Ni ndoto kukomboa wanyonge wa Tanzania ukiwa ndani ya CCM

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
[FONT=ArialMT, sans-serif]Historia inatudhihirishia kwamba mkombozi wa watu ni mtu wa kujitolea. Ni mtu anayeweka maslahi yake pembeni na kuweka mbele maslahi ya wale anaotaka kuwakomboa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hivi ndivyo alivyofanya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fred Mpendazoe. Amedhihirisha kwa vitendo kwa kuihama CCM na kuacha maslahi yake ya ubunge. Kwa maneno yake mwenyewe, “Kwake yeye ukombozi wa wanyonge wa Watanzania ni muhimu kuliko hizo Shs. 45,000,000/= (ambazo anaweza kuzipoteza).”[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Baadhi ya viongozi wenzake wamembeza na kumshangaa kwa kitendo chake cha kuihama CCM, kwa kipindi hiki na kupoteza marupurupu lukuki. Hawa wote hawaelewi ukombozi unahitaji dhamira ya namna gani. Hawa wanafikiri unaweza kuweka maslahi yako mbele na kwa wakati huo huo ukawa mkombozi wa wanyonge. Hii ni fikira potofu. Haiungwi mkono na historia.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa Wakristo, ninatoa mifano michache ya wakombozi wa wanyonge. Kwanza, kuna Musa aliyewakomboa wana wa Israeli kutoka utumwani Misri. Yeye, japokuwa alikuwa Muisraeli aliyelelewa Ikulu ya Farao, akiwa kama mwana wa binti Farao, akihesabiwa kama mwana wa Mfalme.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati huo ilikuwa kujiandaa kuwakomboa ndugu zake, yaani Waisraeli kutoka utumwani, ilibidi aachie maisha ya kuitwa mwana wa Mfalme akikaa Ikulu, na kwenda Midiani kuishi maisha ya kawaida, akichunga kondoo. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Baada ya hapo, ndipo Musa akaonekana kwamba anastahili kuwakomboa ndugu zake kutoka utumwani na kuitwa na Mungu kufanya kazi hiyo. Bila ya shaka kuondoka kwake Ikulu na kwenda kuishi jangwani kwa kuchunga kondoo, ni kitendo cha kujitolea. Musa aliacha marupurupu lukuki. Na kwa kufanya hivyo, alifaulu kuwa mkombozi halisi wa ndugu zake.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mfano wa pili ni wa Bwana Yesu. Yeye aliacha kiti cha enzi huko mbinguni, akaja duniani kwa kuzaliwa kama binadamu wa kawaida na kuishi maisha ya taabu. Ni baada ya kujidhili au kujidhihirisha namna hii, ndipo Yesu alistahili kumkomboa binadamu kutokana na dhambi ya asili iliyowatenganisha wanadamu na Mwenyezi Mungu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika zama zetu hizi, tunaye Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Yeye aliacha kazi yake nzuri ya ualimu na iliyokuwa inamhakikishia mshahara mzuri kila mwezi, akiwa kama mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Pugu jijini Dar es Salaam. Alijiuzulu ualimu na kwenda kufanya kazi ya uongozi wa TANU, bila kipato cha uhakika.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kusema kweli, Mwalimu Nyerere kwa kufanya hivyo alijitolea sana. Na ni katika kufanya hivyo, ndipo aliweza kuleta uhuru wa nchi hii. Bila shaka kama angeweka maslahi yake mbele, pengine mpaka sasa nchi hii ingekuwa bado mikononi mwa wakoloni wa Kiingereza.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Nina hakika Mpendazoe amefuata dhamira ya viongozi niliowataja juu mpaka akafikia uamuzi wa kuacha mishahara yake ya ubunge wa miezi sita iliyobaki na pia kiinua mgongo chake cha mamilioni hayo ya fedha, baada ya Bunge kuvunjwa hapo Agosti mwaka huu. Haya yote siyo maslahi madogo. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lakini kwa kufikiria ukombozi wa taifa hili kutokana na mafisadi na waporaji wengine wote wa utajiri wa nchi hii, marupurupu hayo ni kidogo mno. Si kitu kabisa. Ninampongeza Mpendazoe kwa uamuzi wake huu wa kishujaa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mimi ninaamini, kwa yakini, kwamba Mungu lazima afanye mpango wa kuwakomboa Watanzania kutokana na umaskini na hali waliyomo kwa ujumla, kwa kuwaandaa watu kama Mpendazoe.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ninaamini kabisa kwamba Mungu hawezi kuacha watu wake wakaendelea kuteseka chini ya CCM, ambayo imeacha kabisa kuwa chama cha kutetea wanyonge na kuwa chama cha kutetea mafisadi, ambao wanaendelea kuiangamiza nchi hii kila kukicha. Wale ambao wanajidanganya kwamba wanaweza kuwasaidia wanyonge wa nchi hii wakiwa ndani ya CCM, wasahau kabisa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mfano hai ni suala la kampuni hewa ya Richmond. Mpendazoe na wenzake, ambao walikuwa mstari wa mbele na kujipambanua kuwa wapinga mafisadi, kwa kweli, walijaribu kuhakikisha kwamba wale waliohusika na kampuni hiyo ya kitapeli wanaadhibiwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Lakini walishindwa kabisa. Vigogo wote waliohusika na kampuni hiyo ilishindikana kuadhibiwa, licha ya kwamba walikuwa wanajulikana na mbali ya kubainika kwamba kampuni hiyo ilikuwa ikilipwa Sh. 152,000,000 kila siku, kwa kipindi cha miaka miwili (2), kupitia kampuni nyingine ya kitapeli ya Dowans.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Malipo hayo ya mamilioni ya fedha kwa siku ni kwa kampuni ambayo serikali ilikuwa imekiri kuwa wamiliki wa kampuni hizo walikuwa hawajulikani, ni kuliibia taifa hili mcha na kweupe.