Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Mara kwa mara tumekuwa tukisikia kauli kutoka kwa baadhi ya watu na asasi mbali mbali hapa nchini zinazo ashiria kwamba ni wao tu wenye hati miliki ya jina la 'Nyerere." Itakumbukwa wakati wa uchagizi mkuu uliopita, mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mara,ambaye ni mtoto wake marehemu Nyerere, alifunga safari kwenda wilaya fulani mkoani Mwanza, kwenda kumfunda shemeji yake aliyekuwa anagombea ubunge kwa tiketi ya CDM, kuacha mara moja kutumia jina la Nyerere, eti kwakuwa alikwisha achika. Na hivi leo kuna stori katika gazeti ya sirikali ya Habari Leo, inayomnukuu mmoja wawana familia akiwahasa CDM kuacha kupandia kwa mgongo wa Nyerere. Vile vile CCM na jumuiya zake imekuwa ikitoa kauli zinazo ashiria kwamba kwa maoni yake chama hicho kina hati miliki ya jina la Nyerere. Kwa maoni yangu Nyerere ni baba wa taifa la watanzania/ Tanganyika, hivyo wananchi wote katika ujumla wao ndiyo wenye hati miliki ya jina lake.