of an Order for offence under section 158, or of an attempt to commit the same, guardian against any female under the age of twenty-one years, it shall be
In the power of the court to divest the offender of all authority over such female, and, it the offender is
The guardian of such female, to remove the offender from such guardianship, and in any such case to
Appoint any person or persons to be the guardian or guardians of such female during her minority or
Any less period: Provided that the High Court may at any time vary, or rescind the order by the appointment of any other personas such guardian, or in any other respect

160. Any female person of or above the age of 16 who with consent permits her grandfather , her father, her brother or son to have carnal knowledge of her(knowing him to be her grandfather, father, brother or son as the case may be)is guilty of a felony ,and is liable to imprisonment for five years.

161. In sections 158 and 160 the expressions "brother" and "sister", respectively, include half-brother and half-sister, and the provisions of the said sections shall apply whether the relationship between the person charged with an offence and the person with whom the offence is alleged to have been committed is or is not traced through lawful wedlock.
 
Ndugu kuoana ni mbaya lakini vipi kwa wale wasiojuana kama ni ndugu?

Kuna dada kaoana n akaka yake waliyeshangia baba bila kujuana maana mama zao walipata mimba halafu wakaolewa na watu wengine na mimba hizo zikawa za wababa waliowaoa yani waliwabambika watu wengine, walivyokuwa wakubwa, hao watoto wamepisha na miaka saba yaani mvulana kamzidi msichan miaka saba sasa walivyooana, mama zao kila mmoja kwa wakati wake akaamua kumwambia mwanae ukweli kwamba huyu siyo baba yako kila mmoja bila kujuana akamweleza mwanae ukweli na akampa maelekezo mahali baba yake alipo na jina, wakafunga safari mpaka hicho kijiji wakaenda kwanza kumtafuta baba wa msichana kufika yule msichana alishtuka yani huyo baba na mume wake wamefanana utafikiri mapacha mume wake ana kovu usoni na huyo baba analo, bai wakakribishwa yule dada akajieleza akamtambulisha mume wake sasa yule mwanaume akashangaa majina ya baba zao yanafanana si ikabidi na yeye ajieleze baba yao akawaomba msamaha akasema endeleeni tu maana mmeishafunga ndo na mlikuwa hamjuani sisi ndo wenye makosa.
sasa hapo kuna makosa kweli? na wale wamama walivyojua wakawaambia watoto wanyamaze maana wakisema ndoa zao zitavunjika kwa hiyo wanaendelea.

Wameshajuwana hao kuwa ni ndugu... hiyo ndoa si halali tena. Wakiendelea nayo watakuwa wanavunja sheria ya nchi na kidini pia (kama ni waumini)
 
Na hizi ndoa za watu wa jinsia moja zimeharamishwa wapi? Maana ni kama kaugonjwa sasa hivi humu mitaani tunamoishi. Naombeni verses tafadhali.
 
Tunavyoamini dini zote ni kwamba Mungu alimuumba Adamu halafu akampa usingizi mzito na baadaye kumfanya Mwanamke (Eva/Hawa) kutoka kwenye ubavu wa Adamu. Kwa maaana hiyo walikuwa wawili tu, lakini kwa sasa katika ulimwengu huu tuko mamilioni ya mwanaadam. Je huo uharamu haukuwakumba kizazi cha awali cha Adam na Eva/Hawa?

It was fine in those days during creation. Nevertheless, is biologically not ok marring brethren leave alone biblical and legal encumbrances.
 
Na hizi ndoa za watu wa jinsia moja zimeharamishwa wapi? Maana ni kama kaugonjwa sasa hivi humu mitaani tunamoishi. Naombeni verses tafadhali.
Zimeharamishwa katika Kitabu cha Mambo ya Walawi 18:22 inayosema:

"Nawe usilale na mwanamume kama vile unavyolala na mwanamke. Ni jambo lenye kuchukiza."
 
Back
Top Bottom