Ni ndoa au ndoana?

Ndoa ni Maridhiano/Mkataba kati ya Mwanamme na Mwanamke, ni lazima na common agreement kabla ya ndoa. Sasa ndoa ndio inapokuwa imefungwa bila maridhiano, kwa mfano pande moja haikuridhika kwa sababu fulani fulani basi hiyo ni batili mbele za Mungu na Kidini wanasema It never existed at first place its like a void contract
 
""" When a man steals your wife, there is no better revenge than to let him keep her." Lee Major

eeh!
 
..........Hapa naona watu wengi wanajadili kwamba wadada ndio wanalazimisha ndoa, hii wala sio kweli. Kuna wakaka nao pia wanalazimisha ndoa jamani, nina mfano tosha.
 
Mzee Mwanakijiji nionavyo ni muhimu sana kuingia kwenye ndoa ukiwa tayari na umeamua kutoka ndani ya moyo wako kuwa niko tayari sasa kuanza maisha ya ndoa,na kingine pia tusiingie kwenye ndoa ki-fashion,yaani kwa vile mwenzangu kavaa ngua nyeupe na mimi lazima nivae,sasa kama mtu kaingia kwenye ndoa kwa sababu hataki hiyo fashion impite tunategemea nini hapo? kuna mchangiaji mmoja amesema kuwa wengine huamua kuolewa au kuoa kwa kuondoa mikosi ni kweli hiyo dhana ipo pia kwa watu wengine,hivi mtu akiingia na dhana hiyo kwamba alienda kuondoa mkosi nini kinatokea hapo? au mwingine shida yake ni kuitwa tu MRS.

Nionavyo tunapoamua kuingia kwenye ndoa tuachane na dhana za kusema natoa mkosi,nataka kuitwa MRS na vitu kama hivyo, tujaribu kuangalia mbali,maana ndoa ina wigo mpana sana kuna ups and downs nyingi sana kwa hiyo tuwe makini sana pale tunapoamua kuweka commitment.

....UKIWA MAKINI SANA (Over Cautious) HUWEZI KUOA/KUOLEWA vile vile Usipokuwa makini ktk maamuzi yako,utakuja kujutia.
Msipo kumbushana kuoana hamtaweza kufanya hivyo au mtakujaoana na labda mkaanza kulaumiana,"dah tulichelewa wapi"?
 
Mzee Mwanakijiji nadhani mada yako imekujawakati muafaka, sasa hivi ndoa nyingi mtu unalazimika kuoa, sababu kubwa kwa mfano hapa DAR wachumba wengi wanaishi pamoja, au hata kama hawaishi pamoja wanakuwa tayari wanamegana tena bila kujikinga, matokeo yake ni mimba, binti akishapata mimba sasa anakuja na "BABA atasemaje" au MAMA ntamwambia nini lazima tufunge ndoa, au kama ulikuwa umeshatambulishwa ukweni sasa wakwe watakuambia kijana sisi tunataka ndoa hapa, tayari ushampa mimba binti yetu, na wewe labda hukuwa na mpango wa kuoa hapa karibuni, kweli utalazimika kuoa hivyo hivyo tuu au kama ni mgumu basi utabidi usubiri mpaka binti ajifungue ndo uoe, na wengine utakuta bado alikuwa anatafuta na hiyo imetokea sasa binti wa watu kanasa na wewe hukuwa na mpango wa kumuoa yeye, kwa pressure za wazazi wako na wake unabidi sasa uoe, hapo sasa ndani ya NDOA kunakuwa hakuna amani tena. AMBAO hampo kwenye ndoa jamani OA au uolewe na mtu ambaye you cant live without na si you can live with. Mambo hubadirika sana kwenye ndoa, pale ndo maisha ya kweli sasa kama ilizoea kutolewa kila siku sasa mitoko inaweza ikawa once in a month au ikafa kabisa, majukumu yanakuwa mengi hasa mkishapata mtoto, ukiwa na doubt flani ifanyie kazi kabla ya kuji commit, otherwise utakuja lia.

KUOA KABLA YA MUDA ULIOPANGA SIN JAMBO KUBWA,ISSUE INAKUJA JE ULIYEMUOA NDIYE HUYO ULIYEPANGA KUMUOA KESHO?
Kwenye shinikizo zipo nyingi,wengine wanapewa allowance mara wanapooa hapo ndo mtu kwa tamaa ya pesa anaoa tu ilimradi apate allowance.
 
KUOA KABLA YA MUDA ULIOPANGA SIO JAMBO KUBWA,ISSUE INAKUJA JE ULIYEMUOA NDIYE HUYO ULIYEPANGA KUMUOA KESHO?
Kwenye shinikizo zipo nyingi,wengine wanapewa allowance mara wanapooa hapo ndo mtu kwa tamaa ya pesa anaoa tu ilimradi apate allowance.
 
What is the maximum time to stay in a relationship before marriage? unakuta m2 mko naye miaka nenda miaka rudi kakuvisha pete ya uchumba mpaka ishakua ndogo, bado anakushughulikia tu! should I not remind him that time is going? Some Men!!! Grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!! to hell with you all.

dada ukali mbona..? ile hiyo "mpaka pete ishakua ndogo" imenichekesha hadi nafikiria kununua zile Xtra Large!
 
Ndoa ni agizo la MUNGU na haijalishi upo ktk imani gani au nasaba ipi. Na kikubwa zaidi ndoa ni wito. kama huna wito walah huoi na ukioa utaendelea kuwowa!

Nilipokuwa mtoto mpaka ujanani sikuwaza kwamba nitakuja kuoa ila sasa nipo ktk ndoa mwaka wa pili na maisha yanaendelea mbele. NO friction no acceleration
 
Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kuisha kwa manung'uniko. Ni heri mtu aoe pale ambapo amependa na kupendwa na mahali ambapo anajua kabisa kuwa ije mvua au jua watakuwa pamoja. Ni ndoa inayodumu pale ambapo wawili hao wamekubaliana kwa hiari kuwa pamoja. Furaha ya ndoa ya namna hiyo hupitishwa kizazi hadi kizazi kingine.

Ndoa ya kuvutana na kulazimishana huwa ndoa kwenye vyeti vya ndoa; ni msingi wa watu kutafuta kisingizio cha kwenda nje ya ndoa; ni leseni ya manyanyaso na kwa hakika huzeesha haraka na kusababisha magonjwa lukuki.

Kama lengo la ndoa ilikuwa ni kutimiza matakwa ya wazazi, kufuata mkumbo, kuonesha kuwa na wewe ni "wife material" au kwa namna yoyote kuhakikisha na wazazi nao wanaserebuka na kuimba "akanana" au "Sunda Sunda" au mambo ya kupigwa matarumbeta ya "anameremeta" basi yote yatakayotokea kwenye ndoa hiyo ni mastahili ya wana ndoa hao.

Kwa sababu kabla ya hayo yote (ambayo nayo bila ya shaka ni mema) maswali mawili yafuatayo ni lazima na muhimu yajibiwe:

a. Je tuko tayari kuanza maisha ya ndoa? - Tunaposema "Tayari" tunamaamisha kiuwezo, kihisia, kivionjo, kimaamuzi n.k Je tuko tayari kuwaacha wote na kuwa na huyo mmoja, kuwa tayari kudeal na watoto na mambo yanayokuja na kuanza na familia?

b. Je, ni huyo ndiye ambaye ungependa mzeeke pamoja? Hili swali ni muhimu. Wengi tunapofunga ndoa bado tuko vijana. Hivyo tunaangaliana kwa maumbo yaliyopendeza. Wenye rijali, big ego, mwanamichezo, sauti nzuri, macho mazuri, kifua kilichojaza na kaunta ya vinywaji n.k Hivi vyote ni vizuri wakati huu lakini je miaka 25 baadaye wakati mvi zimeanza kutoka, meno yameanza kugombania kung'oka, mtu kapaswa sidenti, mtoto mmoja kaaga dunia, kibarua kimeota mbawa n.k Je bado utataka kuwa na mtu HUYO katika maisha yako?

Ukijibu maswali hayo mawili bila kupepesa macho "Ndiyo" basi niite niwe mshenga.. unastahili kufunga ndoa.

Otherwise, stay your a..ss. outside marriage!!
 
John Edwards comes to mind....
 
eee, bibie usituchoshe, pete ikukubana unavaa kidole cha mwisho mguuni, mbona warembo wengi wamezishusha petezao. si ulikubali mwenyewe labda anakupima uvumilivu -- who knows!!???
 
What is the maximum time to stay in a relationship before marriage? unakuta m2 mko naye miaka nenda miaka rudi kakuvisha pete ya uchumba mpaka ishakua ndogo, bado anakushughulikia tu! should I not remind him that time is going? Some Men!!! Grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!! to hell with you all.

Kwani wewe kushughulikiwa hupendi? Inaonekana hakupi mautam,iweje useme hivyo?
 
Kwa sababu kabla ya hayo yote (ambayo nayo bila ya shaka ni mema) maswali mawili yafuatayo ni lazima na muhimu yajibiwe:

a. Je tuko tayari kuanza maisha ya ndoa? - Tunaposema "Tayari" tunamaamisha kiuwezo, kihisia, kivionjo, kimaamuzi n.k Je tuko tayari kuwaacha wote na kuwa na huyo mmoja, kuwa tayari kudeal na watoto na mambo yanayokuja na kuanza na familia?

b. Je, ni huyo ndiye ambaye ungependa mzeeke pamoja? Hili swali ni muhimu. Wengi tunapofunga ndoa bado tuko vijana. Hivyo tunaangaliana kwa maumbo yaliyopendeza. Wenye rijali, big ego, mwanamichezo, sauti nzuri, macho mazuri, kifua kilichojaza na kaunta ya vinywaji n.k Hivi vyote ni vizuri wakati huu lakini je miaka 25 baadaye wakati mvi zimeanza kutoka, meno yameanza kugombania kung'oka, mtu kapaswa sidenti, mtoto mmoja kaaga dunia, kibarua kimeota mbawa n.k Je bado utataka kuwa na mtu HUYO katika maisha yako?

Ukijibu maswali hayo mawili bila kupepesa macho "Ndiyo" basi niite niwe mshenga.. unastahili kufunga ndoa.

Otherwise, stay your a..ss. outside marriage!!

Mzee Mwanakijiji mimi nakujibu bila kupepesa macho,bila aibu wala woga,binafsi niko tayari kuingia kwenye ndoa kwa sasa,niko tayari kihisia,kiuwezo,na pia kimaamuzi,niko tayari kuwa mama wa familia na kubeba majukumu yangu kama mama,na hata mtarajiwa pia nimemwambia mimi niko tayari kuwa mama nitakaesimamia nyumba yangu kama mama.

Na kuhusu pia swali la pili niko tayari kuzeeka nae,na si kuzeeka nae tu,hata zitakapo jitokeza ups and downs niko tayari,maana naelewa kwenye ndoa kuna mambo mengi na changamoto mbalimbali,niko tayari kukabiliana na hizo changamoto,siku zote namwomba Mungu nitakapoingia kwenye ndoa anipe uvumilivu.
 
binafsi niko tayari kuingia kwenye ndoa kwa sasa,niko tayari kihisia,kiuwezo,na pia kimaamuzi,niko tayari kuwa mama wa familia na kubeba majukumu yangu kama mama,na hata mtarajiwa pia nimemwambia mimi niko tayari kuwa mama nitakaesimamia nyumba yangu kama mama.

Na kuhusu pia swali la pili niko tayari kuzeeka nae,na si kuzeeka nae tu,hata zitakapo jitokeza ups and downs niko tayari,maana naelewa kwenye ndoa kuna mambo mengi na changamoto mbalimbali,niko tayari kukabiliana na hizo changamoto,siku zote namwomba Mungu nitakapoingia kwenye ndoa anipe uvumilivu.

hongera na karibu kwenye chama chetu:)
 
Back
Top Bottom