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kelele za Mpendazoe na wezake katika Bunge, na katika vikao vya CCM, kwamba wale wote waliokuwa wanahusika na wizi huu, waadhibiwe, hazikuzaa matunda yoyote. Sana sana ziliishia kwa hawa wapambanaji kuzomewa na wenzao kwenye vikao vya CCM na mtu kama Spika wa Bunge kutishiwa kufukuzwa CCM. Na mwisho wake Bunge likabariki kufungwa mjadala wa kashfa ya Richmond![/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Sasa katika hali kama hii, nani anaweza kusema kwamba anaweza kuleta mageuzi akiwa ndani ya CCM? Kama yupo atakuwa anajidanganya. Sana sana ataendelea kuwa ndani ya CCM ili kulinda maslahi yake na siyo kwa nia ya kuwakomboa wanyonge wa Tanzania.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa wale ambao ni wapambanaji wa kutetea maslahi ya wanyonge, ambao bado wako CCM, ninawaambia kwamba wanapoteza muda wao bure. Kwani CCM iliacha kuwa chama cha kutetea wanyonge tokea mwasisi wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alipoacha kuiongoza. Tokea hapo chama hiki kimekuwa kikitetea maslahi ya matajiri na siyo wanyonge tena.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hiki chama, tokea enzi za TANU, kilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi. Baada ya Mwalimu kuondoka kilitekwa na matajiri. Hawa ndio wanaelekeza nini kiamriwe kwenye vikao. Kama mjadala unakinzana na maslahi yao, lazima uzimwe. Hii ni bahati mbaya sana hapa kwetu Tanzania. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Tumejikuta katika hali kama hiyo wakati chama hiki cha CCM ndicho kinatawala. Ni chama ambacho kina wajumbe wengi katika Bunge, ambalo ndilo lingesaidia kuwasemea wanyonge. Vyama vya Upinzani vilivyopo havina sauti kabisa katika Bunge, kwa kuwa na viti vichache sana vya Wabunge. Hali ilivyo ni sawa sawa kwamba bado tuna utawala wa chama kimoja.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Sasa kama hiki chama kimoja kinachoshika hatamu kimeamua kuwa mtetezi wa matajiri, hali ya wanyonge na hatma yao itakuwa vipi?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hapa kwetu ni tofauti na Marekani. Huko kuna vyama viwili vikubwa. Kuna Republicans na Democrats. Chama cha Republicans kimejipambanua kuwa mtetezi wa maslahi ya matajiri na mabwenyenye, wakati cha Democrats ni mtetezi wa wote, yaani matajiri na wanyonge kwa ujumla.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hivyo, wanyonge wa Marekani wakiona maslahi yao yamesahauliwa kabisa na watawala wa Republicans, hukusanya nguvu zao kuwaondoa madarakani na kuwaweka Democrats madarakani. Hivi ndivyo ilivyotokea katika uchaguzi uliopita wa Rais wa Marekani. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wanyonge wa Marekani walichoshwa na sera za Rais Bush wa Republicans za kuangusha uchumi na kuendeleza vita ambavyo viliua watoto wao kila kukicha na hivyo wakaamua kukiondoa chama cha Bush madarakani na kumweka madarakani Rais Obama wa Democrats.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Matokeo yake mwaka huu, 2010, chama cha Democrats kimeweza kupitisha Sera ya Bima ya Afya, ambayo itawalinda watu wa hali ya chini, wasiopungua milioni 32.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Watu wa Marekani wamefanikiwa hivyo kwa vile kulikuwa na chama kingine cha kutetea wanyonge chenye nguvu. Hapa kwetu vyama vya upinzani ni vinyonge sana. Hali hii, bila ya shaka ndiyo iliyomsukuma Mpendazoe kuondoka CCM na kujiunga na CCJ, ambayo anaamini ina sera na uongozi unaoelekea kwenye ukombozi wa taifa letu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mwanzo utakuwa mgumu, lakini la muhimu ni kwamba kinachotakiwa ni sera nzuri na uongozi bora wa chama hicho. Hii itakuwa kama mbegu ndogo, ambayo ikishapandwa, yaweza ikazaa mti mkubwa wa ajabu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kama CCJ itakuwa na sera nzuri na uongozi bora, itakua na kuweza kuitoa CCM madarakani. Hivyo CCM isitambe kwamba haing’oleki. Hakuna utawala uliokuwa wa nguvu kama wa Warumi. Wakati ulipofika uliyeyuka. Huko Mexico chama kimoja kilitawala kwa miaka 70. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati ulipofika kiliondolewa na Bwana Fox, ambaye alikuwa anajulikana kama msema ovyo. Na hapa jirani yetu Kenya, kulikuwepo chama cha Kanu. Hiki chama kilikuwa na nguvu sana tangu kitawale nchi hiyo miaka ya 1960. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati ulipofika hata Rais Moi, aliyekuwa mtawala wakati huo, hakuweza kuzuia kuanguka kwa Kanu. Mpaka sasa Kamu ni miongoni mwa vyama vidogo vya upinzani huko Kenya. Kwa hiyo CCM ijue kwamba wakati ukifika itayeyuka kama Serikali ya Rumi ilivyoyeyuka au Kanu ilivyoporomoka.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hakuna haja ya Mpendazoe na wenzake kuogopa vitisho. Ninawashauri waendelee na dhamira yao ya kuwakomboa wanyonge wa nchi hii. Mwisho wa yote, ni ushindi kwao na anguko kubwa kwa CCM.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mungu ibariki Tanzania na watu wake.[/FONT]



CHANZO: NIPASHE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom