Ni nani huyu Lameck Madelu Mkumbo??

majorbuyoya

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
1,828
564
Natanguliza heshima kwenu wana JF!. Leo niliamua kuperuzi peruzi gazeti la Raia Mwema kwenye safu ya Maoni/Makala nikakutana na makala yenye kichwa cha habari kisemacho ''Nyerere angemkemea Dr. Slaa au CCM?'' ambayo imeandikwa na Arcado Ntagazwa.................. Ndani ya habari hii napenda nijikite zaidi kwenye paragraph moja ambayo mwandishi anasema:- ''Lakini, kwa mfano, mheshimiwa fulani anajua kuwa kuendelea kutumia majina ya kudandia kwa kughushi badala ya majina yake halisi ya Lameck Madelu Mkumbo, siku si nyingi yatamfikisha kwenye makosa ya kijinai. Wanasema ukitaka kuheshimiwa uanze kujiheshimu''..........mwisho wa kunukuu, nilikuwa napenda kufahamu huyu mheshimiwa aliyetajwa hapa kutumia jina lisilo lako wakati jina lake halisi ni Lameck ni yupi? je kwa nini atumie jina ambalo si lake kuna kitu gani anakificha na sheria ya nchi inasemaje katika suala kama hili?
 
Ni kada mwandamizi wa CCM, mjumbe wa kamati kuu na secretary ya CCM, Mbunge wa Iramba mashariki(?)

Anajiita/anaitwa Mwigulu Lameck Nchemba, jina ambalo anadaiwa na watu kadhaa hasa humu JF si la kwake!
 
Juzi Star TV walikua na kipindi maalum juu ya maisha ya huyu bwana.
Walionyesha mambo mbalimbali yanayomuhusu huyu bwana ikiwamo shule aliyosoma.

Zaidi zaidi walimuonyesha baba wa huyu bwana na wakamtambulisha kama Mzee Madelu!!
 
Kumbe ndioo yule mchumi wa daraja la kwanza. Kwanini aliamua kulikana jina la Baba yake mzazi na kutumia majina mengine?..........Kila mara tumesikia serikali ikiwachukulia hatua wanavyuo, wanajeshi, polisi n.k wanaopatikana na hatia ya kutumia vyeti ambavvyo sio vyao au vya kufoji, mbona huyu jamaa anaachwa kijinga jinga hivi huku akiendelea kujisifu kuwa ni mchumi daraja la kwanza?
 
CDM - jimbo la huyu jamaa ni lazima tulichukue by hooks or crooks!.. makamanda jitokezeni mtuwakilishe.
 
Naisubiria vita ya jimbo hilo kati ya Dr na Lameck!ushindi unajulikana ni w anani ila kuna upande mmoja utapambana na kivuli chake kumwaga mipesa ili hali wapiga kura hawatajali yote hayo!!
 
Kumbe ndioo yule mchumi wa daraja la kwanza. Kwanini aliamua kulikana jina la Baba yake mzazi na kutumia majina mengine?..........Kila mara tumesikia serikali ikiwachukulia hatua wanavyuo, wanajeshi, polisi n.k wanaopatikana na hatia ya kutumia vyeti ambavvyo sio vyao au vya kufoji, mbona huyu jamaa anaachwa kijinga jinga hivi huku akiendelea kujisifu kuwa ni mchumi daraja la kwanza?

Ndugu yangu HAKULIKANA jina lake na la Babaye, bali ALIFELI mtihani wake wa kwanza wa darasa la saba kisha AKARUDIA kwa jina lake la sasa, na baada ya kufaulu, hakuangalia nyuma kulirudia jinale la mwanzo!
 
Sheria za Tanzania si msumeno na hivyo hazikati kote kote, zipo kwa ajili ya kundi fulani la watu. Iba kuku wewe mtanzania wa kawaida utakwenda jela miaka 5 wakati wale wa Kagoda wenyewe adhabu yao ni kurudisha. Huwezi kuja kusikia ameshitakiwa kwa kufoji chini ya utawala huu tulionao, kamwe hilo halitatokea!
 
Labda lilikuwa jina la kusomea praimare jamani. Zamani ukifeli ulikuwa unaenda kurudia kwa jina la watoro wa shule.

exactly! Nadhani hata huyu Burn karudi alitumia huu mtindo wa zamani wa watu waliofaulu lakini hawana fedha kwa ajili ya kuendelea na masomo yalichukuliwa ama kununuliwa na watoto wa wenye fedha waliofeli hasa shule za primary, huu mtindo ulikuwa common sana zamani na ndio unaomfanya mama yangu kila siku analaumu nafasi yake kuchukuliwa na mtu mwingine kisa mama yangu hakuwa na uwezo wa kifedha kujiendeleza na masomo ya sekondari na mpaka sasa huyo mtu anatumia jina la mama yangu kwenye kazi yake lakini hana hata shukurani
 
Kumbe ndioo yule mchumi wa daraja la kwanza. Kwanini aliamua kulikana jina la Baba yake mzazi na kutumia majina mengine?..........Kila mara tumesikia serikali ikiwachukulia hatua wanavyuo, wanajeshi, polisi n.k wanaopatikana na hatia ya kutumia vyeti ambavvyo sio vyao au vya kufoji, mbona huyu jamaa anaachwa kijinga jinga hivi huku akiendelea kujisifu kuwa ni mchumi daraja la kwanza?

hata David Mathayo David amemkana baba yake Cleopa Msuya CCM ni laana tupu
 
Back
Top Bottom