Ni nani mzalendo na nani Mpinzani wa kweli?

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Ni nani mpinzani wa Kweli na Nani Mzalendo wa Kweli nchini Tanzania?

Wimbi la kuvurugana kwenye vyama vya upinzani bado linaendelea kuvitesa vyama hapa nchini!

Kina David Kafulila kufukuzwa, Hamad naye huko CUF vivyo hivyo hadi unajiuliza maswali mengi tu kama vile je hawa walifanya makusudi ama kwa kurubununiwa na kutumwa ili wadhoofishe upinzani kwa kisingizio cha kutoa siri za vyama vyao? Au ni watu kama kina Mbat** wanaosemwa ni NCCM ndio wanafanya kazi waliotumwa?

Huko CHADEMA nako sitashangaa kusikia baadhi ya viongozi wa juu huenda wana ajenda za siri kuhusu upinzani na mustakabali wake - na wengine wametuhumiwa hivyo

Frankly ukweli wa uzalendo na wa upinzani unabakia siri yako wewe moyo wako kama una uchungu na nchi yako na hatima ya wanyonge wa Tanzania inaendelea kuwekwa rehani kwa unafikli na maslahi binafsi ya wengi wetu ambao ni wasaliti!
 
Mzalendo wa kweli ni mtu mwenye uwezo wa kufikiria hadi kizazi cha saba (7th Generation) Mtu asiye mbinafsi na mwenye mawazo endelevu. Kwa wanasisa walio wengi hapa nchini wanajifikiria wao na familia zao tu na huo ndio mwanzo wa migogoro mingi ndani ya vyama vya siasa.
Mfano, Uundwaji wa katiba mpya ni kitu ambacho ni muhimu sio tu kwetu lakini pia kwa manufaa ya vizazi vijavyo, lakini kwa wanasiasa wengi ndani ya chama tawala wanahofia mslahi yao binafsi na hivyo kuudhoofisha mchakato wote wa uundwaji wa katiba.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom